Saturday, March 13, 2010

KOERO NDANI YA DAR.......

Foleni Jijini Dar
Hatimaye baada ya safari ndefu nimeshawasili Jijini Dar. Kama kawaida nitaendelea kuwakilisha katika blog yenu hii ya VUKANI.

Jiji letu nimelikuta vile vile, hakuna mabadiliko makubwa na foleni ya magari ndio usiseme. Kwa wale waliozoea kuendesha magari kule mikoani, hususan Arusha na Moshi, basi wakija hapa inabidi wapunguze jazba maana unaweza kujikuta unapigana kutokana na kukerwa na kile wanachoita kuchomekea, hasa Daladala, unaweza kuwa umekaa folen muda mrefu, lakini ghafla unakuta daldala hiloo limekuchomekea, yaani unatamani ushuke umlambe mtu makofi, lakini weee, watu wa Daladala ni washari ajabu, ngumi mkononi.
Ngoja nisianze porojo hapa, nikapumzike halafu tukutane kesho.................

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Shukrani kwa Mwenye Enzi mdogo wetu umesafiri salama. Haya pumzika na tuonane hiyo kesho...

EVARIST said...

Tunasubiria michapo zaidi ya jiji la Dar

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Karibu TANZANIA dada!

Mzee wa Changamoto said...

Basi nilipopita hapa JANA nikakuta "malizio" kuwa TUKUTANE KESHO. Nikaona "hakuna haja ya kuanza POROJO ambazo Da K amekataza. Sasa ntarejea "kesho"
Sasa na leo nakuta bado yasomeka "tukutane kesho". Ngoja nisubiri labda by kesho itasema "tuykutane leo"
Much Luv Sis
Blessings

mumyhery said...

Pole na safari

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___