Sunday, March 21, 2010

HOFU YOTE HII NI YA NINI?

Hii ndio njia wanayotumia kuingia nchini

Jana nilikuwa na Dine na rafiki yangu mmoja, binti wa Kijerumani katika mghahawa mmoja marufu ulioko maeneo ya Masaki.
Yeye, yuko hapa nchini kama Expert akiwa anafanya kazi katika sekta ya Utalii.

Wakati tukiendelea kula huku tukipiga soga, mara wakaingia Wachina kama kumi hivi wakataka waandaliwe meza ya pamoja, lakini baada ya kuingia hao Wachina, atmosphere ya pale ndani yote ilibadilika kwani karibu wateja wote waliokuwepo pale ndani ambao mostly walikuwa ni wazungu waligeuka kuwatazama.

Wachina wale walikuwa wakiongea kwa kikwao tena kwa sauti kiasi kwamba utulivu uliokuwepo pale mghahawani ulitoweka ghafla.

Yule rafiki yangu ambaye muda wote alikuwa amewatumbulia macho, alinigeukia na kuniuliza, “Ninashangazwa sana na serikali yenu kuwakumbatia Wachina kiasi hiki, mnadhani watasaidia kuinua uchumi wenu”

Kwa kifupi nilimjibu kuwa huu ni utandawazi na serikali yetu haina mkataba na taifa Fulani kuwa ndilo lenye mamlaka ya kuingia na kuishi au kufanya kazi hapa nchini, kwa hiyo yeyote yule mwenye kutaka kuja kuwekeza hapa nchini anaruhusiwa ili mradi asivunje sheria a afuate taratibu za kuingia hapa nchini basi.

“Nadhani huko sahihi”, alisema binti wa Kijerumani, “Unajua sisi inapotokea tunataka ku renew working permit zetu, kunakuwa na usumbufu mkubwa sana, ukilinganisha na hawa Wachina, wao wapo kila mahali na wanafanya biashara ambazo zilipaswa kufanya na nyie lakini hawabughuziwi kama tunavyobughuziwa sisi wazungu, imefikia mahali sasa tunahisi kubaguliwa waziwazi tofauti na hawa Wachina”

“Wewe unadhani tatizo ni nini?” Nilimuuliza.

“Sikiliza, hawa wachina ni wajanja sana wameleta miradi ya ujenzi wa barabara kama danganya toto, na katika miradi hiyo wamejipenyeza kwa kisisngizio cha expert na baada ya mradi kuisha wanendelea kuishi hapa nchini kwa kisingizio kingine cha wawekezaji ambapo hufanya shughuli ambazo zilipaswa kufanywa na nyie wazawa, na wamejipenyeza katika maeneo ya uswahilini na kuishi na wenyeji kwa ushirikiano na wamejifunza Kiswahili kiasi kwamba wamegeuka sehemu ya jamii ya chini kabisa, lakini baadae hawa watu wata take over kila kitu na kuwaacha mkishangaa, sio watu hawa jiangalieni”

“Ok, kwa nini na nyie msifanye hivyo” nilimshauri,

Haiwezekani, unajua sisi tuna utamaduni tofauti na nyie, lakini Wachina huenda utamaduni wao hauna tofauti kubwa na wa kwenu na ndio maana wameweza ku corp na society yenu bila shaka” alinijibu……….

Kwa kifupi mjadala ulikuwa ni mzito na mrefu kiasi kwamba ulichukua sehemu kubwa ya mazungumzo yetu…….any way labda nilichotaka kuwauliza hapa ni Je kuna haja ya watanzania kuhofia ujio wa hawa Wachina, au wamekuja kusukuma mbele gurudumu la maendeleo?

7 comments:

Anonymous said...

Wa nini kwani waacheni si wanawajengea nchi yenu.

Yasinta Ngonyani said...

MMMMHH! hapa kazi ipo, ngoja nitafakari ntarudi.

Candy1 said...

Kama wahindi walivyo-take over huku? (no offence)...it can be an advantage na disadvantage. Huku kila biashara mhindi isipokuwa kwenye makampuni makubwa makubwa kama benki vile but they seem to RUN EVERYTHING!

Lakini huku .... this is a developed country so I don't think it is that much of a problem ...the problem could be illegal immigrants ila I think they are handling it....sasa imagine wachina taking over Tanzania....I swear!!!! GOD FORBID! Kuwa na hofu...mmh...SIJUI! ila tuwe waangalifu...na maendeleo? Sawa ila wasituonee tu...lol...mambo ya panya kukutafuna huku anakupuliza..dang!

Anonymous said...

Hiyo ndio faida ya UTANDAWIZI, (Glob- 2.0 by Tom Friedman)ambapo dunia inasogea kutoka size medium to size small. Sina uhakika kama ni win-win situation kwa wazalendo, lakini serikali ya Tanzania haina la kufanya; suala hili limekuwa headache kwa serikali za dunia nzima.
Wazungu sharubu zinawacheza kwa kutokuwa na ufumbuzi wa kupambana na suala la wahamiaji (haramu na halali).
La muhimu ni serikali kuhakikisha kwamba ni wale wenye haki ya kuishi hapo ndio wanaondelea kufanya shughuli zao (Hello corruption!!!).
Wachina wameisha ujua ule msemo wetu wakiswahili usemao: PENYEE UDHIA PENYEZA RUPIA.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

waache waje. kwanza huyo rafikiyo ni mjerumani, tunawajua kwa ubaguzi wao wa Kinazi nk. wabaguzi sanana anasikitika sana kuona sisi hatuwabugua watu anaowachukia (wachina)

hivi nani alichagua kuwa mtanzania, mzungu au mjermani?? nani alichagua Uafira, uchi-na au hata uarabu? si ni ajalitu?? iweje tubaguaane??

kwani nani aliamua na kuomba kuwa mtanzania?? acheni ubaguzi wandugu.

Anonymous said...

Kamala. Usipende kugeneralize kwamba wajerumani wote ni ma-racist. Inawezekana lakini siyo wote.Such sweeping statements sio nzuri kwa mtu kama wewe mwenye blog unayejaribu kuwaelemisha wenzio. Iam sorry kama nimeku-offend.

Kurudi kwa Wachina, nadhani ni part ya frustrations za waafrika. Maana we have been friends (if that is the right word anyway) with the western world for many years and we have got nothing to show for it. Wamechukua madini yetu, mafuta na mengineyo (ofcourse na sisi kupitia kwa akina Mkapa and co tumechangia kuwapa) wakati tukizidi kudidimia kwa ufukara. Perhaps viongozi wetu wanaona wachina watakuja na different package.

Ukweli ni kwamba, maendeleo ya Africa yataletwa na mwafrika..forget about uwekezaji na mengineyo. Hii dunia kila mtu anajihangaikia mwenyewe. Awe US, China, UK au nani..kila mtu anahangaikia maslahi yake. Its only in Africa tunaofikiria kwamba misaada ya UN au World Bank will make a difference in our loves. We are in for a groomy night my fellow compatriots...

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___