Sasa hivi neno Mafisadi limetamalaki katika midomo ya watanzania wengi, wakizungumzia ubadhirifu wa viongozi wetu waliowahi kushika madaraka makubwa au walioko madarakani.
Ni kweli kuna hali kama hiyo, lakini kwa kuangalia viongozi wa nchi duniani, hatuwezi kujifananisha na nchi za Asia, Latin Amerika au Ulaya, kwani nchi hizo nazo zimewahi kuwa na viongozi wabadhirifu, wala rushwa na mafisadi, huku Afrika ikiwa na viongozi wawili tu kati ya viongozi kumi waliotajwa.
Kwa kuangalia kiwango cha fedha ambazo viongozi wameiba au kuchukua kwa njia zisizo halali anayeongoza kwa fedha nyingi haramu ni aliyekuwa Rais wa Indonesia, Suharto, ambaye aliiba kiasi cha dola za marekani kati ya Bilioni 15 mpaka 35.
Wa pili ni Ferdinand Marcos wa Phillipines ambaye aliiba kiasi cha dola za Marekani kati ya Bilioni 5 hadi 10.
Mobutu Sese seko wa iliyokuwa Zaire ambayo sasa hivi inajulikana kama Congo DRC, huyu anashika nafasi ya tatu kwa viongozi wabadhirifu duniani.
Huyu alikomba kiasi cha dola za Marekani Bilioni 5.
Sani Abacha wa Nigeria naye alikomba kiasi cha dola za Marekani kati ya 2 hadi 5.
Slobodan Milosevic wa Serbia na Montenegro alijitwalia kiasi cha dola za Kiamrekani bilioni 1.
J C Duvalier wa Haiti alijichukulia dola za Marekani milioni 300 hadi 800.
Albert Fujimori wa Peru alikwiba dola za Marekani milioni 600. Pavlo Lazarenko alijichotea dola za Marekani kati ya milioni 114 hadi 200
Arnoldo Aleman wa Nicaragua alihamisha dola za Marekani milioni 100, na Joseph Estrada alichukuwa dola za Marekani kati ya milioni 78 hadi 80.
Kwa hiyo sio kweli kwamba Afrika ikiwemo Tanzania ndio tu inayonuka kwa ufisadi.
Je wadau mnasemaje?
JAFO AIPONGEZA TBS KWA KUANDAA TUZO ZA UBORA KWA WAFANYABIASHARA NA
WAJASIRIAMALI
-
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo (Mb) ametoa rai kwa
Wazalishaji wa bidhaa Nchini kuweka kipaumbele suala la ubora wa bidhaa
kwani ndio aje...
1 hour ago
5 comments:
Dada yangu,hudhani kwamba inawezekana kwamba mafisadi wetu wamechuma kiasi kikubwa zaidi ya hicho?IPTL wanalipwa dola ngapi kwa mwezi,na wameanza kupewa fedha hizo lini,na hadi itapobainika wamepewa kiasi gani....vp kuhusu richmond waliokuwa wanachukua shs milioni 150+ kila siku (na hizo ni data tunazolishwa kufurahisha masikio yetu,pengine ni kiwango kikubwa zaidi)...na je hadi anakufa,kuna yeyote anayefahamu utajiri wa Ballali?Hapo BOT zimeshaliwa dola/shilingi kiasi gani kabla ya ishu ya EPA kusikika?
Tatizo la uhakika wa kiwango cha fedha inayoibiwa liko zaidi kwenye ukweli kwamba ni hadi mtu anapokamatwa na kidhibiti ndio mnafahamu thamani ya alichoiba.Je vipi kama kuna nyingine ziomefichwa mahala flani?Na hawa mafisadi sio wajinga wa kuweka mali zote katika majina yao.Huenda hata huyo Abacha alikuwa na utajiri mkubwa zaidi ya huo "aliokutwa nao".
Je wewe binafsi unaamini kwamba Tanzania hakuna mafisadi kwa vile tu hatuko kwenye 10 bora?
sjui kama sisi tunaowaongelea mafisadi sio mafisadi wakkubwa zaidi kwa sababu ndio tunaowapa hao mianya ya kutuongoza kifisadi zaidi.
katika utambuzi tunasisitiza kujikagua na kujisahihisha kabla ya kuwakagua na kuwasahihisha wengine.
soma hii juu ya dini
toka lini dini zikawa na lengo tofauti na biashara na kutawala watu kiroho? nani kakwambia ukristo wa leo una maana halisi ya ukristo? nani kwa kwambia upuuzi mnaoufanya makanisani kwenu una harufu ya ukristo?
acheni ujinga, tafuteni ukweli na kweli imo ndani mwenu sio kanisania na nyie ndio kweli yenyewe. mwapotola mkiitegemea kutoka kwa matapeli wa kiroho na kimwili
Ahsante sana Kamala kwa mchango wako.
Naomba nichukue nafasi hii kuwafahamisha wasomaji wangu kuwa hakuna mada ambayo nimeifunga, mada zote nilizoweka hapa ziko wazi kwa hiyo nakaribisha wasomaji muendelee kutoa maoni yenu kwa sababu huwa napitia mada zote nilizoweka humu ili kuangalia kama kuna wachangiaji wapya.
Kwa mfano, bado kuna mjadala mzito unaendelea kwenye ile mada ya
"Je Msomi hasa ni nani?"
Kama unataka kuendelea kuchangia unakaribishwa maana mada imefikia patamu hasa.
Hata hivyo si vibaya kama mkipitia na kusoma chanagmoto za wale waliochangia.
Wote mnakaribishwa..........
Namna ambavyo wananchi wa nchi fulani wanavyokabiliana na athari za ufisadi na ubadhirifu wa fedha ni tofauti kabisa. Kwa mfano, wananchi wa Indonesia ambapo ndiko alikotoka fisadi mkubwa kabisa, yawezekana hawaexperience madhara ambayo sisi tunakumbana nayo kutokana na ishu ya ufisadi., pamoja na kwamba nchi yetu haijatokea kwenye hiyo chati.
Binafsi naweza kusema kwamba ufisadi na ubadhirifu wa pesa katika nchi yetu ni wa kupindukia na unaofanywa kwa ustadi mkubwa kabisa kiasi kwamba inakuwa vigumu kutambua.
Ishu hizi za ufisadi zilizoibuka yawezekana zilikuwa zikizimwa kwa muda mrefu lkn ilifika mahala maji yakazidi unga na ikalazimika kuweka hadhani. Hivi kweli kupotea kwa mabilioni yote hayo,kweli serikali isigundue! Hapa napata mashaka kuwa kuna ishu nyingi tu tena kubwa zaidi ambazo hazijafichuliwa.
Umasikini ambao watanzania wengi tunakabiliana nao unachangiwa sana na hali hii ya ubadhirifu wa pesa na rasilimali. Mbinu tofautitofauti ktk kukabiliana na hali hii ya umasikini ndio imepelekea kwenye hali hii mbaya sana inayopelekea maalbino kuwa katika hali ya hatari wakati wote pamoja na ujambazi uliokithiri.
Dada Koero pamoja na wanablog wote karibuni sana kwenye kibaraza changu tujadiliane
Niliwahi kubishana kwa hoja na Victor Katabaro kupitia RAI kuhusu jambo hilo, kwani alikuwa akitetea kwamba siasa siyo wizi. SAWA hawa walikwiba kama mtu wakati kwetu waliiba kwa kutumia kundi/jopo na linajuana. Sasa ukiniambia waliorejesha siyo mafisadi nashangaa na ukisema wasiorejesha ni mafisadi napigwa na butwaa. Kweli toka gavana mkuu wa BOT hadi kitengo cha EPA kuna maafis wandamizi wangapi ambao hawakuona/kuachilia wizi ule? ndiyo maana nasema kesi za kiustu kama filamu ya A TRIP TO THE MOON, igizo kali sana au hata la akina Maramba na Yona ni igizo kama la EGOLI/SUNSET BEACH yaani kichekesho sana. Lakini jambo la msingi ni uchumi wa nchi na kama TZ na wizi wa mafisadi walioufanya. Je fisadi ni nani, kumbuka ile stori ya kazi na yule mzee aliyelipia chumba!!! tafsiri ya mafisadi wamevaa sura nyingi.
samahani kwa leo, napumzika kidogo nasikiliza nyimbo za kinyanja- Malawi 'kondakta nirudishie pesa zangu".
Post a Comment