Wednesday, February 24, 2010

TANZANIA INA NINI CHA KUJIVUNIA?

Je tumekosa viongozi wenye ubunifu?


Au tumekosa ardhi nzuri yenye rutuba na rasilimali?


Hii nimeidesa kutoka katika mtandao wa jamii Forum, imeandikwa na Mdau mmoja anayejulikana kwa jina la Dalali.
Kutokana na kuvutiwa nayo, nimeona sio vibaya wasomaji wa Blog hii ya Vukani nao wakiweka changamoto zao hapa, kwani huenda kuna jambo tukajifunza wote.

Wana JF,

Wiki iliyopita nilipata mtihani mgumu baada ya mgeni wangu ambaye namuheshimu sana alipoamua kunitupia suala ambalo sikulitarajia. Sijui yalimjia mawazo gani lakini wakati tunakaribia kuagana ghafla aliniuliza kwa kizungu "Are you proud of your country?"

Nilishusha pumzi na kupepesapepesa macho nikijaribu kutafuta jibu la haraka nikashindwa.
Kwa vile ni mtu ninayemuhesimu sana, sikuweza kumtoa njiani au kumdanganya.
Nilijaribu kuwaza mambo ambayo naweza kuyaita yakujivunia nikashindwa.
Kila kilichokuwa kikija mawazoni mwangu kilikuwa si cha kujivunia bali cha kutia uchungu.
Mambo yaliyonijia haraka yalikuwa kama:-
rushwa iliyopindukia mipaka, - viongozi mafisadi, wezi waliojaa kila sekta na taasisi za serikali ambao hujitajirisha kwa kila nafasi anayoipata mtu,

- miaka karibu 50 ya uhuru hatuna hata umeme wa uhakika,
- watoto wanakaa chini mashuleni na hakuna kinachosomeshwa,
- mahospitali hayana madawa,
- barabara yo yote inayojengwa au kufanyiwa ukarabati basi ni kwa pesa ya msaada,

- tumeshindwa hata kujilisha licha ya kuwa na ardhi ya kutosha ambayo kama ikitumiwa kitaalamu tunaweza kulisha eneo kubwa la Afrika

- hata kuvua samaki tukala sisi wenyewe na kusafirisha tumeshindwa licha ya kua na eneo kubwa la bahari,

- hao tunaoambiwa ni wataalamu wetu hawana hata kitu kimoja walichovumbua,

- tumefanya mageuzi ya kutokana na udikteta wa chama kimoja tumeshidwa.Demokrasia imeshindwa kupiga hatua.Vyombo vyote vya dola vinafanya kazi na kutumikia chama tawala na hata uchaguzi ukifanyika ni mizengwe mitupu,
- hata kwenye mambo ya michezo ni aibu tupu. Tunashindwa hata kuingia kwenye mashindano ya kombe la Afrika.Mwisho ilibidi nimeze mate machungu nimjibu,
"NO, I'm ashamed".
Dalali

7 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Sina jibu la haraka! Labda tujivunie KUWA na RASILIMALI lukuki zinazoibwa kirahisi!

ILA kwa UHAKIKA tunakosa VIONGOZI wenye DIRA. Tulionao ni kanyaboya ambao wanasubiri waambiwe kila kitu na wakoloni.

Hata jambo ambalo linaonekana ni baya kwao wao watafurahia...Hujashangaa mtu anatoa kamsaada kadogo halafu bwana mkubwa anasema kuwa msaada huo umikuja wakati MUAFAKA?

kwa hiyo tunaongozwa na watawala wa WAKATI MUAFAKA :-(

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ina Koero Mkundi! Anayebisha aseme.

Mzee wa Changamoto said...

Tumekosa WANANCHI WANAOJUA NINI WANATAKA NA VIPI WATAPATA WATAKACHO hata kama ni kwa kumaanisha kuwang'oa madarakani waliopo.
Tumekosa UZALENDO na TUMEJAALIWA UNAFIKI

Anonymous said...

Miss Mkundi, ningependa kuhitilafiana kidogo na waheshimiwa hapo juu. Nadhanani nchi yetu, japo inamapungufu mengi, lakini tukijilinganisha na nchi nyingine za Africa, haswa majirani zetu, nadhani tunayo mengi tu ya kujivunia.
Kwa mfano, pamoja na ups na down zetu (Zanzibar) tumeweza kufanya political transition kwa amani kuliko majirani zetu kama vile Kenya, Rwanda, Burundi, Congo nk.
-Tumeweza kudumisha amani, umoja na mshikamano licha ya kuzunguukwa na majirani wenye matatizo mengi ya kisiasa.
- Kiswahili kimeendelea kutuunganisha na kutupa heshima dunia kote, ingawa hivi karibuni watu wengi wameonyesha kupendelea kiingereza zaidi. Binafsi hili sikubaliani nalo. Ukilinganisha na majirani zetu ambao ENGLISH ndio lugha yao kubwa, lakini kujamii, hawakawii krukiana kwenye KOO.
Watanzania we are still the coolest CAT out there because of our CIVILITY NA USWAHILI WETU. Ukitaka kuhakikisha haya ninayoyasema, go hang out na WAKENYA (kikuyu na Jaluo)ndio utaelewa ninachoongelea.
Kiuchumi na kupambana na umaskini, well hapa nadhani hakuna cha kutetea, kwani nchi bado inaendelea kustruggle, na ninaamini kwamba inabidi mambo mengi yabadilishwe ili tuweze kujikwamua na hili tatizo. Ukiangalia kwa ujumla, nchi zote ambazo zilikuwa zinafuata siasa za mrengo wa kushoto, hata zile ambazo zimeishaingizwa kwnye umoja wa Ulaya, bado pia zinatembea mwendo wa kinyonga kiuchumi. Kwa Tanzania itatuchukua muda mrefu kidogo kwa sababu ya RUSHWA SERIKALINI, UZALENDO MDOGO, UZEMBE,NA UKOSEFU WA NIDHAMU KWENYE UCHAPAJI KAZI.
Tanzania tuna cha kujivunia kwa sababu ya WAZALENDO KAMA WEWE KAERO MKUNDI; YOU ARE DOING A HECK OF A JOB KUELIMISHA UMMA WA WATANZANIA KUHUSU HAKI ZAO. Wewe na mablogger wengine (TZ Civil Society)mnafanya kazi kubwa sana, lakini itabidi muongeze bidii kuwaelimisha WANANCHI ili waweze kutumia nguvu waliyonayo wakati wa UCHAGUZI.
NI SISI WAPIGA KURA NDIO TUNAOCHAGUA VIONGOZI WABOVU, NA AMBAO WANAKUJA KUTUDHURU KWA MIAKA MITANO, KABLA YA KUPEWA HAKI YA KUCHAGUA TENA.

SIMON KITURURU said...

Mmh!

Markus Mpangala said...

George Bush alifanya uhalifu wa kivita kiasi ambacho uchunguzi unaonyesha anavyo vigezo vyote kwenda jela The Hague.
Pamoja na mambo mengine kashfa ya WATERGATE ya Rais Nixon... nina hakika hakuna Marekani atakye sema NO I'M ASHAMED.

suala la kujivunia nchi hakuendani tu na mambo hasi ya rushwa,ubadhirifu n.k

KUJIVUNIA NCHI YAKO NI MADA PANA SANA.
uSWISI NI MAARUFU KWA KUWEKA PESA ZA MAFISADI NA WANAJUA KUWA PESA NI ZA WIZI LAKINI HAKUNA raia atakaye chukizwa na hilo halafu asijivunie nchi yake.

JIBU la huyo msheshimiwa eti hakuona la kujivunia kwangu ni hadithi za kusadikika, sitakaa nijivunie nchi nyingine zaidi ya Tanzania na uovu kadhaa uliopo. Endapo rushwa imeshamiri wa kulaumiwa ni wananchi wanaochagua viongozi wezi kwahiyo ni kamba TUONE AIBU KWA UCHAFU HUO LAKINI siyo kwa kutojiuvunia nchi yangu. Huwezi kujivunia nchi kwa au kutojivunia kwa kuangalia tu masula la siasa. Wakati Chavez alipmweleza ukweli Rais Bush tuliona siku ya pili maandamano na kuambiwa aondoke, je ilimaanisha nini kwa ilivyokuwa.

Kuikana nchi yako kwa swali la mgeni au mheshimiwa yoyote ni hoja dhaifu bora aseme tu haijiskii kuwa Mtanzania, usifikirie kila mmoja nafurhia hali iliyopo lakini haiwezi kuniondoa kujivunia nchi yangu. Kilichoulizwa kililenga uzalendo kwanza, kabla ya kero na mahangaiko

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___