Thursday, September 23, 2010

JE NI SAHIHI KIJANA KUTAFUTIWA MWENZA NA WAZAZI ANAPOFIKIA UMRI WA KUOA AU KUOLEWA?

Mwenzenu jana nilikuwa na mjadala hapa nyumbani, na mada kuu ilikuwa ni juu ya namna nzuri ya kupata mwenza.

Dada yangu mkubwa ndiye aliyeanzisha huo mjadala kwa kumuuliza mama kama ni vyema mtu kutafutiwa mke au mume wa kuoa au kuolewa, au kila mtu anawajibika kujitafutia mwenyewe mwenza wake na kuanza maisha?

Mama alikuwa na haya ya kusema. Alisema kuwa kimsingi hapo zamani wazazi walikuwa wakiwatafutia watoto wao wenza wa kuoa au kuoelwa na lengo kuu lilikuwa ni kutaka mtoto wao aangukie katika mikono salama na mojawapo ya vigezo vikuu vilivyokuwa vikiangaliwa ilikuwa ni historia ya ukoo husika, kwa mfano, je ukoo huo unaanguka kifafa? Je ni ukoo wa wachapa kazi kwa maana ya kujituma kwa kufanya kzi kwa bidii ( Ikumbukwe kuwa zamani kazi kuu ilikuwa ni kilimo). Je Sio ukoo wenye mkono mrefu, yaani sio wezi ( Sijui kwa nyakati hizi kuna haja pia ya kuwajumuisha na mafisadi yaani kama ukoo una hulka ya ufisadi)

Jambo lingine lilikuwa ni kuangalia kama ukoo unashambauliwa na magonjwa sugu, kama vile anemia (Upungufu wa damu wa mara kwa mara) Kansa, kisukari na maradhi mengine yaliyokuwa yakitafsiriwa kuwa yanaweza kuushambulia ukoo.

Sina hakika kama vigezo hivyo bado vinazingatiwa kwani kule vijijini bado utaratibu a kutafutiana wenza upo lakini sio kwa kiwangom kama cha zamani kwa sababu ya mabadiliko yaliyoikumba jamii, kwani kila mtu sasa na lwake.

Kulizuka hoja mbalimbali ambazo kama nikiziweka hapa nitawachosha, na lengo langu ni kutaka kuwashirikisha wasomaji wa kibaraza hiki kisichoisha visa na mikasa kutafakari kwa p

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa zamani ilikuwa ni lazima waziza wanahakikisha wanaifahamu hiyo familia kama ulivyosema kwani nami nimewahi kusikia simulizi hiyo. Lakini kitu ambacho mimi nashangaa kwanini wazazi wamtafutie binti/kijana wao mchumba na wakati sio wo watakuwa na huyo binti/kijana muda wote. Ni binti niye atayeolewa au ni kijana ndiye atakayeoa na kuishi pamoja. kama ni taabu au raha sio wao wataipata. Hapo ndipo ninapotatanishwa na hili swala. Lakini pia naweza kukubaliana nao kuwa katika maisha yaa zamani na yetu waafrika tuliishi/tunaisha kwa ppamoja sana kwa hiyo labda kama sina unga naweza kwenda kwa mama mkwe na kupata ugali....ngoja niache hapa na wengine wapate nafasi...

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

inategemea...unaweza kutafutiwa akawa kime ama ukatafuta mwenyewe akawa kimeo!!!!

inahitajika umakini na kumtegemea muumba wako!

emu-three said...

Wazee wtu walikuwa wanaona mbali, walikuwa na elimu ya hekima. Elimu hii nii ujazo wa kila kitu. Sasa hivi elimu kubwa ni ya darasani, kukariri marejeo? Sio mbaya, ila ilitakiwa elimu hiyo ijazwe hekima.
Sio lazima kila rejeo lifae kila mahali, hapo unatumia hekima kutafiti.
Sasa wazee wetu walijua hili ndio maana kila kitu walidadisi undani wake, ya kuwa mke bora au mume bora hutokea kwenye shina bora. Kwa minajili hiyo magonjwa ya kurithi yaliepukika, tabia za kurithi zilikuwa haba, na hatimaye hata umri ulikuwa mrefu, kwasababu vipunguzi vya umri vilikuwa vichache!
Leo hii tunachoangalia ni `mvuto' mkikutana na `ashiki' ikachukua mkondo wake, basi ni mapenzi yanatajwa...tumependana...je wamjua, hapana, tutajuana mbele kwa mbele..baada ya ndoa unagundua makubwa ambayo huwezi kuyabeba...ndoa inakuwa ndoana!
Ni mjadala mzuri huu

Albert Kissima said...

Wazazi hawapaswi kumchagulia mtoto wao mchumba. Hali ya sasa na ya zamani, ilikuwa ni tofauti kabisa. Kwa nijuavyo mimi, zamani akina kaka walikua wakitambua kuwa watatafutiwa wenza, na wanawake vile vile. Jamii ya sasa haijakuzwa kwa mtizamo huu na hata wazazi wanalea wakijua kuwa hawana haki ya kufanya hivi, tofauti sana na wazazi/walezi wa enzi hizo.
Wazazi kujihusisha na kumtafutia mtoto wao mwenza, kunaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha malumbano, migogoro, kukosekana kwa amani ktk familia n.k. Binafsi naona hasara ni nyingi kuliko faida.
Hebu fikiria, wazazi walikuchagulia mchumba, wewe ukamkataa, na ukamuoa/olewa na mtu uliyemchagua wewe, punde mambo yakawa mabaya, vurugu, ngumi, mateke kila uchao. Wazazi kama si waelewa, ni dhahiri watakukatisha tamaa na watakuona uliyekaidi na sasa Idi imefika, wanakutazama unavyofaidi. Vile vile unaweza kumpata mpenzi mzuri, maisha yakanyooka, ya furaha, upendo na amani tele, lkn wazazi wasio waelewa wakaandaa mabomu ya kupoteza amani, upendo na furaha ndani ya ndoa ili kutaka kuleta ukuu wa mawazo yao ya kukutafutia mchumba na ukamkataa.

Niliyoyasema hapo juu si kitu lakini kikubwa hapa ni kuwa,
'wazazi wa leo wajibu wao mkubwa ni kuwafundisha watoto wao mbinu sahihi za namna ya kuwapata wenza,njia sahihi, yapi ya kuzingatia na kwa kuzingatia hekima ya wazazi(wazazi wana hekima sana), basi wanaweza kutoa pendekezo na maamuzi ya mwisho yabaki kwa mtoto'
Ni mawazo yangu tu ambayo naamini yanaweza kuanzisha mawazo mengine pia, kwa hiyo, bila kujali usahihi wake, mawazo haya bado ni muhimu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kama lengo lilikuwa ni kudumisha ndoa, siku hizi sio lazima ndoa idumu kwani kuna za mkataba nk

mwenye muwasho ndiyo anayejua kijiti cha kumkuna akaridhika na sio jirani

MARKUS MPANGALA said...

Mantiki ya Kamala imekaa vizuri, lakini zaidi ya kufikirio tunaweza kujiuliza ndoa ni kitu gani? ni kwanini watu hufunga ndoa? au labda ni kwanini tunafikiri kuwa na wenza maishani? samahani kwa mantiki yangu pinda.

Yasinta Ngonyani said...

Koero upoooo?? salama huko ulipo??