Thursday, May 6, 2010

DALILI HIZI SIO ZA KWELI.............


Shhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!


Kuna makala ameweka mwanablog mwenzangu Kamala katika kibaraza chake yenye kichwa cha habari kisemacho, 'Kublog ni elimu' na kama ukitaka kujikumbusha unaweza kubofya hapa kusoma habari nzima.

Nimevutiwa na makala hiyo, lakini naomba nikiri kuwa nami nimeelimika vya kutosha katika tasnia hii ya blog, katika namna tofauti. Maana naamini suala la blog siyo la kulifanyia mzaha au la kupita, ni elimu tosha ukiwa makini kwa blog makini.

Labda kuna jambo moja ambalo nilikuwa sijalijua kutoka kwa wanaume na kwa hakika ndiyo maana nasema blog zimenipa uelewa huo, sasa nafahamu kwa kiasi chake. Kwahiyo baada ya kuanza kublog nimejikuta nikiwafahamu wanaume kwa upande mwingine, yaani kufahamu hulka zao na mambo mengine yanayowahusu.

Nakumbuka mwanzoni kabisa wakati naanza kublog nilianza kupata baruapepe nyingi sana kutoka kwa wanaume mbalimbali ambao walikuwa wakinipa moyo na kunipa maelekezo ya hapa na pale juu ya kublog na mambo mengine yatokanayo.

Kupata baruapepe hizo ilikuwa changamoto kubwa na faraja kwangu, kwani sikutegemea sana ingawa nilifahamu nitawasiliana na watu mbalimbali iwe wanablog au wasomaji wasio wanablog. Wapo waliokuwa wakinitumia baruapepe za kutaka kunifahamu zaidi na sikuwaficha kitu nilikuwa nawaeleza historia yangu kwa ufupi.

Kwakuwa natambua kwa ufupi huo unaweza kuwasaidia kunifahamu kwa kiasi fulani.
Kuna baadhi yao ambao nilikuwa nikiwasiliana nao mara kwa mara. Na katika kuwasiliana kwetu huko kwa njia ya baruapepe tulitaniana na kufanyiana mzaha wa hapa na pale ambayo kwangu lilikuwa jambo la kawaida kabisa.


Hata hivyo kuna wakati niliduwazwa na mambo kadhaa ambayo yalinifanya nijisaili maradufu,na kashangaa zaidi. Nasema katika hali ya kushangaza, kwasababu kuna baadhi naona walikwenda mbali zaidi ya mzaha wenyewe. Maana haikuwa utani tena bali kukawa na jambo jingine limeingizwa humo. Sikutarajia hilo kwakuwa kwangu nilikuwa nawasiliana kwa heshima na taadhima.

La haula! nikaanza kutongozwa, tena bila kificho. Aaaah! mweeh! nikaona makubwa haya nitayaweka wapi, madogo yana nafuu. Yaani kumbe yale mawasiliano yetu wenzangu wameyageuza mapenzi? Kumbe ule mzaha umegeuka kitongozeo’?

Nikaduwaa zaidi, kisha nikajiuliza kidogo, lakini nikaishia kunyamaza. Yaani ile midadi ya mzaha ikageuzwa na kudhani nimevutiwa nao kimapenzi.

Haki ya nani hivi! Kaaaazi kweli kweli!

Lakini naomba niweke wazi kuwa hao sio miongoni mwa wanablog wenzangu, na wale tunaowasiliana kwa heshima zote na taadhima, maana hao nimeendelea kuwasiliana nao na tumekuwa tukiheshimiana sana.

Na heshima hii imenipa hamasa zaidi ya kublog na kushirikiana nao daima. Sasa, kuna baadhi ya wanaume huziona dalili za mwanamke kumtaka kimapenzi kwa namna ambayo siyo kabisa.

Na ndio maana mara nyingi mwanamke anapomchangamkia mwanaume na kuwa naye karibu kimazungumzo katika hali ya kawaida, anaweza akajiaminisha kwamba hiyo ni dalili ya kupendwa na mwanamke husika.

Sijui niseme namna gani, lakini hayo ni mawazo ya ajabu kabisa. Jamani hata kuchangamkiana itafsiriwe ni ‘kunogea penzi’? Aaah!

Wallahi hii siyo kabisa, haikubaliki. Na hiyo dalili huwapa wakati mgumu sana wanaume pale wanapogundua kuwa mwanamke husika hakuwa na fikra za kuwa na uhusiano nao kimapenzi kama walivyodhani.

Hayaishii hapo, inatafutwa njia mbadala, ndipo fedha na nguvu itatumika ili kuhakikisha anampata mwanamke huyo na wakati mwingine hata vitisho pale njia hizo mbili zinaposhindwa kutoa matokeo anayotarajia.

Tabia hii ya baadhi ya wanaume inaleta hitilafu. Yaani anaweza kuamini kabisa kuwa mwanamke fulani amempenda kimapenzi, wakati sio kweli. Na anapomtongoza mwanamke huyo na kukataliwa, hapo ndipo mbinu chafu zinapoanza kutumika kwa kuwa wanaume hawakubali kushindwa katika jambo hilo.

Kwa kawaida wanawake na wanaume, wanayo mikabala tofauti katika kuonesha dalili za kupenda. Wakati kwa wanaume kuchekewa, kuchangamkiwa na kutaniwa na mwanamke, kuna maana ya mwanamke huyo kumpenda mwanaume husika. Lakini kwa mwanamke, kufanya chochote kati ya hayo au kufanya yote hakuna maana ya ‘kumpenda’ mwanaume huyo.

Na hapo ndipo suala la kuwa waangalifu linapokuja, hususan tunapofanya masihara na baadhi ya wanaume maana wenzetu wanaweza kutafsiri ‘tunahitaji penzi au kujitongozesha’.

Kwani ule utani na ukaribu wetu kwao unatafsiriwa vibaya. Kila mwanamke anayo dalili ya kuonesha kuvutiwa na mwanaume lakini sio kwa dalili za wazi kiasi hicho.

Waama, Waswahili walikwisha kusema, 'ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo'. Kwa kawaida wanawake huonesha vitendo kuliko maneno....LOL

15 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kutongozwa ni fahari ya mwanamke kamili

unaonaje utuwekee na email hizo za kutongozwa labda tujifunze na kudhibitisha ulisemalo? usije ukawa unajisifia tu jinsi unavyotongozwa mtandaoni

Ramson said...

Kamala isije ikawa nawe ni mmoja wao....angalia usije ukaumbuka akiziweka hapo kibarazani....LOL

Anonymous said...

Mie naogopa kusema lolote.....nisije nikaambiwa namtongoza Koero...LOL

Yasinta Ngonyani said...

Hii mada nimeipenda sana inafundisha na kuelimisha na nitiomba nami niiweka pale kwangu... maana mmmmhhh!Ahsante Koero mdogo wangu.

Faith S Hilary said...

Ah dada...mbona wapo wengi tu hawa wanaume wa namna hii! Inakuwa kichekesho pale wewe mtu unaona tu ni kama marafiki then anatoboa jipu! YALLAH! Most of them hawaelewi maana ya jibu "hapana"...anaanza kukuchunia...KHA! nilikutuma? lol

MARKUS MPANGALA said...

Yaaaaaaaaaallllllllllllllllllaaaaaaaaaaaaaaaa CANDY1 akina nani hao??? ha ha ha Lol jamani hili mbindinge kali sas Mchungaji Koero unachukia kutongozwa wakati enzi zile nikiwa primary dada zangu niliwafuma wakiongelea kuwa siku nyingi hawatongozwa Lol yaani walikuwa wakilalamika

Mmmmh NILIKUTUMA CANDY1???? ULIMTUMA (.......) Lol
Ipo kazi aiseeeee

Raha ya ubwabwa chachandu,
utamu ukizidi sema bandu bandu

Lol sijui nini ila kuna nini sijui

KIDOGO NI KIDOGO,
KIDGODO KINA MNOGO
JAPOKUWA NI KIDOGO

MVUMILIVU HULA MBOVU hamuiiiiiii lakini si mnajua WANAWAKE ni mabingwa kutongoza hapa duniani hata kama hawasemiiiiiiiiiiii bisheni halafu tumsome mwana utambuzi MUNGA TEHENAN katika MAISHA NA MAFANIKIO. Mi nakubali. Lo
Mchungaji anaogopa kutongozwa ili watu wajaribu EMCHEKU kisha wapime kam TBS ha ha ha ha ha MCHARUKOOOOOOOOO

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Koero: Nanukuu "Nakumbuka mwanzoni kabisa wakati naanza kublog nilianza kupata baruapepe nyingi sana kutoka kwa wanaume mbalimbali ambao walikuwa wakinipa moyo na kunipa maelekezo ya hapa na pale juu ya kublog na mambo mengine yatokanayo".

Usishangae kwa hilo kwani kila mtu anaweza kuwa na malengo yake pindi anapokuwa anawasiliana.

Kama ulivosema malengo yanatofautiana.

Na kama vile wengine wanavoweza KUTONGOZA kwa kuwa ati wamevutiwa na GUU, titi, macho, sauti, muondoko, sura nk yawezekana wao walivutiwa na uandishi wako...lol

Pengine kama asemavo Mpangala, walipaswa kutia 'EMCHEKU' ili mambo yawe sawa lakini wakabugi stepu...lol

Mambo mawili:

1: si wa kwanza kutongozwa kwenye blog. wengine wametongozwa Facebook na mitandao mingine ya kijamii.

2: pengine na wababa wanablog watupe uzoefu wao. Je na wao wametongozwa?...lol

Nianze na Kamala na Mpangala..lol

Na nikihitimisha kiukweli: Unadhani hujawahi wewe Da Koero KUTONGOZA hata kwa kumbinyia mtu jicho? Yaani hivi? ;-)

Koero Mkundi said...

Chacha o'Wambura Ng'wanambiti....kusema cha ukweli nilimtongoza sana Kamala lakini akanichunia na kwenda kuoa kwao Bukoba.....Si unawajua WAHAYA walivyo wabaguzi...kasoro Mubelwa yeye amepiga 'EMCHEKU' kwingine..LOL (I wish mkewe hatasoma hii maneno)

Lakini nimekubali matokeo na sasa nimehamishia EMCHEKU kwingine kwa mtu anayeitwaaaaaa..........

Ramson said...

NANUKUU:

"Lakini nimekubali matokeo na sasa nimehamishia EMCHEKU kwingine kwa mtu anayeitwaaaaaa.........."

Bila shaka atakua ni Fadhy Mtanga.....LOL

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Ramson bila shaka umenisoma kuwa kutongozana ni ufahali, ila jibu lako na chacha kalitoa mhusika mwenyeeeewe.

@chacha mimi natongozwa sana kwa malengo tofauti, kuna wanaonitongoza niweka mada waipendayo nk

Fadhy Mtanga said...

....mada tamu hii....halafu ya motooooo...

Godwin Habib Meghji said...

Hapa Da Mdogo Koero tuliosoma saikoloji kidogo, tunajua ni kwanini umeandika hii makala. Ila naamini itasaidia mtu kuelewa.. Hongera na ufurahie maisha mapya.... NAAMINI UMENIELEWA/MNANIELEWA NINAMAANA GANI...
Pia ujumbe umefika kwa walengwa. Ila wasikate tamaa kurusha kete sehemu nyingine, tatizo timing zao ndio hazikuwa sahihi....

Christian Bwaya said...

Ninachoshukuru ni kwamba dada Koero amelizungumzia hili kwa mtazamo chanya.

Kwa anayetongonzwa sidhani kama yapaswa kuwa kero na kwa anayetongoza kwake ionekane ni shauku tu ya ubinadamu. Kutongoza si kosa, kosa kulazimisha mambo. Tusilione suala hili kama balaa fulani hivi. Tulione kama aina nyingine ya fursa za mtandaoni. Ndio mlango haswaa wa nyenzo hizi mpya za mawasiliano.

Unknown said...

Da Koero natumaini haulalamiki kuwa unatongozwa. Ukweli ni kwamba mwanamke kutongozwa kwake ni fahari. Inawafanya wajisikie wanakubalika na 'it makes sense'. Suala ambalo labda lingenikera na kuona umevunjiwa heshima ni pale unapojaribu kumuelewesha mtu kuwa hauko tayari na akawa bado anakung'ang'ania. Ving'ang'anizi ni kama kupe, lakini basi kama haukukutana nao hao kupe basi uko salama. Natumaini "anaitwaaaa" atafahamu nafasi yake na kukuenzi daima.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Koero - hivi ukikata mwaka bila kutongozwa utajisikiaje???

Wanaume pia wamejifunza kuwa ving'ang'anizi kutokana na ukweli kwamba nyie wanawake mkipewa mistari a.k.a kumwagiwa sera a.k.a kutongozwa huwa ni lazima mdengue, eti mnaogopa mtaonekana warahisi. Hamkubali moja kwa moja mtu akajua. Mabrazameni basi inabidi wahakikishe mara mbilimbili kama kweli ndiyo weshaliziwa buyu ama la! Sasa mambo yamebadilika lakini wakati ule tunakua kule vijijini Usukumani mpaka umtongoze msichana
na "ukafanikiwa" mbona ilikuwa kasheshe. Kulikuwa na lugha maalum ya kutumia na kwa bahati mbaya mimi ilikuwa inanipiga chenga kweli mbali na kuwa na waalimu kibao...