Saturday, January 31, 2009

NIMEZISHITUKIA OFA ZA WANAUME!!!!!!!

Tumezishitukia ofa zao

Kwa huku kwetu ni wanaume wachache sana wanaomsaidia mwanamke bila lengo la kumpata mwanamke huyo, na akimtaka, mwanamke anaweza kujisikia vibaya wakati mwingine kwa kudhani kwamba misaada hiyo itakoma haraka kwa sababu hakuna jambo lenye kuwashika, yaani tendo la ndoa, hivyo hulazimika kukubali kutoa tendo la ndoa ili misaada isikome.

Hata hivyo sio wanawake wengi wanaokubali kulipa fadhila kwa njia hiyo, lakini wanaume wengi hutumia misaada au ofa kama chambo cha kuwanasia wanawake.

Kwa wanawake kusaidiwa ni kusaidiwa tu huwa hakufungwi na kutakiwa kimapenzi, lakini kwa wanaume kusaidia huwa kunafungwa pamoja na mapenzi.

Je sababu ni nini?

Wanaume wamelelewa na kufanywa kuamini kwamba wanatakiwa kuonesha sifa fulani kwa wanawake kabla hawajawatongoza.

Kwa hiyo mwanaume kabla hajatongoza huanza kujisifu kwanza, ili mwanamke amuone kama mtu anayeweza, hivyo mwanaume anapotoa msaada kwa mwanamke kuna mawili kama sio matatu, ama anataka kusifiwa au anamtaka mwanamke huyo, au vyote.

Lakini pia wanaume wengi huamini kwamba kwa kutoa ofa, mwanamke atajua kwamba anamtaka, hivyo kwa wanaume hao ofa ndio kutongoza kwenyewe. Kwa hiyo mwanume kama huyu anapotoa msaada kwa mwanamke anatarajia kumpata kimapenzi mwanamke huyo.

Kwa mijini kwa mfano mwanamke anayepewa lifti ni yule mzuri kwa sura na umbo, ukweli nikwamba hakuna msaada hapo bali mwanaume anaanza kununua penzi ambalo hajalipata.
Mwanaume akimpa lifti mwanamke na kumtongoza, na mwanamke huyo akakataa, basi huo msaada unafutwa mara moja.

Kwenye baa, mwanaume anaweza kumtuma mhudumu ampe pombe mwanamke fulani. Hajui mwanamke huyo kaja hapo baa na nani na anafanya kitu gani. hiyo ofa sio ya urafiki bali ni ombi la mwili wa mwanamke huyo, kwani hiyo ni hatua ya awali ya kuwa karibu nae.

Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hujitolea kuwasomesha, kuwapa au kuwatafutia ajira wanawake, lakini nyuma ya kujitolea huko, kuna agenda ya kuutaka mwili wa huyo mwanamke.
Mara nyingi mwanamke anakuwa hajui kwamba misaada mingi ya wanaume imefungwa pamoja na mapenzi. Ni wanaume wachache sana waliolelewa tofauti wasiofanya hivyo.

Ukweli ni kwamba wanawake wengi wamekuwa wahanga wa misaada .
Utakuta mwanaume anamsaidia mwanamke, mwanamke anapokea misaada hiyo akijua ni ya kibinadamu, kumbe akilini mwa mwanaume ni kwamba amewekeza. kwa hiyo anapokuja kumtongoza mwanamke huyo akakataa basi vita huanza.

Mwanaume anaweza kukumbushia misaada aliyotoa. na katika hali ya kushangaza mwanamke huyo hushikwa na butwaa. kwani hakujua kwamba alikuwa anapewa misaada ili atoe mwili wake.

Kuna wanaume wengi tu ambao wanaweza kumpa mwanamke soda kama taarifa kwamba amempenda, na mwanamke anaweza kupokea soda hiyo akijua kwamba ni ofa ya kawaida, lakini baadae hushangaa akija kutongozwa, na akikataa, anadaiwa soda aliyokunywa.

Nawasihi wanawake wenzangu wawe makini na ofa za wanaume kwani nyingi zimejaa utata mkubwa.



Habari ndiyo hiyo..........









5 comments:

Simon Kitururu said...

DUH!

Albert Kissima said...

Wanawake waliowengi sio kwamba ofa hizi huwa hawatambui mwisho wake utakuwa nini?

Hivi ni kwa nini wanawake wadanganywe au washawishike kwa sifa tu? Huu ni udhaifu mkubwa ambao asilimia kubwa ya wanawake wanao. mwanaume akitaka kumtokea msichana anaweza kuazima nguo nzuri au simu ya bei ghali,basi mdada kumwona jamaa na pamba kali,simu ya ghali,basi mwanadada anategeka kiulaini kabisa.Huu ni udhaifu.

Mwanaume hategeki kwa ofa(kuna wachache wanaotegeka) .Wanaume wengi wanategwa sana na maungo ya mwanamke na ndio maana wengi wetu tunakuwa na tamaa kwamba tunamtamani kila tumuonaye.

Pia kuna wanaume ambao hutoa misaada kwa maana ya misaada. Mimi nadhani tabia ya mtu binafsi pamoja na kujielewa ndivyo vitakuwa silaha yake ktk kukubali au kutokubali ofa ambazo mwishowake zitademand ngono.

Kwani hao wanawake ambao huwa hawapokei ofa hizi ambazo mwisho wake huishia kutakwa kimapenzi wanawezaje kukabiliana na hali hii?

Albert Kissima said...

Jamani ,sentensi ya kwanza kabisa hapo juu ,badala yakuuliza( ?) weka nucta. Ni matatizo ya mwandiko wa mlazo mcharazo

MARKUS MPANGALA said...

Koero umejiandaa kwa mada hii kweli?
Maana maswali yanaweza kuzidi pipa halafu ukaosa nguvu ya kugandamiza mpira?

Haya weeeeeeee! kawaida napenda kuhoji kama ambavyo nilikuwa nikijibishana kwa sms na msomaji wa makala ya dini. Yeye alitaka maoni yangu kuhusu dini lakini nilimpelekesha kwa maswali kisha akapotea hewani. Sikuweza kutoa maoni yangu wakati hajibu maswali ipasavyo.
NASHUSHA AYA:
Ofa ni kitu gani? Kwanini maisha yaendane na ofa? Kwanini wanawake wanapenda ofa hata kama wanajua mwisho wake? Ni kweli wanaume hutoa ofa kwa matarajio fulani? yaweza kuwa ndiyo kiutani lakini siyo kiundani inategmea na nani akupaye ofa!
Inawezekana hili ni tatizo kubwa na dada Koero umeliona na nashukuru kwa kuliwasilisha, lakini hebu tumia dakika mbili tu kutafakari mwenendo wa OFA halafu jipe jawabu! Ingawaje wengi tunadhani kwamba OFA ni jambo muhimu au kutoa ofa kwa mwanamke ni umahiri sana. Lakini tunaona waziwazi kwamba yapo mambo yanayochangia kufikia hapo, na sijui kama wanawake wenyewe wapo tayari kulijua hilo. Je kwanini ukubali lifti ujuayo inakuletea madhara? Je kuna umuhimu gani wa OFA?
DUH! najieleza vema kweli? Lakini mimi nasema hivi, ikiwa wanaume ni watoaji ofa kwa kudhani wanataka penzi, basi hilo ni tafsiri ya wapokea ofa kwani kama wasipopokea ofa basi haitakuwepo ofa kwao. Naongopa jamani?
SIJAMALIZA lakini naona nasita kuongeza. ngoja nipumzike kwanza

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe huoni hata nchi zetu zinavyopata matatizo kwa kupenda ofa (misaada)