Wednesday, July 7, 2010

MTANDAO UNAPOKUWA KIMEO!


Ni Siku ya tatu leo mtandao umekuwa Kimeo hapa Arusha kiasi kwamba mawasiliano na wanablog wenzangu na wasomaji wa kibaraza cha Vukani yamekuwa adimu kweli.
Sina taarifa za masaibu yaliyoikumba TTCL mpaka kufikia kutunyima haki yetu ya msingi ya kuwasiliana na wapendwa wetu.

Naomba mwenye taarifa zaidi anijuze maana leo imenibidi nipate mawasiliano kwa jirani mwenye kutumia Satellite ili niwasabahi wasomaji wa kibaraza hiki.
Jamani msione kimya bado ningalipo, na kwa sasa niko kwenye mchakato wa KUTANGAZA NIA kupitia Viti maalum vya CHADEMA huku Arusha.
Naomba wahafidhina msije nitoa roho……….NATANIA TU….!!!!

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pamoja daima ahsante kwa taarifa na sasa tunajua upo nasi.

nyahbingi worrior. said...

Nimepita kukusali na kupata habari za hapa na pale.

Sellasi I.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nimezoea hali kama hizo!!

Anonymous said...

wanablog tumuunge mwenzetu mkono mwenzetu da Koero anatarajia kutangaza nia huko Arusha....LOL

Fadhy Mtanga said...

We tangaza tu nia tutakuunga mkono.

Kuhusu mtandao ni tatizo la kiufundi kutoka kwa kampuni ya Seacom ambao ndiyo wenye mkonga wa mawasiliano. Kuna hitilafu imetokea kiasi cha kuwafanya service provider kufulia ghafla.

Naona wapo katika harakati za kurekebisha hitilafu hiyo. Tatizo hilo limewakumba wote wanaotumia huduma hiyo kuanzia TTCL, Zain, Selcom.

Ila wakati huu naona hali imeanza kutengamaa kidogo.

chib said...

Da Koero.... ebu acha utani, kwa nini unatukata maini kwa kutuambia ya kuwa unatangaza nia halafu unapaa tena.
Yaani tutakuunga hata mguu, nina hakika mwanamke atapata ukombozi kama utaingia huko kwa wahesh.
Tunakosa mtu mwenye fikra kama zako.
Pole kwa kukosa mtandao, lakini nasi pia tuna sua sua tu

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Koero - ni kweli umetangaza nia?

Mtandao hapo Arusha hata mimi ulinitoa knockout wakati ule...

Nimerudi na chakula kitamu na kichungu kinakusuburi kule jikoni kwangu. Pamoja.

Godwin Habib Meghji said...

Mtandao ulikuwa kimeo Tanzania nzima. Naona huu Mkongo bado haujawa stable. Nilikuwa dar es salaam na nilipata tatizo hilo hilo

Bwaya said...

Hivi kila aliyetangaza nia ni lazima agombee?

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___