Friday, August 13, 2010

VISA VYA HUYU KIUMBE MWANAUME!

'Kwenye swala la mapenzi wanaume hawana mzaha'

Katika Gazeti la Mwananchi la hivi karibuni la May 18, 2010, kuna habari iliyoandikwa na mwandishi Anthony Kayanda wa Kigoma ambayo ilinisikitisha sana. Habari yenyewe ni ile iliyohusu mtu mmoja kuuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani kwa tuhuma za kutembea na mke wa mtu.Kwa mujibu wa Gazeti hilo, tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kitagata kilichopo katika tarafa ya Makere, Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

Marehemu ametajwa kuwa ni Ally Bwisigwa ambaye ni mkazi wa kijiji hicho.Ilidaiwa kwamba Marehemu alikuwa akitembea na mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Perusi ambaye aliwahi kuolewa na Hassan Rashid mkazi wa Kasulu Mjini na waliishi pamoja kwa muda mrefu kabla ya mume huyo kufungwa gerezani.Baada ya mumewe kufungwa, Perusi alirudi kijijini kwao huko Kitagata na ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na marehemu.


Inadaiwa kuwa baada ya Mume huyo kutoka Gerezani alimuonya mtuhumiwa mara kadhaa kuacha kutembea na mkewe lakini marehemu aliendelea na mchezo wake huo mchafu.Inadaiwa kuwa Hassan alifanya majaribio mawili ya kutaka kumuua marehemu kwanza kwa kutaka kumgonga na pikipiki na tukio la pili lilikuwa ni lile la kumchoma kisu ambapo hata hivyo kisu hicho hakikumpata.
Nimesema kuwa tukio hilo limenisikitisha sana kwa sababu bado nashindwa kuelewa hivi inakuwaje mpaka mtu unapoteza maisha kwa sababu ya mwanamke, tena kibaya zaidi mke wa mtu!Ingawa inasemwa kwamba wanawake ni viumbe wa ajabu lakini naamini wanaume ndio viumbe wa ajabu kupindukia.
Kwa nini ninasema hivyo? Ninasema hivyo kwa sababu, wanawake kwa ujumla wao wanavyo vibweka vyao katika swala zima la mapenzi, lakini ukija kwa wanaume naamini nao wanavyo vibwekwa vyao tena vya hatari ukilinganisha na vile vya wanawake.Kwa mfano, hivi ni mara ngapi tumeshawahi kusikia baadhi ya wanaume wakiamua kujinyonga kwa sababu ya kushindwa kuwashawishi wanawake wanaowapenda?
Namini kuwa matukio ya aina hiyo yapo sana na sio kwa huko nyumbani tu bali pia hata katika nchi zilizoendelea. Linapokuja swala la mapenzi kuna baadhi ya wanaume wanakuwa kama Nyati waliojeruhiwa, na ndio sababu unaweza kukuta baadhi ya wanaume wanajiingiza kwenye vitendo viovu kama vile vya wizi au ujambazi kwa lengo la kuwashawishi wanawake wanaowapenda ili wawakubali. Wakati mwingine hujiingiza kwenye matumizi ya Pombe kupita kiasi au hata matumizi ya Bangi na madawa ya kulevya kutokana na kuachwa na wanawake wanaowapenda.
Tabia hii ya wanaume kuhatarisha maisha au hata kupoteza maisha kama tulivyoona katika tukio hilo la Kigoma ni la tangu enzi za kale. Kuna simulizi nyingi tulikuwa tukisimuliwa enzi za utoto wangu huko nyumbani kwamba kuna wakati wanaume walikuwa wakipigana ili kumgombea mwanamke na shujaa anayeshinda katika ugomvi ndiye anayemchukuwa mwanamke anayegombewa.
Inaonekana wazi kwamba uwezekano wa mwanaume kufa mapema au kuhatarisha maisha yake ni mkubwa ukilinganisha na ule wa wanawake. Na hiyo inatokana na wanaume kupenda sifa na kutaka kuwamiliki wanawake wawapendeo. Kuna matukio mengi ya kusikitisha ambayo huwa tunayasoma katika vyombo vyetu vya habari ambapo matukio kama yale ya mwanaume kumuua mwanaume mwenzie ili kumpata mwanamke ampendae ni vya kawaida kabisa.
Kwa mfano katika tukio hilo la Kigoma, licha na kukoswa koswa kuuwawa mara mbili lakini marehemu hakukoma kutembea na mke wa mwenzie, mpaka akasababisha kupoteza maisha.Hivi kumekuwa na uhaba wa wanawake kiasi cha kupelekea baadhi ya wanaume kuhatarisha maisha yao au kupoteza maisha kutokana na kumgombea huyu kiumbe mwanamke au kuna kitu kingine kinachotafutwa hapo?

Ni aghalabu sana kusikia mwanamke kamuua mume baada ya kumfumania au kumuua mgoni wake tofauti na wanaume. Kama ukipima jambo hilo kitakwimu basi utapata idadi ya wanaume ya kutosha ukilinganisha na ile ya wanawake.
Kimsingi wanaume wamewageuza wanawake kama mali zao wanazozimiliki na hiyo ndio sababu inapotokea kumfumania mkewe au mchumba wake akiwa na mwanaume mwingine mambo mawili yanaweza kutokea, kwanza atamuadhibu mgoni wake au hata kumuua kisha mke naye atasulubiwa au hata kuuawa.
Lakini, pale anapofumaniwa mwanaume mambo huwa ni tofauti sana. Kuna uwezekano mkubwa wa mke huyo kusulubiwa kwa sababu amemfumania mume na wakati mwingine hata huyo mgoni anaweza kushirikiana na mume huyu kumuadhibu huyo mwanamke aliyefumania.Nadhani kuna haja ya wanaume kujikagua upya na kubadili mwenendo wao mzima juu ya matendo yao ili kuepuka kupoteza maisha kwa jambo ambalo wangeweza kuliepuka.

Na: Yasinta Ngonyani. Bofya hapa kumsoma

8 comments:

Maisara Wastara said...

Hii mada imetulia mwanakwetu....
Labda nimuulize dada Yasinta kuwa alifikiria nini kuandika mada hii?

emu-three said...

Alifikiri nini alipoandika hili? ni swali muhimu, lakini kila mvuta kamba huvutia kwake, eti, ndio unaweza ukavuta kamba kuelekea kwa mwenzako , hapana.
Ukweli ni kuwa kwenye mapenzi hukosi wivu, ila kuna wivu mzuri na mbaya, na kama wewe humuonei mpeni wako wivu humpendi kisawasawa, utajifnaya tu huoni wivu lakini moyoni unaumia.
Ni kweli wanaume wanamiliki kwa nguvu haki ya mapenzi na kujiona wao ndio watawala, hata ikitokea kosa kwa upande wake ni bahati mbaya ila kwa mwenzake ni makusudi..

SIMON KITURURU said...

Kama alivyosema Emu -Three. Kila mvuta kamba huvutia kwake. Mie naona wanawake ndio kasheshe ila staili tu ya wafanyavyo katika kisasi au hata kuumiza mtu ndio inaweza kuwa inadanganya watu macho. Ni rahisi kushuhudia Mwanamume anapiga mtu , lakini si rahisi kustukia mwanamke akitumia silaha kama sumu.

Na tukumbuke tamaduni na staili za watu za hata wakikasirika hutofautiana katika kuzitoa ndio maana utasikia kwa mfano nikitumia watani zangu wachaga utaambiwa Wanawake wa kichaga wa kutoka eneo fula ogopa ni katili, na wa upande fulani hao pesa tu ndio dawa.

Au utasikia Kabila fulani ukiwaudhi hawakawii kujinyonga. Na ndio hata kimataifa ni hivyo hivyo kwani hukawii kusikia Wasomali wanaume kwa visasi balaa kama tu Wanawake wa Kirusi.

Kwa hiyo kuna uwezekano kabisa kuwa hasira ziondolewavyo hutofautiana na usidanganyike kwa kudhani kwa kuwa mtu hajachoma mtu kisu basi hajaua kwa sumu katika kutuliza kilekile kitu hasira.


Ntarudi tena!Kunauwezekano nimeandika haraka na hoja imepotelea ndani ya mistari ya sentensi za harakaharaka

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza kabisa namshukuru mdogo wango Koero kwa kuiendeleza hii mada. Maisara Nilipoiandika mada hii nilikuwa na mawazo mengi sana kichwani mwangu kwa mfano kwa nini wanaume ni wababe sana na kwanini sisi wanawake tunakubali tu. Ni kama nisemavyo "ya kwamba je? hatutaki kufunguka? kwa kuwa tumejifunga mno na pia tunaamini kuwa wanawake hhatuwezi na kwamba nataka imani hii siku moja itakuja kufa

Koero Mkundi said...

Nilijua hii mada itawagusa wanaume, lakini alichandika dada yangy Yasinta kina ukweli kwa asilimia 100.

Pamoja na sisi wanawake kuwa na makasheshe yetu lakini tukiangalia mizania, wanume wamezidi tena sana.

Ukichunguza maugomvi ya wanaume mata nyingi chanzo ni mwanamke, kwa mfano kule Marekani kuna kipindi jinamizi hilo liliwaandama wasanii kiasi cha kupelekea kuwapoeza wasanii maarufu TUPAC OMAR SHAKUR NA CHRISTOPHER WALLACE aka NOTORIOUS BIG.

Chanzo cha waliokuwa maswahiba hao wawili kutoan roho ilikuwa ni Mwanamke.

Huo ni mfano mmoja kati ya mingi ambayo imetamalaki hapa duniani. sikatai wanawake kujitoa roho, hilo lipo, lakini je chanzo ni nani? kuna idadi ya kutosha ya wanaume ambao wamesababisha vifo vya wake zao kutokana na aidha wivu au ukatili.

Je mpaka hapo mnabisha?
nakuuliza wewe Kituuru...!!!

Markus Mpangala said...

ha ha ha ha ha MCHARUKOOOOOO!!

Mama mchungaji Koero ni kweli kwamba TUPAC alipobashiri hataishi zaidi ya miaka 25 ilikuwa sababu ya mwanamkeeeeeee? ndiyooooo ni MAMA YAKE yule ni mwanamkeeeeee au yule waliyemchungulia UVUNGUNI yaani FAITH EVANS???

ha ha ha Haaa maana milazo ya TUPAC a.k.a Makaveli na BIG POPPA a.k.a BIG SMALLS a.k.a Christopher Wallace chanzo ni mwanamke??? Duh hapa panahitaji AYA za kunithibitishia VIFO vya hawa nguli wa OLD SKUL a.k.a Hardcore rap a.k.a Hipo Hop hebu msikilize katika milazo hii ya UNTIL THE END OF TIME(1999), 7 DAYS THEORY.

halafu rudi kwa BIG POPPA msikilize kwa wepesi LIFE AFTER DEATH, au WHO SHOT YOU.

labda kuna kitu au hamna kitu.... lakini hii ya mwanamke na majigambo ya kihip hop zamani daaaaaahhhh! YATAKA AYA halisi.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
naacha hilo.....

MCHARUKOOOO

popote penye mafanikio ya mwanaume pana mwanamkeeeeeeeee. Na popote penye uharibifu kwa mwanaume kuna

mwanamkeeeeeeeee.....
nimemkumbuka mshikaji wetu MUSIBA pale Mabibo hostel mwaka jana alichoma demu wake kisu kisa kalalamikaaaaaa weeeeee miezi kibaoooo jamani asali wanguuuuu mwanamkeeee wewe mbona unanisalitiiiiii!!!

asali wangu mbona hivi iiiiiii!!! kumbe kuna likigogo fulani kutoka wizara fulani akawa anamrubuni mwanamke yule.

Sawa, kwanini hakumwambia mwenzie waachane tu ili ajiepusha na kisu????? mi najiuliza tu maana sijui itakuwaje kwangu lakini naona kuna uhaba wa kitu hapa katika haya mauaji ya kuchomana visu.....

MCHARUKOOOOOOOOOOOOO

wanawakeeeeeee aaaaah amueni tu achaneni na mwanaume kiumbe huyu anawaghasi sanaaaaaaa AMUENI basi kuweni WASAGAJI amueni tuuuuu kwani nini jamaniiii mizinguo hiii>>....

aaah amueni bwanaaaaa tusitishane hapa waungwanaaaa TUPOTEZEENI wanaume hawana dili wala nini au vipi FUNGUKENI tu amueni kuuza MIILI wasinunue wanaumeeeee,

amueni tu si mnajua siku hizi watu wanapiga sodoma na gomora jamaniiii amueniiiii tu MASHOGA wapo kibaooooo mitaani amueni wanawake nawaunga mkono........

nendeni songeni mbeleleeeeeeee kuleeeeeeee haya mchakamchaka jinja alimselema alija ha ha ha haya haya haha ha ha ha

MCHARUKOOOO bwana kwani nini tunaletea michosho hii.... kuna haja ya kunadi hii mipango jamaniiii amueni tu songeni mbele msitafute MABUZI wala WATANGAZA NIA...... woooooooooohhhhhhh lliiiiiiiiiii

amueni jamaniiii acheni KUZAAAAAAA wanaume zaeni WANAWAKE TUUUUU kwani nini jamani mimi sichangii hayo MATOKEO ya TATIZO nataka tumwuliza huyu jamaa anaitwa MWANAUME aaache wanawakeeeeeeee......... n

ao wasitake kusema yule kaka kafanya hiviiiii au vileeee AMUENI msipigie kura Dr Slaa .....

kwanini nini kiumbe huyu mwanaumeeeee AAAAHHH MUULIZENI HUYU MUNGU kwani hayo hayaoniiiiiiiiii

ebwanaaa nuksi hizi magumashi mtupu naona magazeti tuuuu sioni sura ya mwanamkeeeeeeeee

MCHARUKOOOO

kwanini nini jamani............ ngoja nikaogeleee ziwani kwetu NYASA ........ magumashi hapa jamaniiiiiiiii wala msinibipuuuuuuu wanawakeeeeee

SIMON KITURURU said...

@ Da Koero: Emu -Three alisha mali hoja kwa kusema :

``....kila mvuta kamba huvutia kwake...´´:-(

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___