Thursday, July 29, 2010

WATANGAZA NIA WAMEANGUKIA PUA

Ni jambo la kufurahisha kwamba, kumbe wamezea mate tonge wako wengi, ni kama mchezo wa kuigiza vile au ile tamthiliya tamu ya Egoli. Kama mtakumbuka niliwahi kueleza kuhusu wale wakware wenye uchu anuai walioanza mchakato kabla ya kipyenga kupigwa.

Ni mada isemayo “Dalili hizi si za kweli” kama ungependa kujikumbusha mada hiyo, basi waweza kubofya hapa. Siku za karibuni wakaibuka tena wahafidhina tena kwa kasi wakitangaza nia, sijui ni baada ya kusikia kuwa Koero katangaza nia ya kugombea ubunge kule Arusha.

Wakionekana kuwa makini katika kuzicheza karata zao wakaibuka upya tena kwa kasi, nadhani walikuwa na ndoto za kufunga pingu za maisha na Mbunge…mweeeh Kalaghabahooo!! Yaani wanapiga honi kwa gari waliyopewa lifti??? . Maombi na Cv, zikatumwa, huku wengine wakijimwagia sifa lukuki, kwa tamaa ya kutaka kujimwayamwaya na kimwana…..safi hiyoooo…. Hebu Vuta pumzi msomaji

Nami nikaona huu ndio wakati wa kuweka mambo hadharani yaani HAPO SAWA…….jamanieeee waungwanaeeeeeee!!! Imekuwaje tenaaaaa!! Basi ipo hivi kuna maboksi matatu hapa, kulikoniiii….kaka zangu wakaibuka, lakini aliyeonekana kufuata nyayo za sheikh Wayaya wa kule Mwembe Chai ni kaka yangu mpenzi Markus Mpangala, lakini hata hivyo kaka yangu Chacha Ng’wanambiti na Fadhy Mtanga wakajaribu kuwa Nostradamus wa kudadavua mambo yajayo.

Si haba nikaweka angalizo tena……..Jamanieeee bado tu hamuhisi kitu kabisaaaaaa au mnayeyusha tuuuu!! Patamu hapo!!!….na hapo ndipo wakaibuka tena wadau na ndoto za alinacha……..wanguuuuu……wanguuuuu….nanunua bunduki mie…... najikokiiiii najikokiiii jamaniii salaaaaaleeeeee...…LOL

Kaazi kweli kweli,, na ndio maana nikasema kuwa kublog kuna raha zake, hasa pale unapowachezea shere wahafidhina………safi hiyoooo.

Nasema hivi, Mambo baaaado kabisa, kama ni siku, basi ndio kunapambazuka hata mawio haijafika waungwaaaaaa!!!, na lakini siwakatazi wadau kupiga jaramba maana hamuijui siku wala saa, kukaa benchi halafu ukaambiwa piga jaramba inatia matumaini mweeeeeh!!! kwa maana utukufu utawajia kama mwivi, na hapo ndipo mtakapokenua hadi jino la mwisho……chungu kapata kivunoooo!!! .Je ni nani ataangukiwa na utukufu huo, ni swala la kuvuta subira, lakini kwa kifupi ni kwamba, pamoja na wasifu wao maridhawa,.haikuwa tija kwangu, hivyo wameangukia pua…... wacheke wana mwanyaaaa!!.....LOL

Wera weraaaa, na sasa nawaomba tuelekeze fikra zetu katika kumpigia debe Dr. Slaa, ili kama mungu akipenda, Inshaallah….aingie pale mjengoni Magogoni…..... huku wanablog tukipiga jaramba pale Luthuli kwa mwendo wa kunyatia...... vijana wa mjini husema ..... mdomdo yaani kidogo kidogo.....….

Nasema hiviiiii kipenga bado kupulizwa, kwa hiyo watangaza nia vuteni subira……..... Vuteni Pumzi.......

9 comments:

Subi said...

tehe, we dogo umenifurahisha sana kwa posti yako, yaani nimecheka mpaka basi!
Endelea kuwepo Koero!

Mfalme Mrope said...

ishu ilikuwa kanganyifu hiyo nami nikaona bora niwaangalie maalwatani wakitoa utabiri wao...

Markus Mpangala said...

Daaaaaaaaahhhh! ama kweli maumivu yakizidi muone daktari,
upate afadhali,
uwe muwari,
kwa yako hali,
Punguza munkari,
Uchovye asali,
karibu au mbali,

aaaaah!
mgema sifa akipewa,
tembo maji hutwaa,
Kumbe king'aacho si kidani,
bati nalo lipo vitani,

utamu alwatani
umewashinda maanani,


Eeeeh! Mie simo jamaniiiii eeeehh maana MCHANGANYA ZEGE HAOGOPI KUCHAFUKA,
ANAOGOPA KUKOSEA VIPIMO VYA ZEGE.

Ukiona ngalawa usidhani kuna MVUVI.... ndo hayooo DALILI HIZI ......... kumbe wengine tumooooo Lol

emu-three said...

Kutafuta kula sio mchezo, ukifikiria gari lile gari, yale maposho na zile honeymoon za kila mara, je unaweza ukazikosa, je nifanyeje ili nizipate tena...wakati unawaza haya unaweza ukakumbuka jambo kuwa ni lazima ulifanye ili uendelee kuwepo, na bila kuangalia saa ukajikuta upo mbele kadamansi na kusema,;
'jamani bado nataka kulaaa'
Watu watajiuliza huyu vipi bado unataka kula wakati sie twakuona umeshiba...'
'Ndio sijatosheka, nataka tena...'
Ni kazi kwelikweli, wanashindwa kujua, yale waliyoyafanya miaka mitano iliyopita ndiyo ingekuwa dira yao.Yale matendo yao, yangekuwa yanaongea hata tusingekuwa na haja ya kusikiliza porojo zao majukwaaani, lakini wapi...honeymoon, sana, zimewaghafilisha na sasa wanakurupuka hata kabla muda haujafika. Ombeni kula, lakini subirini kunawa mikono kwanza, na pia ni vyema msubiri kukaribishwa kwanza.

John Mwaipopo said...

mwe!

chib said...

Kumbe ulikuwa uchokozi... ha ha haaa. Haya waliojimwaga hao, tulioshangaa haya... he he hee

SIMON KITURURU said...

Duh!

Bwaya said...

:-D

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___