Thursday, March 17, 2011

ETI NI MIPANGO YA MUNGU!?

Hivi ni mipango ya Mungu au ni kujitakia?

13 comments:

Mija Shija Sayi said...

Mimi naona kweli ni mipango ya Mungu. Ni mipango ya Mungu watu kufanya kazi ili tule, na hapo kwenye baiskeli naona ni kazi inaendelea...

SunTura said...

hello Africa

Yasinta Ngonyani said...

Kila kitu hapa duniani ni mipango ya Mungu...

Anonymous said...

Da Mija na Da Yasinta, Kwa hiyo hata Sunami kule Japana ni mipango ya Mungu?

Naomba msome mtazamo wa Da mdogo Koero kwa jicho la tatu.....

Mija Shija Sayi said...

@Anony, Bahati mbaya jambo hili ni la kimtizamo hivyo halina jibu moja kama hesabu zinavyokuwa.

Binafsi nadhani naelewa alikokuwa anaelekea ila hajatoa maelezo yakutosha kitu kinachofanya hoja yake kuwa huru sana. Nimemjibu hivyo makusudi ili wakati mwingine anapoandika suala la kimtazamo akumbuke kuwa specific.

Kuhusu Sunami pale Japani nalo ni suala la kimtazamo, unaweza ukapata majibu mengi sana wengine wakisema Ni mpango wa Mungu na wengine wakikataa.

Cha muhimu katika kuandika masuala ya kimtazamo ni kuwa specific.

nyahbingi worrior. said...

kumbukeni,walisema hakuna kitu kipya chini ya juwa,vyote hivi vilishatabiriwa.

kila mmoja wetu na riziki yake.

Mungu ndiye anayepanga,Mungu ndiye chanzo cha JAPAN,KATRINA,SUNAMI NK.

hata babu wa loliondo ni Mungu.

Anonymous said...

Da Mija, Sidhani kama uko sahihi, ukisema awe specific una maana gani? kumbuka kuwa Koe ameuliza swali, na alikuwa anatafuta jibu....

Hebu naomba tuwaze kwa pamoja, Je hivi ni halali kweli kumhusisha mungu na ulitima wetu? au hali zetu? au hata haya majanga yanayotukabili?

Kumbuka kuwa Mungu aliwahi kuonya kwa kusema kwamba watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa, Je ni maarifa gani hayo?

Kwa nini tunakuwa ni wepesi wa kumtupia Mungu mizigo ambayo imetokana na udhaifu wetu?

Mija nimekusaidia kutafakari, Je hujagundua swali lilijificha kwenye swali la Da Koe?

Kaka Dimoso

Anonymous said...

Samahani nimekosea hapo juu, nilitaka kusema,
"Mija nimekusaidia kutafakari, Je hujagundua SIRI iliyojificha kwenye swali la Da Koe?"

Kaka Dimoso

Mija Shija Sayi said...

Kaka Dimoso, kwa jinsi ninavyousoma huo ujumbe sioni kama analalamika...au mwenzangu unaupokeaje ujumbe huo?

Anonymous said...

Dada Mijaaaaaa.... Sijasema analalamika, bali nimesema kuna SIRI imejificha ndani ya swali lake.......umeelewa sasa....
Tafakari

Mija Shija Sayi said...

Dah..kwa kweli ngoja nisubiri na wengine maana mimi mtazamo wangu hauko huko kabisaaa...

Yasinta Ngonyani said...

Jamani hii inategema inawezekana hayo ni maandishi tu au pia ni kwamba anamaanisha kuwa Mungi alipenda iwe hivyo. Kuhusu Sunami ya japani sizani ni mipango ya Mungu kwani ile ingeweza kutokea nchi yoyote ile. Siri? mmmhh

Mija Shija Sayi said...

Ngoja ninukuu...
"Hivi ni mipango ya Mungu au ni kujitakia?" Mwisho wa kunukuu..

Kaka Dimoso nikiangalia kwa jicho la tatu uandishi huu niliounukuu umeegemea sana kulalamika na sio Kisiri kama unavyodai.. Hebu tazama kichwa cha habari kilivyokaa..kinaonyesha kabisa jinsi Da Koero alivyopigwa na mshangao wa ujumbe anaousoma katika baiskeli..