Monday, March 30, 2009

KUTANA NA YASINTA, MJASIRIAMALI ALIYESEMA HAPANA KWA WANAUME WAKWARE

Nusura niwe mtoto wa mitaani

Juzi ijumaa nikiwa ofisini kwangu alipita binti mmoja akiwa na begi lake dogo kama yale yanayotumiwa na wanaume kubebea Lap Top.

Alinisalimia kwa uchangamfu na kujitambulisha kwangu kuwa anitwa Yasinta. Alionekana kuwa mchangamfu utadhani tunafahamiana siku nyingi, hata hivyo na mimi nilimchangamkia pia. Kumbe Yasinta ni mfanyabiashara wa kuuza viungo mbalimbali kama vile vya Pilau, viungo vya Chai, kwa kweli sikujua kama chai nayo ina viungo, pia alikuwa na viungo vya kupikia nyama , samaki au hata kuku na hasa kuku wa kienyeji na alitumia muda huo kunifundisha namna ya kutumia. Kwangu mimi hayo yalikuwa ni mapinduzi makubwa katika mapishi ya vyakula vya kiswahili

Yasinta Alionekana kuwa ni mdogo kiumri yaani ukimuangalia kwa haraka haraka anaonekana kuwa na umri wa kama miaka 18, hata hivyo sikukosea sana kwani nilipoomuliza umri wake aliniambi kuwa ana umri wa miaka 19 na mwishoni mwa mwaka huu ndio atatimiza umri wa miaka 20. Mara akaja jirani yangu mmoja ambaye ofisi zetu zinafuatana, alipomuona Yasinta alimshangilia sana na kuwaita wenzake na kuwajulisha ujio wa Yasinta, nilibaki nimeduwaa.

Baadae niliambiwa kuwa Yasinta alikuwa ni maarufu sana pale kwani alikuwa akiwauzia viungo vya mbalimbali na hivyo kufurahia mlo wao wa siku. Waliniambia kuwa walimfahamu Yasinta takribani miaka mitano iliyopita tangu alipoanza kuwapitishia ile biashara, wakati huo akiwa ni binti mdogo sana kwa umbo na umri.

Ni mwaka jana mwishoni alipowaaga kuwa anatarajia kufunga ndoa, na walimchangia fedha na zawadi nyingine. Tangu wakati huo Yasinta hakuonekana mpaka wakadhani labda ameamua kuachana na biashara hiyo, au mumewe amemkataza kuendele nayo.
Nilinunua viungo mbali mbali na niliamua kutumia fursa hiyo kufanya mazungumzo nae.
Yasinta alianza biashara hiyo mnamo mwaka 2005 Mara baada ya kumaliza darasa la saba mkoani Mbeya.

Je alifikaje mjini?

Yasinta alikuja mjini mwaka 2004 akiwa ndio amemaliza darasa la saba, baada ya kuwa hakufaulu na mama yake kutokuwa na uwezo wa kumuendeleza kielimu alichukuliwa na mama mmoja aliyekuwa akiishi maeneo ya Ilala hapa jijini Dar es salaam mwenyeji wa huko huko Mbeya ili kuja kufanya kazi za ndani.

Baba yake alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu wakati alipokuwa darasa la nne na kuanzia hapo majukumu ya kutunza familia aliyabeba mama yake pekee. Akiwa ni wa kwanza kuzaliwa na binti pekee kwa wazazi wake huku akifuatiwa na na wadogo zake wawili wa kiume, hakuwa na jinsi ilibidi aje mjini kufanya kazi za ndani ili aweze kumsaidia mama yake kuwatunza wadogo zake.

Alidumu na yule mama kwa mwaka mmoja. Lakini kutokana na mateso ilibidi atoroke na kujikuta akishia mtaani. Siku moja katika mizunguko yake ya kutafuta kazi alikutana na mabinti wa umri wake ambao walikuwa wakijiuza maeneo ya Buguruni na walimtaka ajiunge nao ili kujitafutia kipato, na walimuhakikishia kuwa shughuli ile ya kujiuza ina kipato kushinda hata ya kuajiriwa, hata hivyo Yasinta alikataa kata kata kujiunga nao, akamua kujichanganya na wale mama ntilie pale Buguruni CCM kwa kuwasaidia ili kujipatia kipato, hata hivyo mama mmoja allijitolea kumpa hifadhi.

Siku moja akiwa katika shughuli zake kama kawaida, alipita mama mmoja na kuagiza chakula, wakati akimuhudumia na kwa kuwa alikuwa ndie mteja pekee kwa wakati huo alianza kuzungumza nae. Katika mazungumzo yao yule mama alimjulisha juu ya biashara ya Viungo, mbalimbali vya mapishi ambayo ndio aliyokuwa akiifanya. Yasinta alivutiwa sana na ile biashara na kwa kuamini kuwa ule ulikuwa ndio wakati wa kuondokana na kazi za kutumwa, alimuomba yule mama amfundishe namna ya kufanya ile biashara.

Kwa bahati nzuri yule mama alimkubalia na na kuahidi kumpitia kesho ili wafuatane nae ili akamuoneshe mahali anaponunulia na kumuonesha namna ya kutayarisha.
Na kweli yule mama alimpitia kesho yake. Yasinta alimuaga yule mama aliyempokea pale Buguruni na kuondoka na yule mama kuelekea Kariakoo kufanya manunuzi.
Yule mama alijitolea kumpa hifadhi ya muda nyumbani kwake maeneo ya Vingunguti na kumfundisha namna ya kutengeneza viungo mbali mbali, Kutokakna na bidii aliyonayo ilimchukua Kiasi cha mwezi mmoja Yasinta kufudhu mafunzo hayo.

Yule mama alimkopesha Yasinta mtaji wa shilingi elfu kumi wa kuanzia.

Yasinta anakiri kuwa awali alikuwa na wakati mgumu sana kutokana na biashara kuwa ngumu lakini yule mama alimpa moyo wa subira.
Haikuchukuwa muda mrefu hali ilibadilika na biashara kumnyookea na kuweza kulipa mkopo aliokopeshwa na yule mama yake mlezi ambaye alimfanya kama mama yake mzazi kutokana na kumlea. Ilimchukuwa mwaka mmoja Yasinta kuhama na kupangisha chumba chake maeneo ya Buguruni na kuanza kujitegemea huku akiendelea na biashara yake hiyo ya viungo. Kuanzia hapo akawa anatuma hela kwa mama yake huko mbeya ili ziweze kumsaidia.

Mwaka mmoja baadae Yasinta alifanikiwa kununua kiwanja chenye ukubwa wa nusu eka maeneo ya Kinyerezi na ili iwe rahisi kwake kujenga. Ikabidi ahamie Segerea ili awe karibu na kiwanja chake. Taratibu alianza kujenga nyumba yake ya vyumba viwili. Ilimchukua mwaka mmoja na nusu kukamilisha nyumba yake ya vyumba viwili na kufanikiwa kuweka umeme na kuhamia nyumbani kwake. Lengo lake la kwanza likafanikiwa.

Yasinta alijiwekea malengo makuu matatu, wakati alipoanza biashara ya viungo.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni kujenga nyumba yake mwenyewe, kukarabati nyumba ya mama yake kule Mbeya na kuwasomesha wadogo zake mpaka chuo kikuu.
Baada ya mdogo wake anayemfuatia kumaliza darasa la saba mwaka juzi akamleta na kumuandikisha katika shule ya sekondari ya binafsi iliyoko maeneo ya Ubungo na gharama za masomo analipa yeye kutokana na biashara yake ya viungo anayofanya.

Je Yasinta amemudu vipi kufikia hapo alipofikia na nini matarajio yake? Nilimuuliza.

Yasinta alikiri kuwa subira na uvumilivu ndio umemfikisha pale alipo sasa, kwani kuna wakati biashara ilikuwa haitoki kabisa mpaka anashindwa kulipa kodi ya nyumba, lakini kwa kuwa alikuwa amejiwekea malengo alihisi kuwa alikuwa na deni kubwa mbele yake na hiyo ilimpa hamasa ya kutokata tamaa na aliamini kuwa atafanikiwa.
Anasema aliponunua kiwanja alianza kuishi kwenye nyumayake kabla hata hajaijenga, kwani alikuwa akijiona kabisa kuwa amejenga na alikuwa akiiona nyumba yake ikiwa imekamilika kabisa, hakudhani kama atashindwa, aliamini tu kuwa ataweza.

Vipi kuhusu wanaume?
Nilimuuliza kwa kuwa yeye ni binti ambaye bado ni mbichi, kabla hajaolewa aliwezaje kukabiliana na vishawishi vya wanaume hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa akiishi peke yake na shughuli zake ni za kuzunguka maofisini?

Yasinta alikiri kuwa alikuwa akipata sana mitihani ya kutakwa na wanaume, wengine wakiwa ni wababa wazima wakuweza hata kumzaa mara tano lakini alikuwa amejiwekea nadhiri ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa, pia alikuwa amepanga kuwa hataolewa mpaka awe amejenga nyumba yake mwanyewe, kitu ambacho amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Je alimpataje Mwezi wake?
Yasinta alicheka kidogo, huku akiongea kwa aibu kidogo, alisema, “ Huyu mume niliyekuwa nae nilijuana nae miaka miwili iliyopita wakati akisoma sekondari wakti huo, tulikuwa tukikutana mara kwa mara kituoni tukisubiri usafiri wa daladala wa kwenda mjini. Kutokana na usafiri wa daladala Segerea kuwa ni mgumu tulikuwa tukigombea mabasi pamoja, siku moja akanilipia nauli, nilikataa kwa kuwa niliona kuwa yeye ni mwanafunzi, kwa hiyo haikuwa ni vyema anilipie nauli, lakini alisisitiza kunilipia na akakataa kupokea hela yake aliyomlipa kondakta wa daladala, na huo ukawa ndio mwanzo wa kufahamiana kwetu.
Baada ya kumaliza masomo alijunga na chuo kimoja mjini na kusomea mambo ya information Technology, na sasa ameajiriwa na kampuni moja binafsi akiwa ni mtaalamu wa kompyuta”.

Je mumeo anayo mikakati gani ya kukuendeleza kielimu, au ndio umeridhika na kiwango cha elimu ya darasa la saba ulicho nacho? Nilimuuliza.

Yasinta alisema kuwa ameanza kusoma masomo ya sekondari ya jioni katika shule moja ya binafsi iliyoko Tabata na ndio ameanza kidato cha kwanza ambapo itamchukua miaka miwili kumaliza kidato cha nne.

Ukweli ni kwamba nilifurahishwa sana na mazungmzo yangu na Yasinta, kwani ni miongoni mwa mabinti wachache hapa nchini wenye mtazamo chanya kuhusiana na maisha, na ameonesha kuwa, ukiamua unaweza, kwani hakuna kisichowezekana chini ya jua, kinachotakiwa ni kujiwekea malengo na kuwa na nia na dhamira ya kufikia malengo uliojiwekea. Kingine ni nidhamu katika kila jambo unalolifanya, kwani bila nidhamu hakuna kufanikiwa.

Hivi ni wasichana wangapi ambao wameshindwa kuendelea na masomo, na badala ya kujitafutia maendeleo kwa njia ya halali wamejikuta wakijiuza ili waweze kujikumu?
Ni wangapi wamekufa kwa ukumwi au wanaugua ukimwi sasa hivi baada ya kujiingiza katika vitendo vichafu vya kujiuza mwili?

Yasinta katuonesha njia kuwa tukiamua tunaweza.
Namtakia kila la heri katika ndoa yake, idumu na iwe na amani na upendo.

23 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Koero, Huyu Yasinta hii habari ni ya kweli maana imenigusa kweli kiasi kwamba nimetoa mchozi. Maana mara moja tu nimejikuta kama ndo mimi yaani katika simulizi. Kazi kwelikweli

Subi Nukta said...

Koero, hii posti inastahili kuwekwa kwenye gazeti ama kuhifadhikwa kwa ajili ya kuchapishwa kwenye kitabu cha mkusanyiko wa hadithi na visa mbalimbali vyenye mafunzo. Umefika wakati sasa wewe na baadhi ya wananlogu wafikirie juu ya kuhifadhi baadhi ya posti zao ambazo zinafaa kuwa sehemu ya kumbukumbu ya maandiko yako.
Kigezo cha mimi kutaka posti hii ichapishwe na kusomwa na watu wasioweza kutumia mtandao ni kutokana na mafunzo halisi yaliyomo katika kisa cha Yasinta. Yapo mengi sana ya kujifunza kutokana na kuwa Yasinta anawakisha watu wa jamii kubwa sana ya Tanzania ambao mtiririko wa mambo katika maisha yao hautofautiani na kinachoonekana kwa Yasinta.
Malengo, Jitihada, Uvumilivu, Imani na Kujidhili ndiyo mihimili mkuu aliyokuwa nayo Yasita ambayo imemfanikisha!
Somo zuri!

Christian Bwaya said...

Kisa kizuri sana. Kinatupa mafunzo murua.

Nimependa namna ulivyoweza kutumia fursa kuanzisha mazungumzo na Yasinta.

Kwa jinsi hii, naamini ushauri wa Da'Subi utadai utekelezaji!

Koero Mkundi said...

Dada Yasinta,

Hiki kisa ni cha kweli kabisa, na hata jina nililotumia ni la kwake kabisa.
Awali nilitaka kubadili jina kwa kuhisi kuwa hii habari itahusishwa na wewe, lakini baada ya kuatafakari nikaona hakuna haja ya kufanya hivyo.
Ukweli ni kwamba habari hii nimeifupisha sana kutokana na kuogopa kuwachosha wasomaji lakini ukisikiliza simulizi za huyu binti unaweza kutokwa na machozi,
Amepitia katika kipindi kigumu mno, huwezi kuamini, mateso aliyoyapata kutoka kwa yule mama aliyemleta hapa mjini ni makubwa na ya kusikitisha sana.

Dada Subi: ushauri wako unahitaji tafakuri, nakumbuka hata kaka Bwaya aliwahi kuligusia swala hili lakini, kuna tatizo la Watanzania kutopenda kusoma vitabu.
Hili ni tatizo kubwa ambalo linawapata watunzi wa vitabu.

Kaka Bwaya: Naona hiyo ni changamoto kutoka kwa Dada Subi, Labda nikuachie wewe mwenzangu maana ulinitangulia kublog na unao uzoefu, naomba tujadili swala hili kwa kina.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pengine hii inafaa kusomwa na kila msichana na hasa yule ambaye bado anatafuta nafasi yake katika dunia hii mchafukoge - huku akipambana na vizingiti vya kila aina katika mfumo dume uliotawala. Safi kabisa dada Koero.

Wazo la Subi ni zuri sana na hata mimi nimewahi kusoma post zenye kuelimisha mno katika blogu mbalimbali kama Mzee wa Changamoto, Simon Kitururu, Bwaya na zinginezo (siwezi kutaja zote). Inasikitisha kidogo kuona kwamba mawazo mazuri namna ile hayasomwi na watu wengi na mchango wa hizi blogu zetu kidogo unatatanisha. Je, ni kweli tunawafikia walengwa? Mtu unaweka post hapa na hasa hasa ni wanablogu wale wale wenzako wanasoma na kuweka maoni yao basi. Inabidi tufikiri jinsi tutakavyoweza kuifikia jamii ambayo tunaipigania. Mimi ni mgeni katika huu uwanja na sijui kama kuna chama. Kama kipo, na kama kiko hai, tunaweza kuunda kamati ambayo itakusanya post nzuri na zenye mafunzo kama hizi na kuzihariri kisha kuzitoa kama kitabu. Gharama za kuchapisha kitabu hicho tunaweza kuchangishana na au kutafuta mfadhili. Mimi nitakuwa tayari kuwa mwanakamati katika kamati hiyo.

Hii nayo inazua swala jingine ambalo Koero ameligusia - jamii kutopenda kusoma. Watu wanapenda kusoma riwaya pendwa - vitabu vyenye matukio ya kusisimua na mapenzi. Ndiyo maana nasikia vitabu vya Erick Shigongo sasa vinasomwa sana - kama wakati ule Elvis Musiba alipokuwa akitamba na Willy Gamba katika riwaya zake za Njama, Kikosi cha Kisasi, Hujuma, Hofu n.k. Hili naomba lisitukatishe tamaa kwani kama tunaweza kupata mfadhili tunaweza kuvipeleka vitabu hivyo mashuleni na sehemu mbalimbali bure. Hata serikali tutaiomba itusikilize (kama ina masikio!) na kutusaidia. Kama sababu mojawapo kuu ya Watanzania kutosoma vitabu ni ughali wa vitabu kama ambavyo imeshawahi kutajwa tutakuwa tumeiondoa sababu hiyo.

Ni mawazo yangu haya katika kujaribu kuifikia jamii kwa upana wake. Vinginevyo tunaweza kuwa tuna mawazo mazuri sana hapa lakini bila kuwafikia walengwa ni kazi bure. Ningependa kusikia wanablogu wengine mnasemaje kuhusu wazo hili. Naomba kuwakilisha!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...
This comment has been removed by the author.
Fadhy Mtanga said...

maisha haya jamani, usione ukadhani,
maishani ni vitani, jemedari kwani nani?
watu huwa taabuni.

maisha haya jamani, tufikiri akilini,
wale walo taabuni, tuwaombee amani,
watu wapo taabuni.

Mzee wa Changamoto said...

Da Subi.
Sina namna nyingine ya kuamini kuwa UELIMISHAJI WA NAMNA HII UNAWEZA KUIFIKIA JAMII zaidi ya ulivyosema.
Nawashukuru nyote kwa maoni.
Dadangu K, kazi ama wajibu huu naamini ni mkubwa mno na umeutimiza ipasavyo. Ambaye anapenda maendeleo na kujitegemea kwa taifa letu na asiguswe na hii atakuwa na "issues"
Mdogo wangu Yasinta. UBARIKIWE

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo

leo nimesoma gazeti jipya uliloandikia makala ya Lugha. labda gazeti hilo liwe na ukurasa maalumu unaoitwa kutoka bloguni au bloguni wiki hii ili vitu kama hivi vichapishwe humo.

Niwazo tu

ERNEST B. MAKULILO said...

Hoja ya kuwa na kuandaa kitabu chenye post za kuelimisha na kusisimua kama hii ni muhimu mno.

Kaka Matondo, sijui hapo tujipange vipi ktk hili.Mimi naona kwa kuwa wanablog wengi tunajuana, kuna umuhimu mkubwa mno wa kuliweka hili wazi na kuona tulifanyaje.Naamini tukikusanya makala au habari kali za kila blog itatoa kitabu kimoja kizuri mno.Tupange modality wandugu ktk hili

Dada K, tunashukuru kwa kuleta habari hii nzuri ya ukweli.Naamini ina mafunzo makubwa mno kwa ktk njia ya kufanikiwa.Ila kama mchangiaji mmoja hapo juu, nina wasiwasi kuwa habari hii inasomwa na watu wachache mno.Kama unachunguza, hata comments zote ni za watu wenye blog tu, kama Da Subi,Mzee wa Changamoto,Kamala na wengine wengi.Maana yake ni watu wachache mno nje ya wana blog wanaopitia habari hizi.Hivyo wazo la kukusanya habari kama hizi na kutoa chapisho moja itakua ni jambo la busara mno.

MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com

ERNEST B. MAKULILO said...

Hoja ya kuwa na kuandaa kitabu chenye post za kuelimisha na kusisimua kama hii ni muhimu mno.

Kaka Matondo, sijui hapo tujipange vipi ktk hili.Mimi naona kwa kuwa wanablog wengi tunajuana, kuna umuhimu mkubwa mno wa kuliweka hili wazi na kuona tulifanyaje.Naamini tukikusanya makala au habari kali za kila blog itatoa kitabu kimoja kizuri mno.Tupange modality wandugu ktk hili

Dada K, tunashukuru kwa kuleta habari hii nzuri ya ukweli.Naamini ina mafunzo makubwa mno kwa ktk njia ya kufanikiwa.Ila kama mchangiaji mmoja hapo juu, nina wasiwasi kuwa habari hii inasomwa na watu wachache mno.Kama unachunguza, hata comments zote ni za watu wenye blog tu, kama Da Subi,Mzee wa Changamoto,Kamala na wengine wengi.Maana yake ni watu wachache mno nje ya wana blog wanaopitia habari hizi.Hivyo wazo la kukusanya habari kama hizi na kutoa chapisho moja itakua ni jambo la busara mno.

MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Makulilo Jr.

"Naamini tukikusanya makala au habari kali za kila blog itatoa kitabu kimoja kizuri mno"

Ndiyo kitakuwa kitabu kizuri sana na kama tutaweza kupata mfadhili basi kitabu hicho kitaweza hata kusambazwa bure.

Hata wazo la Kamala ni zuri. Mmoja wa waanzilishi wa gazeti hilo jipya la Kwanza Jamii ni Mwanablogu mashuhuri na sidhani kama atakataa kututengea ukurasa mmoja au nusu ukurasa kwa ajili ya kutolea makala nzuri za wanablogu. Kwa hali hii tunaweza kupanua wigo wa hadhira yetu. Wanablogu wengine mnasemaje?

Unknown said...

Wazo hili la kutengeneza kitabu niliwahi kulizungumzia Siku moja nilipokuwa na Kamala, pia niliwahi kulizungumzia kwa njia ya simu na kaka Bwaya, nadhani dada Koero katufikirisha kiasi cha kulifufua hili wazo.

Ni kweli tunahitaji kitabu kitakachokuwa na mkusanyiko wa mijadala mbali mbali ntunayoiandika katika blog mbali mbali.

Habari ni ya kupigiwa mfano, ni vyema wanablog tukawa tunaaandika madhila na mafanikio ya wanajamii ili jamii iweze kujifunza kutokana na uzoefu wa wenzetu, tunapopata visa na mikasa inayotokea katika jamii inayotuzunguka tunajifunza mengi kupitia humo.

Naomba wazo hili lisiishie hewani wote tulijadili na kama wazo la kamala litakubaliwa sawa ila tuendelee kufanyia kazi wazo kuandaa kitabu. nimefurahishwa kuona kuwa wanablog karibu wote tunaounda kijiji hiki tuna wazo linalifanana....

Naomba maoni zaidi yatolewe ili tujue tunaanzia wapi....

Albert Kissima said...

Hongera Koero, ni kisa kizuri ambacho naamini kwa yeyote atakayekisoma ni lazima atajifunza. Nimejifunza kwamba ujasiri, uvumilivu na mipango thabiti ktk maisha ni mambo ya msingi sana katika kuelekea kwenye mafanikio.

Hongera sana Yasinta.Ni dada wa kuigwa na mfano mzuri ktk jamii.

Nami pia nawaunga mkono wenzangu waliotangulia kuhusu kuanzishwa kwa kitabu hicho.

Rama Msangi said...

hivi ni kwanini Wazawa tunapenda kuwaita WAJASIRIAMALI, na wenye ngozi nyeupe WAWEKEZAJI? Ulishawahi kulisikia neno mjasiriamali wa kihindi hata siku moja? au wa kichina, au wa kimarekani? ila kwa wazawa ndio kila mmoja ni mjasiriamali!!

mercy said...

very inspiring!..

scr888 play for free said...

I wanted to thank you for this great scr888 slot game download malaysia read. Your blog is one of the finest blogs. Thanks for posting this informative article.

flag said...


Thanks for taking the time to discuss that, I really 918kiss free credit new member feel strongly about it and love learning more on that topic. If achievable, as you gain competence, would you mind updating your blog with more information It is highly helpful for me.

OneGold88 said...

I really enjoy scr888 big win reading your blog as the postings scr888 bonus are so simple to read and follow. Outstanding. Please scr888 club keep it up. Thanks.

methew william said...

Thanks for always being the source joker123 download pc that explains things instead of just putting an unjustified answer out there. I loved this post.

3win8 said...

You are a extremely clever person!
http://www.authorstream.com/Presentation/aladdin99my-4104223-aladdin99s/

Woodman J Parker said...

Ultra Fast Keto Boost speak on your physician earlier than beginning a physical exercise recurring.
- medicines
In cases wherein modifications in eating regimen and bodily pastime do no longer bring about a reduction in ldl cholesterol, your doctor may additionally prescribe medicinal drugs to manipulate LDL.
https://purefitketodietplan.com/ultra-fast-keto-boost/

enable-ai said...

We have a wide variety of magic mushroom edibles, like mushroom edibles chocolate, candy, and tea. It's easy for you to know how much psilocybin you're taking in at any given time because our edible mushrooms are carefully infused with a fixed dose of psilocybin in each portion.