Sunday, February 14, 2010

MSIONE KIMYA JAMANI NIKO HUKU ARUSHA..........

Katika pitapita zangu katika mji wa Arusha nikajikuta niko humu, jamani kublog Raha kweli

Jamani msione kimya niko huku Arusha nakula Valentine Day, niliondoka huko Dar, leo alfajiri na namshukuru mungu nimefika salama. Nitakaa huku kwa majuma kadhaa nikishughulika na masuala ya kifamilia, huenda nikaadimika mtandaoni, lakini nikipata muda nitatembelea Vibanda vya mtandao kuperuzi na kupata habari mbalimbali kupitia vibaraza vyenu na kama nitapata fursa nitaendeleza libeneka kama kawaida.


Basi mwenzanu nilijua huku hali ya hewa ni Baridi nikabeba nguo nzito, Duh, kuna joto bala kama Dar, hivi kesho lazima niamkie madukani kufanya manunuzi ya nguo za joto kabla ya kueleka Karatu kuchapa kazi, maana huku niko kwenye kampeni ya KILIMO KWANZA.

8 comments:

Candy1 said...

Poa sie tupo dada Koero and stay safe...na ninavyojua mie Arusha baridi inakuwa ile miezi ya kati kati ila sasa hv it shud be warm

Yasinta Ngonyani said...

namshukuru mungu kama umesafiri salama. happy valentines day. Erik ana sema:- Ha det bra på alla hjärtans dag!!!

kibunango said...

Kila la heri kwa wakati wako wote utakao kuwepo hapo Arusha. Aidha wasalimie wote huko.

Anonymous said...

Ni nani unayekula naye Valentine huko??? Twamwonea wivuuuuu!!!!

Koero Mkundi said...

Anony, usione wivu, nimekula VALENTINE DAY na mdogo wake EDO NDAKI......LOL

SIMON KITURURU said...

kila la kheri Da Koero!

Markus Mpangala said...

SHIBE MWANA MALEVYA NJAA..........

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___