Saturday, August 28, 2010

TAFAKARI A LEO: BEN CARSON, DAKTARI ALIYETHIDITISHA KUWA HAKUNA MTOTO MPUMBAVU

Dk. Ben Carson akivishwa nishani ya Uhuru na Aliyekuwa Rais wa Marekani G. W. Bush


Mojawapo ya vitabu vyake vilivyojizolea umaarufuMapacha Ladan na Laleh Bijan wa Iran ambao Operesheni yao iliyoongozwa na Ben Carson ya kuwatenganisha haikufanikiwa, walifariki wote wawili


Daktari Benjamin S. Carson (amezaliwa tar. 18 Septemba, 1951) ni daktari na mtaalamu wa Nyurolojia, na pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia kwa watoto katika hospitali ya Johns Hopkins huko nchini Marekani. Alitunukiwa na raisi medali ya uhuru mwaka 2008

HISTORIA YA ELIMU.

Benjamin Solomon Carson alizaliwa katika eneo la Detroit katika jimbo la Michigan. Mama yake, Sonya Carson, aliacha shule akiwa katika daraja la tatu na kuolewa na Robert Solomon Carson, aliyekuwa mchungaji mzee zaidi katika eneo la Tennesee, wakati mama yake Ben akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu.

Wakati Carson akiwa na umri wa miaka nane tu, wazazi wake waliachana. Mama Carson aliachwa kuwalea Benjamin na kaka yake Curtis, yeye mwenyewe. Alifanya kazi katika sehemu mbili au hata tatu kwa mara moja ili aweze kuwatosheleza watoto wake wawili. . Mwanzoni Carson alikuwa na maisha magumu shuleni. , hali iliyopelekea kuwa wa mwisho mara kadhaa katika darasa lake. Alikuwa akiitwa majina mbalimbali kutokana na hali hiyo, hivyo ikapelekea kukua kwa hasira kali ndani yake.


Akiwa amedhanmiria kubadilisha maisha ya mtoto wake, mama yake Carson akazuia muda wake wa kuangalia televisheni na kumzuia kutoka nje kila siku hadi pale atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku. Mama yake Carson alimtaka Kusoma vitabu viwili kutoka maktaba na kuandika taarifa juu ya vitabu hivyo kila wiki, bila kujali elimu yake ndogo, hata hivo hakuweza kusoma vitu ambavyo vilikuwa vimeandikwa.


Lakini mapema, Carson alimshangaza mwalimu wake na wanafunzi wenzake kufuatana na maendeleo yake. Anakumbuka “Ni wakati ule ndipo nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu” anagundua baadae. Carson anaendelea kuwashangaza wanafunzi wenzake na ndani ya mwaka mmoja alikuwa na ujuzi na kuwa katika nafasi ya juu katika darasa lake.


Baada ya kugundua kuwa alitaka kuwa daktari wa magonjwa ya akili, Carson alimaliza shule na matokeo mazuri yenye heshima na hivyo alijunga na chuo kikuu cha Yale ambapo alipata shahada yake ya kwanza katika maswala ya saikolojia ya akili. Pschology. Baada ya kutoka Yale, aliendelea na shule ya udaktari ya michigan, ambapo hapo ndipo nia yake ya kuwa daktari wa magonjwa ya akili ilipobadilika na na kuwa daktari wa mishipa.

Uwezo wake mkubwa wa kuona na uwezo wake wa kufikiri haraka ulimfanya awe daktari wa upasuaji mzuri zaidi Baada ya kumaliza shule yake ya udaktari, alikuwa daktari wa mishipa msaidizi katika hospitali ya Johns Hopkins katika jimbo la Baltimore. Akiwa na umri wa miaka 33, alikuwa profesa wa hospitali na pia mkurugenzi wa idara ya upasuaji mishipa ya watoto.


KAZI ZAKE ZA MAPEMA.


Mwezi wa tisa mwaka 1987, Carson alifanya upasuaji wa kutenganisha mapacha wenye umri wa miezi saba, waliokuwa wameungana katika sehemu ya kichwa. Carson alikuwa ndiye kiongozi wa upasuaji huo mgumu, Mwaka 1997, Carson pamoja na timu yake, walienda Afrika ya Kusini, kuwatenganisha Lukas na Joseph Banda kutoka Zambia. Watoto wote wawili waliweza kuishi baada ya upasuaji na hakuna hata mmoja wao aliyepata uharibifu wa ubongo. Watoto hao wa Banda walikuwa ni watoto wa kwanza walioungana kwa upande wa juu wa vichwa vyao kuweza kuishi baada ya upasuaji. Upasuaji huo ulifanyika kwa saa 28.


Mwaka 2003, Carson alikuwa moja kati ya madaktari waliofanya upasuaji wa watu wazima waliokuwa wameungana katika sehemu ya vichwa, Ladan na Laleh Bijan. Lakini wote hawakuweza kuishi baada ya upasuaji. Alipoulizwa kwa nini alikubali kufanya upasuaji wa kubahatisha kiasi hicho alisema, ndugu hao walikuwa wamekubali bora wafe kuliko kuendelea kuishi wakiwa wameungana.


MAISHA BINAFSI.


Carson amepokea tuzo mbalimbali katika miaka mbalimbali, kama vile, Shahada za heshima za Udaktari 40, pia ni mwanachama katika chama cha American Academy of Achievement, Horatio Alger Association of Distinguished Americans, Alpha Omega Alpha Honor Medical Society Ushirikiano wa yele, (Bodi ya wakurugenzi wa Chuo kikuu cha Yale) na mashirika mengine mengi. Pia ni mwanzilishi na mkurugenzi wa The Carson Scholar Fund, ambayo huwasaidia wanafunzi kutoka katika historia tofauti tofauti walio na vipaji maalumu katika masomo.


Mwaka 2007, Carson alijumuishwa katika Chuo kikuu cha Indiana Wesley, katika Society of World Changes na kupokea nishani ya heshima ya udaktari alipokuwa akiongea katika Chuo hicho. Aliporudi, alirudi na rafiki yake alyeitwa Tony Dungy ambaye naye alikujuishwa katika jamii. Tarehe 19 mwezi wa 9 mwaka 2008, Carson alopokea nishani ya raisi ya uhuru kutoka kwa Raisi George W. Bush


UTAALAMU NA MAGONJWA.


Carson ameandika vitabu vitatu vilivoongoza katika mauzo na vilivyochapishwa na Zondervan shirika la kimataifa la uchapaji la kikristo, Vinavoitwa : Gifted Hands (Mikono Yenye Vipawa: Hadithi Ya Ben Carson) , The Big Picture, na Think Big Kitabu cha kwanza cha Historia ya maisha ya mtu, na vitabu vingine viwili ni kuhusu filosofia ya maisha yake hususani katika mafanikio yake yanayoenda sambamba na imani yake kwa Mungu.Carson ni Mkristu katika dhehebu la sabato.

Mwaka 2002, Carson aliamuriwa kusitisha kuonekana katika maeneo yenye umati wa watu, baada ya kupata matatizo ya kiafya ya kwake mwenyewe. Mwezi wa sita alikutwa na dalili za kuwa na Saratani ya Kibofu cha mkojo, lakini kwa bahati nzuri, saratani hiyo ikiliweza kukutwa katika muda muafaka.

Lakini pamoja na hayo, Carson alibadilisha mfumo wake wa maisha, Bado anafanya upasuaji kwa zaidi ya watoto mia tatu (300) kwa mwaka lakini amekuwa akijaribu kupunguza muda wake.Carson amekuwa akifanya kazi kuanzia saa 7:00 asubuhi na kumaliza saa 8:00 usiku, lakini tangu agundulike kuwa na saratani amekuwa akifanya kazi na kuondoka saa 6:15, jioni. Hii inampa muda zaidi wa kukaa na mke na watoto wake watatu (3).

Makala ya video kuhusu maisha ya Carson inayoitwa Gifted Hands: Kitabu kinachohusu, hadithi ya Ben Carson kilitolewa na Zondervan mwaka 1992, hali iliyopelekea mwaka 2009, filamu ya Televishen iliyotolewa ikiwa na Jina hilo hilo, katika TNT tarehe 07/02/2009, na kushinda tuzo ya Academi ya Gooding jr ikiongozwa na Kimberly Elise akimwelezea mama yake.

10 comments:

Fadhy Mtanga said...

Leo umenisuuza sana moyo wangu kwani mie ni shabiki mkubwa sana wa Ben Carson.

Yasinta Ngonyani said...

Hii tukumbuke wote kuwa mwanzo ni mgumu. Lakini kuna watu ambao hawataki kuanzia mwanzo wanataka mafanikio yaje tu. Habari kama hizi watu wote wangekuwa wanazisoma nadhani wengi wangepata moyo. Na akina mama wengi wangemwiga mama Carson kwa kumtia moyo kijana wake nadhani wengi leo wangekuwa na mafanikio mmazuri tu. Dr Carson hizo tunu ulizotunikiwa unastahili. kazi njema na twakitakia afya yako iwe nzuri kwani bado tunakuhitaji. Na Koero nawe twakusukuru kwa kuiweka habari hii hapa katika kibaraza hiki cha VUKANI.

Malkiory Matiya said...

Benjamin Carson ni role model na mwalimu mzuri kwa malezi sahihi ya watoto wetu.

TUPENDANE said...

One of the most inspiring lives of all time...

Markus Mpangala said...

mama mchungaji uliwaza nini leo?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????? au ulikunwa CCM(Chai, Chapati, Maharage)?

mimi hapo kwenye BIG PICTURE na THINK BIG baaaaaaaaaaaaaaaaaaaaassssssssssssssssssssssssssssiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

leo ingelikuwa upo ndani ya ndoa na mtangaza NIA hakika angeaambiwa umemlisha limbwata maana viungo na vikorombwezo tamu tamu tamu kama sukari mweeeee

Mzee wa Changamoto said...

Ben Carson.
Niliwahi andika kumhusu na bado nasema "Ni mbegu ndogo iletayo mazao makubwa"
Mama asiyejua kusoma akawekeza kwa watoto ambao wamekuwa msaada kwa dunia.

emu-three said...

Hawo ndio wale tunawaita `waishiyo milele'. Waishio milele ni wale watu wakiwa hai dunianii walihakikisha wanafanya mambo makubwa, ambayo hata uhai wao unapokatika, yale mambo yao yanaendelea kutumika, na kukumbukwa.
Nimeipenda hii, Ahsante sana kwa kutuletea kitu kama hiki, ambacho kinatupa changamoto kuwa `kweli hakuna mtoto mpumbavu, na kweli hakuna mtu mjinga'

Bwaya said...

Alichonifunza cha kwanza: Kumbe kila mtu anaweza kuwa chochote akitaka! Na wazazi wanaweza kumfanya akataka! Mtoto yeyote anaweza kuongozwa kuwa mtu wa kuibadili dunia kwa mema na mabaya kutegemeana na aina ya malezi alimokulia. Malezi hamua mwelekeo wa mtoto! Majambazi. Vibaka. Madaktari. Walimu. Walaghai. Mafisadi...kumbe wote wanaweza kutupa picha ya malezi ya jamii yetu!

Nimependa uchambuzi wako dada Koero. Ubarikiwe sana!

Msangi said...

Sina cha kusema kuhusu Dr. Carson...zaidi ya kumtaka yeyote ambaye hajawahi kuzijua kazi zake, azitafute kwa haraka sana

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___