Wednesday, February 3, 2010

KWA NINI IWE NI WANAUME TU WANAONUNUA MKUYATI?

Jamaa akinunua Mkuyati

Kuna wakati wanaume wanaweza kuwa na ugumu wa kujua kwamba wake au wapenzi wao hawaridhiki kimapenzi. Hiyo inatokana na uwelewa mdogo waliokuwa nao wanaume juu ya tofauti kubwa iliyopo kati ya wanawake na wanaume kuhusiana swala zima la hisia za kimapenzi.

Wanawake wana matarajio makubwa sana katika kila eneo linalohusu maisha yao, lakini linapokuja swala la tendo la ndoa mambo ni tofauti sana. Kwa kawaida wanawake wengi ambao hawaridhishwi na tendo la ndoa kwenye uhusiano wao huwa wanafanya siri.

Bila kujali kama tatizo liko kwao au kwa waume zao, wanawake hufanya siri kutoridhika kwao kimapenzi, na huweka siri kwa waume zao na hata kwa madaktari. Na ndio maana sishangai kuona kwamba wateja wa wauza dawa zinazohusiana na kuongeza hamu ya tendo la ndoa yaani Mkuyati ni wanaume.

Nilipokuwa nyumbani Tanzania, jijini Dar Es Salaamu nilishangaa sana kuona katika magazeti maarufu ya Udaku, {Tabloids} matangazo mengi ya biashara yanayotawala katika magazeti hayo ni ya kuuza dawa za kuongeza nguvu za kiume au hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na nyingine zilikuwa ni za kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume, dawa kama Mkuyati, Mzakaru, Super Shaft, Kifaru, Sekwa na nyingine chungu nzima ni maarufu sana jijini Dar Es Salaam.

Sio kwamba wanawake hawana matatizo ya tendo la ndoa, la hasha. Wanawake wanayo matatizo hayo ya tendo la ndoa lakini kwao hiyo siyo agenda, yaani si kitu cha kuwaumiza sana kichwa. Lakini kwa wanaume ni tofauti sana, wanapokuwa na tatizo la kukosa ufanisi katika tendo la ndoa huo utakuwa ni mgogoro mkubwa sana, kwani kwao hili ni jambo linalopewa kipaumbele kuliko mambo yote.Kwa wanaume kukimbilia hospitalini au kwa mganga wa jadi na kusema “nina tatizo kubwa” ni jambo la kawaida kabisa….

Lakini wanawake hawafanyi hivyo, Badala ya kulifanya tatizo hili ni mgogoro halisi, huwekwa chini kabisa kwenye orodha ya matatizo yao, huwekwa kiporo na litashughulikiwa kwa wakati atakapojisikia kufanya hivyo kwa wakati wake.Wanawake wanaweza kwenda kuomba ushauri au kuwasimulia mashoga zao, kuhusu matatizo ya ndoa.

Lakini ni hadi wachokozwe ndipo wanapoweza kusema kwamba maisha yao ya tendo la ndoa na waume zao hayako sawasawa. Hilo halipewi uzito wa juu au naweza pia kusema hufanywa siri.Wanawake hawaridhishwi na tendo la ndoa kwa sababu mbali mbali. Lakini bila kujali sababu hizo, kwao ni vigumu sana kusema kuhusu kutoridhishwa kwao.

Ukiona mwanamke anatangaza sana kuhusu kutoridhishwa kwake na tendo la ndoa, basi ujue huyo na mumewe wako kwenye uhusiano mbaya sana. Kwani atakuwa anatumia maelezo ya kutoridhika kwake kama adhabu ya kumkomoa mumewe kwa kumuaibisha.

Lakini wale walioko kwenye ndoa imara ni vigumu kuwasikia wakilalamika kwamba hawaridhiki na tendo la ndoa. Inawezekana kutoridhika kwake kunatokana na yeye mwenyewe, yaani labda hana hamu au hafiki kileleni kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya kisaikolojia au matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, lakini bado sehemu kubwa wanaume huchangia. Hata hivyo pamoja na sababu hizo, mwanamke hayuko tayari kusema kuhusu kutoridhika kwake.

Kushindwa huko kunatokana na jinsi jamii ilivyomfunga mwanamke, kutoonesha kuhitaji tendo la ndoa. Akionesha kutoridhika na tendo la ndoa huonekana ni Malaya, kwa hiyo hukaa kimya na kuonesha kutojali. Lakini bila shaka nadhani umefika muda wa wanawake kuwa huru kuhusu tendo la ndoa na kusema hisia zao wazi wazi bila kuogopa jamii itawaonaje, kwani jamii imekandamiza haki yao ya kuzungumzia tendo la ndoa kwa muda mrefu sasa.

Wanaume nao wanapaswa kujua kwamba wanawake hawapendi au hawawezi kuzungumzia kutoridhishwa kwao na tendo la ndoa, hivyo kutosema kwao kusitafsiriwe kuwa ndio wanawaridhisha, ni vyema kutoa ushirikiano kwa wake au wapenzi wao na kutafuta kujua kama wanawaridhisha.

Ni jambo la busara kama mwanaume atadadisi kwa upendo na lugha ya upendo na kuonesha kama yuko tayari kutoa ushirikiano pale ambapo mke au mpenzi ataonesha kutoridhishwa na tendo la ndoa.

Mada hii nimeichukua kutoka kwenye kibaraza cha MAISHA, cha dada Yasinta, nami nimevutiwa nayo nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha.

6 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Swala hili ni two way traffic. Yawezekana akina baba na mama wote wana tatizo :-(

NDIYO: waweza kuta wotw wana matatizo ya AKILI :-(

utakuta baba/kaka/mama/dada katika shughuli nzima ya kuonja/kuonja atataka apige/apigwe mabao kibao :-(

wakati kuna staili nyepesi tu ambayo waweza piga bao moja demu akawa hoi wiki nzima....lol

na mkaka asitake tena kwa mwezi mzima :-)

ndo sababu nathema mambo yote ni AKILI tu koero...lol

MARKUS MPANGALA said...

baada ya mada hii kuwasilishwa katika kibaraza cha dada Nangonyani, niliamua kunyamaza ili nifanye uchunguzi wangu. kabala sijafanya nilikutana na mwanablogu Shaban Kaluse, tkajadili mambo mbalimbali kuhusu blogu na mada mbalimbali. lakini mada hii ilitugusa kiasi, nikamweleza nia yangu ile kwamba iwapo tatizo hilo linatokea basi ni matokeo siyo chanzo. na endapo magazeti ya udaku ndiyo chanzo na uatafiti, nikasema inabidi nianze kusoma magazeti hayo ili nione kunani.
nimeona matangazo ya aina hiyo nimeiona ofisi ya dk Kifimbo pale magomeni, na maeneo mengi sana.
sawa inawezekana kuna tatizo hili, lakini siyo kwamba wote wanaokwenda kununua mikuyati wanatatizo na nguvu ndogo bali simulizi na kupeana habari za umahiri wa dawa hizo katika kuchunguliana uvunguni.. mimi nimekulia mazingira yenye dawa hizo, nimekulia mazingira ya dawa za kuongeza ukubwa wa uume, nimeona dawa za kuchanja ukeni zinazotumia ULEZI, nimeona dawa za aina mbalimbali. hata hii ya mkuyati wala huna haja ya kufuata masharti, zipo dawa/mimea ambayo inawezesha kuongeza nguvu lakini wanaoongeza inatokana na tatizo la kisaikolojia tu.
Pengine kupoteza hamu kwa wanaochunguliana uvunguni, na sikubali kuwa samaki mmoja kioza wote wameoza. Yapo matatizo mengi, kuna shehe yupo mwembechai magomeni nimemkuta majuzi kafungua ofisi eti kusaidi matatizo, wapo wanawake wanaohangaika ili wapendwe sana, wamejazana kwa shehe ya yahya. Nakumbuka Koero uliandika kuwa wapo wanaume wanaotumia au kutafauta dawa za kuwatafuta wanawake wenye pesa. Sikushangaa kwani nimekulia maeneo yana dawa aa aina mbalimbali siyo simulizi za mikuyati ambazo zinatokana na ujinga wanaume wenyewe. Wengine wanakwenda kwasababu tu wamesikia dawa hizo ni nzuri lakini hawana tatizo la kupungukiwa nguvu. ewe mwanaume nakwambia kuanzia leo uwe na kawaida ya kualamba asali walau kijiko kimoja asubuhi na jioni.... halafu uje uniambie huo uume wako unafanyaje endapo hukuwa na nguvu. Pia fanya mazoezi ya mshipa wa KEGEL kila unapokojoa hasa asubuhi au wakati wowote.

SASA matatizo ya wanaume kupungukiwa nguvu kama tunavyolazimishana TUAMINI. wanawake wamekuwa WASGAJI na idadi hii inaongezeka kila siku, huku wengine wakisema waume zao wanawachungulia uvunguni kwa nguvu kama ng'ombe, wanatumia mb"""" bandia ili kujiridhisha kimapenzi. na hili linachangia kuadai eti sitaki wanaume... kumbe wanaji'"""""" wenyewe.
yako mengi ambayo ningeweza kuandika hapa tangu dada yasinta aweke mada hii, lakini naamua kunyamaza tu kwani SIAMINI KATIKA MKUYATI naamini ninaouwezo wa kumshughulikia mwanamke yeyote kwa njia ambazo tumejaliwa wanaume. NI MTAZAMO TU, kwani magazeti ya UDAKU hayaja nihakikishia kwamba ni suala la UTAFITI WA KISAYANSI kuwa ndiyo tatizo lenyewe.
MCHARUKOOOOOO HUUOOOOOO

nyahbingi worrior. said...

Nimekuwa nikipita hapa vukani kwa muda na leo itakuwa mara ya kwanza kwangu kuacha maoni.

Sellasi I.

Anonymous said...

Mpangala - hizo dawa za kuongeza unene wa uume zinafanya kazi? Sema tutajirike bwana..

MARKUS MPANGALA said...

Suala la kutajirika nakwambia unapaswa kutajirika kwa njia halali ya nguvu na juhudi za kazi siyo mitishamba, nimeona madawa na kila yaina ya mime ambayo inaelezwa ni dawa nzuri za kupata utajiri lakini maishani mwangu siwezi kukwambia utumie dawa utajirike kwakuwa sina uwezo wa kukusaidia zaidi.
sasa hili la dawa za kuongeza nguvu za kiume naona watu waqnahangaika bureeeeeeee wakati wanaouwezo wa kushughulikia tatizo lao kwa njia za kawaida kabisa

Unknown said...

Style ipi hiyo