Wednesday, March 23, 2011

KWA HILI, WACHINA WANASTAHILI PONGEZI

Huwa tunawalaumu Wachina kutokana na bidhaa zao kuonekana hazina ubora lakini kwa upande wa Yebo Yebo nawafagilia, kwa mfano watoto hawa, wote wametinga Yebo Yebo na ambazo kwa kweli bei yake ni rahisi kuimudu hata kwa familia zenye kipato kidogo. Na zinasaidia sana kwa watoto kuchezea na kuepuka kuchomwa na miiba au kuingiwa na funza kwa wale wanaoishi maeneo yenye funza kama vile kule Sambaani Lushoto. Hapa watoto hawa wakiwa wamepozi kinamna
Na hapa wakifurahia MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI……LOL

2 comments:

Simon Kitururu said...

Wako katika umri mzuri kweli - ule umri ambao mengi ya letwayo na ukubwa hawayajui bado!


Ila kwa hali inakoenda sasa hivi mpaka watoto watajifunza RUSHWA ni nini na ni nini ufanye ili uwefisadi ufaidiye NCHI.:-(

Fadhy Mtanga said...

safi sana.. Hivi umewaza nini?

Yeboyebo pouwa sana aisee. Unaivaa kama ndala uendapo bafuni. Kisha waivaa kama kiatu cha wazi (sandals) kwenye mtoko.

Kweli maisha bora haya!