Saturday, May 15, 2010

HATIMAYE NIMEPONA!

Kuugua sio kufa jamani......

Baada ya kusumbuliwa na homa ya matumbo ambayo inavutia zaidi ukiita Typhoid, namshukuru muumba kwa kuniponya na sasa ninatarajia kurejea hapa na kuliendeleza libeneke hili la Vukani.

Naomba nitoe shukurani kwa Daktari Aliyenipatia tiba na Wanablog wenzangu wakiwemo wasomaji wa kibaraza hiki kwa kuniombea ili nipone haraka.

Nimefarijika sana na pole zenu na nimejisikia fahari kuona kuwa kumbe kupitia blog hii nimejijengea marafiki wengi kupindukia.

Najua kutoweka kwangu katika mtandao kutokana na kuumwa kuliwakosesha kusoma ujinga wangu ambao kupitia kwayo mmekuwa mkijifunza pia.

Kwa bahati mbaya kutokana na kuumwa nimeshindwa kuandika Tafakari ya Leo. Najua kuna watu ambao watasononeka kutokana na kukikosa kipengele hiki wiki hii, lakini naomba mniwie radhi kwani nitajitahidi wiki ijayo kipengele hicho kiwepo.

Jamani kuugua sio kufa, nimerejea tena…………

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

namshukuru mwenye enzi kwa kukulinda salama na pia kwa kufuata masharti ya daktari kula dawa zote. Ni kweli kuugua sio kufa..

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mungu Ashukuriwe....

Kwa vile kipengele cha Tafakari ya Leo hakipo, basi itabidi niende kanisani leo.

Fadhy Mtanga said...

Pole sana jamani....tunashukuru sana kuwa umepona...huhitaji kutushukuru bloggers....ni wajibu wetu..

Uwe na wakati mzuri sana.

MARKUS MPANGALA said...

Aaaah MCHARUKOOOOOO nimegundua kumbe Mchungaji Koero umeshindwa kujiponya hadi unamshukuru mungu amekuponya? Lol

Aaaah nimegundua unaumwa huu ugonjwa aise, kwanini upate ugonjwa huu???

Aah MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA, TUNAKUOMBA UZIDI KUMPATIA NGUVU HUYU BINTI MKUNDI.... MAANA AMESHA EXPIRE, matumbo yanamkonyeza..

MUNGU UFAHAMU KUWA HUYU NI DHAHABU, UMTUKUZE DAIMA NA KUMPATIA ULINZI MARA KWA MARA.
AMEN

tipempani N'nungu akuike Bwino kumeneko anjatu. AMEN

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mpangalaaa! hiyo ndo zawadi ya besidei yako kwa Koero?..lol

Karibu Da Koero

mumyhery said...

Pole sana Koero, tumshukuru Mungu

Faith S Hilary said...

duh! hata sikuwepo ndio hata sijui kulikuwa kunaendelea nini ila pole sana dada!! I am glad u r feeling better...pole!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwanini hukufa???