Sunday, January 18, 2009

MADA YA MSOMI HASA NI NANI? MAONI YA MARKUS MPANGALA

Wasomaji wangu wapendwa toka jana nilikuwa shamba na kule hakuna mtandao kabisa, ndio nimerejea na kukutana na maoni ya wasomaji wangu wapendwa, wakiendelea kutoa changamoto zao.
Miongoni mwa maoni niliyosoma, nimevutiwa sana na maoni ya kaka Markus Mpangala, naomba kwa ruksa yenu niyaweke hapa barazani bila kuhariri chochote.

Jamani kila nikitaka kuweka mada nyingine nakutana na changamoto zinazonivuta niendelee na hii mada, kaka Markus kauliza swali, nitamjibu.

Jumanne siku ambayo Rais mteule wa Marekani Bwana Barrack Obama ataapishwa nitaweka msimamo wangu juu ya hii mada, lakini sitaifunga.

Ujumbe maalum kwa mwana blog mpya KISIMA: Kaka juzi nilikutembelea nikataka kutoa maoni yangu lakini blog yako sijui umeiset vipi pale tunapoweka maoni, maana nimeandika maoni yangu nikashindwa kupost, naomba msaada tafadhali.

Sasa naomba musome haya maoni ya kaka Markus Mpangala hapa chini:

********************************************************************************************************************************************************
Hakuna matata mmepakua sana, sina nyongeza ngeni. Lakini mfano Jenerali Ulimwengu anahimiza kuhusu usomi wa wananchi katika mazingira yao, ni sawa na kile akisemacho Jean Jacques Rousseau kwamba kusoma ama kupata elimu lazima kuendane na mazingira. Kwanu naamini kwamba iwapo mtu akimaliza darasa la saba halafu akawa na ujuzi ambao nchi yake imetengenezea mazingira ya kuwa mjuzi zaidi wa kile akijuacho basi ataitwa msomi kwani tayari yupo katika utaalam/fani fulani. (soma UJAMAA NI IMANI cha J.K NYERERE). swali linabaki


USOMI ni nini hasa? hata kama mtu atakuwa kama kaka Everist na kupakua ujuzi ughaibuni, je dhana ya VX ni usomi au tafsiri juu ya mwonekano wa kisaikolojia kwamba aendeshaye hayo ni msomi? Huyu msomi ni yupi hasa? Ikiwa dhana ya usomi inaendana na kukaa darasani kisha ukaongeza ujuzi, vipi wale wasioingia darasani halafu wakawa na upeo mkubwa kuliko wasomi ambayo hutumia upeo wa wale wasioingia darasani? Sacrotes au?

Utakuta dhana hii ndiyo asemayo Nelson Mandela nataka kutambulika kama Mandela na siyo mtu aliyesoma na kujaza maktaba ya vitabu ambavyo vinamfanya aelewe kile anachokielewa bila kuwaelewesha wengine. Lakini swali hicho anachokielewa ni nini? Sawa twaweza kusema ni ujuzi wake wa fani fulani.

Mfano wapo wasomi wa masuala ya umeme lakini tuna mafundi wangapi wasiopita darasani kuongeza upeo? Je iwapo kutumia taaluma vibaya haina faida kwa jamii? kuna nadharia za faida ya uhalifu ya CRIMENOLOGY(nimesahau waandishi wake ila wapo wawili). Wao wanasema uhalifu ni jambo zuri sana kwani linaleta jamii yote pamoja na kushirikiana. Iwapo uhalifu unatokea katika jamii, kila kundi linatoa suluhisho kuhusu kukomesha uhalifu hata kama jamii hizo zinatofautiana ktk madaraka. Sasa mimi nauliza hivi, umewahi kusikia kitu kinaitwa WADAU? je hao ni nani? na ikiwa wasomi wanafanya utafiti wa jambo fulani, halafu wanawauliza wasio wasomi kupata mawazo yao na ufahamu wao kuhusu jambo wanalolichunguza. Mbona tunakuta kuna mambo wasomi hawayajui kabisa na wameyapata toka kwa wasiosoma.

Je msomi ni nani? katika uhai wake Sacrotes aliwahi kuwasha kurunzi(kama sijakosea) mchana na kuvinjari sokoni. walimcheka lakini akasema chekeni kuna watu wapo gizani ingawa mwaiona nuru. Je huyu alikuwa msomi kiasi gani wakati darasa halikufikia uzamili? Tunapotumia muda kublogu, wakati huohuo tunajuzwa kuna mtoto wa miaka kumi nchi afrika kusini anablogu; habari tamu hii, je utaalam wetu nao ni usomi?

Usomi ni ujuzi wa kitu fulani? sasa msomi huyu ni yupi? aliyekaa darasani na kuongeza ujuzi yule aliyebuni kitu bila kukaa darasani? Bado najifunza sijui msomi ni nani, ikiwa wasomi wenyewe wamekabidhiwa nchi kuongoza lakini wamekuwa vipofu waonao? Je hakuna anayejua kwamba tuna makatibu wa wizara wasomi halafu wanaingia mikataba ambayo asiyesoma kama Markus anahoji uelewa wa wasomi?

Je tutaendelea kupiga ramli kwamba msomi anayetegemewa kujaribu kuondoa umasikini lazima awe mjuzi wa kuandika mipango ya kuombea ngawira ughaibuni? Au msomi kama Profesa Ali Mazrui? Kumbe usomi hauna ubongo wala akili ya ziada bali ni kama nomino ya dhahani tu. Basi tukabli maneno ya kocha Jose Mourinho kwamba ukishindwa au kutojua jambo fulani basi jichukie.

Iweje wewe msomi mwenye Uporofesaaaaaa halafu utengenezewe simu na asiyesomea utengenezaji wa simu yenyewe, lakini unaamini ni mtaalam? Je utaalam na usomi ni tofauti?Koero swali hilo hapo: UTAALAMU WA JAMBO/FANI na USOMI ni tofauti? Je yule unayempelekea kutengeneza gari/baiskeli/simu n.k ni msomi kiasi gani? alikaa darasani?

Haya napumzika na wimbo wa miondoko ya KWAITO wake MANDOZA uitwao 'MYEKE BABA' unahusu usitumia nguvu kumpata mlimbwende panga hoja zenye mwitiko

January 17, 2009 10:55 AM

6 comments:

Shabani Kaluse said...

Koero naoan mada inaendelea kuleta changamoto.
Mimi sina maoni, maana naona walionitangulia wamesema mengi.

Nasubiri huo msimamo wako ambao umeahidi kutuwekea hapa kesho ili tujue umesimamia wapi.

Dada Koero nina swali ambalo liko nje ya mada hii.

Juzi nilimtembelea kaka Mpangala, usishangae unajua hizi blog zinawakutanisha watu.

Basi katiaka mazungumzo yetu tulijadili mambo mengi kuhusiana na hizi blog zetu, na hapo ndipo lilipokuja swali; Eti hivi ni kwa nini blog yako umeeiita VUKANI?

Je hili neno lina maana gani na linapatikana katika lugha gani?

Tunaomab majibu yako, kwa faida ya wasomaji wengine.

Ahsante kwa kutufikirisha.

Koero Mkundi said...

He! inaonekana hicho kikao kilikuwa ni kizito, hapa mzee wa utambuzi Kaluse na pembeni kuna Markus Mpangala mzee wa ziwa nyaza.
Vipi mlijadili hayo au na mengine?

Ok, swali lako kaka Mtambuzi nimelipata.
Ukweli ni kwamba nimekuwa nikiulizwa swali hilo na marafiki zangu wengi walionizunguka, na nimekuwa nikiwajibu, lakini kwa sababu umeuliza hili swali hapa kwenye blog, basi na mimi nitakujibu humu humu.

Naomba nitangaze dau la Lunch for two pale Kilimanjaro Kempinsky Hotel kwa wale watakaojaribu kutueleza maana ya neno VUKANI kabla sijawekaa majibu humu.

haya kazi kwenu wadau nasubiri majibu yenu.NB:si lazima zawadi iliyotajwa itolewe na muhusika bali ni hiyari yake mwenyewe.

Markus Mpangala said...

Duh! hii kali sana! kaka Kaluse! upooo?
Ni hivi, kuhusu mazungumzo bali ni soga,gumzo na mseto wa mambo ya blogu. Najua sijawahi kuuliza hili swali kuhusu VUKANI maana nilikuwa nawaza kwahiyo ikabidi nimwulize swali hilo mtambuzi.

Mazungumzo yalikuwa katika huduma za Agriggator/bloglines,NeoCounter na huduma za bure za blogu zetu. Sasa mada ilianzia katika binadamu na nyani ni tofauti? basi bwana tukakumbushana kuhusu hii mada, kisha tukazama katika falsafa za kaka Simon na mawazo ya Bwaya. Yapo mengi na tukajadili kuhusu wanablogu wenzetu mambo kadhaa ya kubadilishana, tukamwonea WIVU dada SUBI na Nukta 77 yake maana ni nzuri sana, tukajiuliza je nasi tutapakua zetu kama Jikomboe?

Hapo ndipo nikakumbuka swali kuhusu VUKANI, siyo siri kwani nimelipenda jina halafu sijui maana yake, lakini kwakuwa umeweka shindano basi tuawaachie wajuao. jamani tupeni jawabu nina HAMU SANA!

Markus Mpangala said...

Samahani Koero nimerudi tena. Kuna jambo nilisahau kulisema jamani. Ni hili: Hivi tunakijua chuo cha BAREFOOT? yaani BAREFOOT COLLEGE! kwa taarifa yenu kitafuteni muone vituko vya elimu na usomi tunaoujadili. kama sisi wanablogu hatuna sifa ya kujiunga. Wewe Koero hutakiwi kwani hutoki kijijini na una vyeti vya elimu. kitafuteniu hicho muone mambo. gonga hapo google watakupatia jibu la sifa za chuo.

nampumzika kwa wimbo wa NKALAKATHA wa MANDOZA akiisifu nchi yake.

EVARIST said...

Msomi,Mtaalam,Mjuzi,nk,nk...hivi hatuna mwenzetu hapo BAKITA atusaidie kidogo?Je hakuna mwenzetu mwenye kamusi ya Kiswahili Sanifu itusomee ingizo MSOMI?
Mzee Mpangala nimekupata,lakini sina hakika kama mtu ambaye hakuenda shule KABISA halafu akatokea kuwa MJUZI katika kutengeneza simu (kwa mfano) anaweza kuitwa MSOMI.
Dada Koero,kabla ya kufunga mjadala naomba ufanye jithada ndogo tu ya kutafuta kamusi ya kiswahili sanifu inasemaje kuhusu neno MSOMI.

Subi said...

Markus nilikuwa sijakusoma hapa kabisaaaaa, shukrani kwa kutaja nukta77 kuwa blogu nzuri (nadhani kwa mwonekano), kazi ipo katika kuweka posti zenye maana na faida, na kwa hilo la pili kwa kweli linahitajika chekeche zuri sana maana blogu ni nyingi zenye mada nzuri za kufunza, kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha jamii nzima! wachilia mbali zile zenye kutia watu njaa kila wanapozitembelea mara leo samaki, kesho ugali, keshokutwa matunda basi tu alimradi Markus unajua sana kulazimisha wenzio wapate njaa kwa picha na maelezo yako!
Koero, una mada za kukuna kichwa mdogo wangu.