Sunday, May 16, 2010

HATIMAYE YAMETIMIA: DDT KUANZA KUTUMIKA KUDHIBITI MALARIA

Kuna wakati niliwahi kushauri serikali iridhia matumizi ya dawa ya kuuliwa wadudu ya DDT ili kuteketeza mazalia ya mbu, ukitaka kujikumbusha unaweza kubofya hapa. Pia baada ya uzinduzi wa Zinduka malaria Haikubaliki niliandika hapa kibarazani kwangu kumshauri Rais kwamba ni vyema angetumia fursa ile ya uzinduzi kuhalalisha matumizi ya dawa hii ya DDT bila kujali kelele za wanamazingira na wafanyabiashara. Ukitaka kujikumbusha unaweza kubofya hapa

Leo hii nimefarijika baada ya kusoma katika Gazeti la Mwananchi kuwa hatimaye serikali imeridhia matumizi ya dawa hiyo. Hao wanaopiga kelele wajaribu kuangalia nchi zilizofanikiwa kuwatokomeza hao mbu kwa kutumia dawa hiyo bila kuleta madhara kama wanavyodai. Mbona hapo Zanzbar dawa hiyo imekuwa ikitumika na hakuna athari zilizoripotiwa kama inavyochagizwa na hao wahafidhina?

Tuacheni unafiki, Tufikie mahali tukubali kuwa inatosha na tuitokomeze malaria kwa nguvu zetu zote.

******************************************


DDT kuanza kutumika kudhibiti malaria

Na Sadick Mtulya wa Gazeti la Mwananchi.


SERIKALI imesema pamoja na kwamba inagawa bure vyandarua ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa malaria, ipo mbioni kupuliza dawa ya DDT ili kuua mazalia ya mbu.Kufuatia mpango huo, serikali imewataka watanzania wasiwe na hofu kuhusu DDT na kwamba madhara yake si makubwa kama inavyoelezwa.
Akizungumza na Mwananchi juzi jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa alisema nchi nyingi Dunia zimefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kutumia DDT na kwamba dawa hiyo itakuwa ikipuliziwa katika kuta na dari za nyumba.“Wananchi waondokane na hofu kuhusu DDT kwani hadi sasa hakuna ushahidi wa kimaabara unaoonyesha kuwa kuna mtu ameathiriwa na dawa hiyo.
Dawa hii itakuwa ikinyunyuziwa katika kuta na dari za nyumba na mbu akitoa eneo hilo hufariki,” alisema Profesa Mwakyusa Profesa Mwakyusa alisema dhana iliyojengeka kuwa DDT inasababisha saratani si ya kweli na kwamba hadi sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kupata ugonjwa huo kutokana na dawa hiyo.
Alisema DDT itakuwa ikipuliziwa kutegemeana na eneo ambalo watu wanaugua kwa wingi ugonjwa wa malaria na kwamba mpango huo, umeanza katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.Waziri Mwakyusa pia alisema tayari vyandarua milioni tisa vya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa malaria vimegawiwa bure nchini kote.

Alisema idadi hiyo ni kati ya vyandarua milioni 14 vilivyotolewa na serikali pamoja na taasisi na mashirika binafsi.“Vyandarua milioni tisa vimekwisha gawiwa bure nchini kote,” alisema Profesa MwakyusaKatika hatua lingine, matokeo ya utafiti wa hali ya magonjwa ilivyo nchini, inatarajiwa kutolewa mwezi juni mwaka huu.Hatua hiyo inafuatia timu ya waataalamu wa afya kukamilisha utafiti wa magonjwa yote, ulionza mwaka jana.

“Mwezi Juni mwaka huu, wizara yangu itatangaza matokeo ya utafiti wa jinsi hali ya magonjwa ilivyo nchini. Hii ni baada ya timu ya wataalam wa afya kukamilisha utafiti ulionza mwaka jana,” alisema Profesa Mwakyusa.Profesa Mwakyusa alisema Tanzania ilianza utaratibu wa kufanya utafiti wa magonjwa mwaka 1996 na kwamba kila baada ya miaka minne utafiti huo hufanyika.

5 comments:

kibunango said...

Pamoja na jitihada zako kuhusu DDT mimi binafsi napinga matumizi hayo...

Ramson said...

Kibunango sina haja ya kulumbana na wewe, lakini kuwa mkweli kwa nafsi yako, hivi ni athari gani ambazo umezishuhudia kule Zanzibar zinazotokana na dawa hii ya DDT?

Mie naona hapa tunaimba wimbo ule ule wa mataifa ya Magharibi ambayo yanataka kuigeuza Afrika kuwa soko lao la Madawa.

Tatizo letu sisi Waafrika tunaamini kile linalosemwa na wenzetu wa Magharibi bila kupima jambo hilo kwa kiwango cha Utambuzi.

Hebu msome dada Subi hapa:

"Thanks for sharing the study and findings.
I think we still have a war to fight in this. At the moment Malaria seem to be in the winning side. A multi approach is required in eradicating this disease. I wonder why there is no much talk about DDT anymore. Please do not bombard me with it's ill health effects - what's more ill than a death of a child due to Malaria every 1 minute that passes us by? and oh, about the environment concerns - please, give me a break, how much have the third world cared for the environment? and what does the Global Warming report project towards Sub Saharan Countries? - Expect the worst. What good does the environment do if all it does is propagate the breed of more mosquito and other disease vectors? I already know about that, am not ready for a lecture now.

I still defend and advocate for the wise use of DDT in eradicating Malaria. We have used it before at our home in Moshi and for the first 22yrs of my life I never suffered any illness due to Malaria until one stupid day after just a 1 month's field work in Mlali, Morogoro. My kidneys are just perfect, my relatives as well and none had ever been diagnosed with Cancer due to the DDT we carefully used to kill mosquitos. Why did we stop using it? Well, where can we buy it? It's no more in the shops and "Duka la Ushirika" is no more. Politics! Politics! Politics! Too much politics will keep on dividing and killing us even on things that we needed no any tiny bit of it in. Why aren't Italians suffering from the ill effects of DDT? This notion of just agreeing and accepting everything sometimes tickles me off badly big time. Why would they say, "no don't use DDT, it's bad"....after they themselves used it? Puhleez! Alright, say they are right, okay, what difference does it make except changing the mode of death? It's still a death anyway, isn't it?

While others are pushing and making Nuclear Bombs, we on the other end are can not agree to make DDT for safe local use, and we proudly boast that we have distinguished scientists? Yeah, distinguished scientists my foot! Yaani we are debating about making and using DDT carefully as if we are careless? Boy, does anybody need proof what we are. Basically by agreeing with them to not use DDT, we have accepted that we can't be careful. Please give a me a good reason to dispute the benefits of using DDT (and please do not repeat what I said I already know - there is no point of doing that).
What a pity!
I think I am talking to myself too much here.
Have a good week!"

.end.
Subi

Yasinta Ngonyani said...

kwa kiswidi

Miljögift
DDT är ett miljögift och räknas som en långlivad organisk förorening. För insekter, till exempel mygg, är DDT direkt dödligt. Men ämnet kan även ansamlas i fettvävnader. En mus får i sig DDT från vegetationen, en fågel äter många möss och får i sig deras doser, ett lite större djur äter många fåglar och får deras doser och så fortsätter det. De stora rovdjuren är de som i slutändan får det tunga lasset, och störningar i fortplantningen är ett faktum. Havsörnen var under en lång tid svårt utrotningshotad på grund av miljögifter och DDT kan ha spelat en roll. Enligt vissa forskare orsakade ämnet äggskalsförtunning, vilket gjorde att djuren inte kunde ruva sina ägg utan att de gick sönder.
DDT användes i Sverige fram till 1980-talet i utvärtes läkemedel mot skabb, huvudlöss och flatlöss.

NA HAPA NIMEJARIBU KUTAFSIRI KWA NJIA YA GOOGLE SIJUI KAMA ITAELEWEKA

Kizimamoto
DDT ni sumu ya mazingira na ni kuchukuliwa na kuendelea kikaboni kizimamoto. Kwa wadudu, kama vile mbu, DDT ni lethal moja kwa moja. Lakini pia somo hujilimbikiza fatty tishu. mouse anaweza kuwa katika DDT kutokana na mimea, na ndege kula panya wengi na huweza wa viwango vya wenyewe wao, kubwa kidogo kula wanyama ndege nyingi na kupata dozi zao na hivyo unaendelea. The predators kubwa ni wale ambao mwisho juu na kupakua mizigo, na matatizo ya uzazi ni ukweli. Sea Eagle ilikuwa ni ugumu wa muda mrefu katika hatari ya kufa kutokana na föroreningar mazingira na DDT, wanaweza kuwa na mchango. Kulingana na baadhi ya watafiti, na dutu hii husababishwa äggskalsförtunning, ambayo ilimaanisha kwamba wanyama hakuweza kizazi mayai yao lakini kwa sababu ya kuvunja chini.

DDT ilitumika katika Sweden mpaka miaka ya 1980 katika madawa ya topical kwa scabies, chawa kichwa na kaa.

Bennet said...

hii sasa afadhali maana kulalia vyandarua sehemu za joto ni usumbufu vinaongeza joto halafu ukiwasha kifeni chako wakati uko ndani ya chandarua basi vumbi lote lililonata kwenye chandarua litakuishia wewe

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___