Tuesday, May 18, 2010

WACHAGA NA ‘KITOCHI,’WAPARE NA ‘KIBARA CHA MAWA!’

Bila Kitochi kwa Wazee wa Kichaga, mazungumzo hayatanoga!

Jana nilikuwa natafakari kauli ya Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete juu ya hekaya za Wachaga na Kitochi, Wakati alipokuwa akiongea na viongozi wa dini juu ya mustakabali wa nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu.

Raisi alisema kuwa ni vigumu kudhibiti takrima katika uchaguzi mkuu, akatolea mfano kuwa kule Klimanjaro ni vigumu kuwakusanya Wazee wa Kichaga bila kuwapa Kitochi. Kitochi kwa kule Kilimanjaro ni kipimo cha pombe ambacho naambiwa kina ujazo wa nusu lita.

Sina haja ya kurejea kile alichokieleza Rais kwa undani kwa sababu hata hivyo msajli wa vyama amedai kuwa ule ulikuwa ni utani tu wa Rais kwa iongozi wale.

Katika kutafakari kwangu niliwaza, hivi na Wapare nao wakidai 'Kibara cha Mawa' itakuwaje? Maana kila kabila lina mila zake za kuwaita wazee na kuwakutanisha pamoja. Kama ilivyo kwa Wachaga kuita Kitochi, wapare nao wana utaratibu wao wa Kibara cha Mawa. Yaani kibuyu cha pombe.

Mara nyingi Kibara cha Mawa hutumika pale mtu anapowakusanya wazee ili kuzungumza nao jambo au kama mtu ameleta posa na anataka ijadiliwe na wazee au hata mashauri mbalimbali yanayowakutanisha wazee, basi Kibara cha Mawa ni lazima kiwepo.

Je kwa makabila mengine kama Wasukuma, Wangoni, Wahaya, Wakurya, Wajita, Warundi, Wanyakyusa, Wahehe na makabila mengine wanaitaje utaratibu huu?

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

obufumolelo

Fadhy Mtanga said...

...pale hakuna cha utani mchungaji...ndo ukweli kuwa takrima binti rushwa ndo kishindio.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Dada Muamshaji: nachelea kutosema kabisa hiyo kitu kwa kikurya inaitwaje kwa kuwa nina hasira kwa kiongozi wa nchi akila njama na 'viongozi' wa dini kulalalisha rushwa :-(

Huu ni ujinga kwa kuwa WAZEE huwa hawaitwi kwa mambo ya kajinga bali kwa mambo ya maana. Ndiyo-kijinga kwa kuwa mtu anapowaita wazee unatakiwa kutoa hoja ama kuzungumzia jambo la maana lakini sivo kwa wanasihasa wetu. Wao wanawatumia wazee kama daraja la kupata kile wanachokitamani ili waweze kuwanyonya wananchi. Na matokeo yake wazee sasa wamekuwa wakitumika ama kutumiwa kuliangamiza taifa.

Ningefurahi kama wazee ndo wangemuita mwishiwa na kumuuliza juu ya wafanyikazi na siyo yeye kuita kakikundi ka watu (vijana wakiwamo) kwa jina la WAZEE wa Dar wakati pengine wanatoka ILALA tu na wote wamevaa KIJANI tupu:-(

Tuombe (kwa maombezi yako ya KITAKATIFU kama siyo KITAKAVITU), wazee wawaite watu na kuwaomba wagombee na si watu wawaite wazee kuwambia ujinga wao.

Anonymous said...

Mwaka huu mpaka uishe, au bora zaidi awamu hii na inayokuja mpaka iishe tutaona drama za ajabu sana. Sijui kama tatizo ni leadership vacuum ama nini. Ama kweli kama maandiko (Bible) yasemavyo "without a vision, a nation perishes"! Kristu uturehemu!