'Mfalme Suleman akaagiza mtoto yule akatwe kichwa'
“Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku Mungu akamwambia omba utakalo nikupe Sulemani akasema umemfanya mtumwa wako Daudi baba yangu fadhila kuu kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli na haki na katika unyofu wa moyo pamoja nawe, nawe umemwekea fadhila hii kubwa maana umempa mwana wa kuketi kitini mwake kama ilivyo leo na sasa.
Tafakari ya leo ningependa tusome katika 1 WAFALME 3:5-13. kisha tutafakari kwa pamoja.
“Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku Mungu akamwambia omba utakalo nikupe Sulemani akasema umemfanya mtumwa wako Daudi baba yangu fadhila kuu kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli na haki na katika unyofu wa moyo pamoja nawe, nawe umemwekea fadhila hii kubwa maana umempa mwana wa kuketi kitini mwake kama ilivyo leo na sasa.
Ee BWANA Mungu wangu umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu nami ni mtoto mdogo tu, sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia na mtumwa wako yu kati ya watu wako uliowachagua watu wengi wasioweza kuhesabiwa bila kufahamiwa idadi yao kwa kuwa ni wengi kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako na kupambanua na mabaya maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi.
Neno hili likawa jema machoni pa Bwana ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. Mungu akamwambia kwa kuwa umeomba neno hili wala hukujitakia maisha ya siku nyingi wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako wala hukutaka roho za adui zako bali umejitakia akili za kujua kuhukumu basi tazama kama ulivyosema.
Tazama nimekupa moyo wa hekima na wa akili hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. Na mambo yale yote usioyaomba yote nimekupa mali na fahari hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe siku zao zote.
Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi. Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalem, akasimama mbele ya sanduku la agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.”
Na katika hiyo hiyo Wafalme hebu tusome katika
1 WAFALME 3:16-28.
“Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. Na mwanamke mmoja akasema, Ee, Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. Kisha siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu.

Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. Akaondoka kati ya usiku akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe! amekufa.
Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.
Ndipo Mfalme Suleman akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo, bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu.
Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme, kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee Bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai , wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, asiwe wangu wala wako; na akatwe. Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake.
Na Israel wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme; wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.”
Na Israel wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme; wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.”
Labda wewe unayesoma hapa, nikuachie swali hili utafakari, ‘Je, mungu akikwambia omba utakalo nikupe, utaomba nini?
Tafakari hii itaendelea Jumamosi ijayo……….
8 comments:
Nitamwomba Mungu awalinde Mayatima wote na awape maisha mema,
Eeeh , Mungu a uwalinde Yatima wote amina. Upendo Daima.
"Mungu kama watu wakifa wanazaliwa tena wakiwa katika miili mingine, basi mie naomba nikifa, nizaliwe katika mwili wa dada Yasinta ili niwe kama yeye......."
Koero hilo ndilo ombi langu nitakalomuomba mungu kama akinitaka niombe chochote ninachotaka.....Ha ha ha haaaaaa
Tegelezeni
Busara!! Ndio ningeomba busara kwani ni kiona mbali muhimu maishani. Uwezo wa kufikiria na kuona mambo katika upeo wa tofauti. Kuweza kuona madhara ya yale yaonekanayo lulu kwa sasa na kumbe sivyo...Niombee da Koero tafadhali
Ntaomba BUSARA kama Kaka Mrope. Lakini sitaiomba kwangu tu. Ntaomba BUSARA kwa jamii yetu. Jamii yetu nikimaanisha DUNIA.
Ni kwa busara tutakuwa na UPENDO, AMANI NA MAISHA YASIYOTEGEMEA PESA NA UBABE.
Ntaomba busara za kuelimisha na kuelimishwa. Za kusikiliza na kusikilizwa, za kuwa sehemu ya suluhisho kwa kila sehemu ya tatizo ninayohusika.
Shukrani Dada
Ntaomba ukimya kwani ni katika ukimya yote huwezekana!
Nitaomba moyo wa kuridhika na kile nilichobarikiwa nacho. Tamaa ya mambo ndio imekuwa chachu ya matatizo mengi duniani. Kuridhika na hekima vyaweza kufaa sana katika ulimwengu huu!
nitaomba kupelekwa SACH KHAND
Ningeomba kuwa na hekima.
Post a Comment