Friday, January 2, 2009

JE WANASAYANSI HAWA WALIKUWA NI VICHAA!!!?

Kila mmoja wetu amewahi kusikia kuhusu wanasayansi wakubwa walioonekana kama vichaa au Maprofesa waliokuwa kama wana upungufu wa akili.

Kwa mfano
Albert Einstein ni mwanasayansi alieweza kuelezea kwa undani kuhusu uwiano mwingi wa masuala ya sayansi. Yeye alifurahia sana kuwa na nyumba ndogo.
Hiyo nyumba yake ndogo alikuwa ni binamu yake na aliishi nae kwa takribani miaka mitano kabla hajamuacha mkewe wa ndoa ambaye alizaa nae watoto kadhaa kabla ya kufunga nae ndoa, na kuioa hiyo nyumba ndogo.

Charles Darwin huyu ningependa kumuita mzee wa utata, huyu nae ni mwanasayansi aliyezungumzia kuhusu mabadiliko ya viumbe (Evolution). Alikuwa akiishi peke yake kwa muda mrefu bila ya kuoa kwa sababu alikuwa akijiuliza faida ya kuoa na kuishi bila kuoa kabisa.
Mwansayansi huyu nae alikuwa na vituko vingi, kwani kuna wakati alisema, “ Kwa kiasi fulani mke ni bora kuliko mbwa, lakini ni kupoteza muda wako tu kuwa nae”
Hata hivyo alikuja kuoa baada ya kuwa na uhusianao wa muda mrefu na mwanmke huyo aliyemuoa.

Sigmund Freud, Huyu ameweza kueleza vizuri kuhusu saikolojia na ufahamu, kwa ujumla alikuwa ni mtu mzuri, lakini alikuwa na mzozo na rafiki yake, kutokana na tabia zake za kushindwa kudhibiti hisia zake za kutojitosha, na hivyo kutaka kuabudiwa na kunyeyekewa.

Isaac Newton ambaye aliweza kukokotoa na kutoa kanuni za mwendo zijulikanazo kama Newton laws of motion, na kanuni ya nguvu za mvutano za dunia, alilelewa na bibi yake, baada ya baba yake kufariki na mama yake kuolewa na mwanamume mwingine, ambaye Newton hakumpenda kabisa. Newton alikuwa na tabia ya kupenda ugomvi na mizozo isiyo na umuhimu na wanachuo wenzake na hata marafiki zake, pia alishawahi kulelewa kwenye vituo vyenye kutoa ushauri nasaha.
Kumbuka hapa namzungumzia mtu ambaye ugunduzi wake kwenye Fizikia haujavunjwa hadi leo.

Marie Curie ambaye aligundua Radioactivity, aliishi na mume wake kwenye nyumba iliyokuwa na vitu vichache na vilivyozagaa kwa sababu alichukia sana kazi za ndani, sijui wakati huo kulikuwa hakuna watumishi wa ndani (House Girls)?
Wakati wakifanya shughuli zao za uchunguzi kuhusu radioactivity walikuwa wakiishi katika kibanda chao kilichokuwa na matundu, kiasi ambacho hata mvua ikinyesha maji yaliweza kuingia ndani.
Hawakuwa na fedha nyingi na mara nyingi walitumia fedha kidogo walizonazo kununua kahawa na kunywa kwa furaha, huku wakiota katika jiko lao la stovu. Marie Curie nae alijishindia tunzo mbili za Nobeli.

Paul Erdos mmoja wa wanahisabati katika karne ya 20, ambaye amesaidia sana katika kutengeneza Kompyuta, huyu naye hakuwa ametulia sana.
Hakuishi maisha ya kifahari, karibu maisha yake yote yalikuwa ya kifukara, kwani alitegemea misaada ya chakula na nguo kutoka kwa marafiki wema.
Hakupenda kujilimbikizia mali ingawa angeweza kama angetaka.

Je sasa umeweza kushawishika kwamba watu wenye vipaji maalum (Geniuses), huenda ni watu ambao kwenye upande wa pili wa maisha yaani katika kujenga maisha yao, hawana uwezo?
Lakini Je sio kwamba watu wanapokuwa na uwezo mkubwa kiakili hatimae mambo mengine kama vile fedha na ufahari vinakosa maana kwao? Nadhani hili ndilo la msingi.

Lakini cha ajabu ni kwamba, wanaofaidi ni wale waliokaririshwa nadharia za wanasayansi hawa.

Nadhani hii ni changamoto kwa kaka
Bwaya na kaka Kaluse, je walikuwa wanayafahamu haya?

Mimi sio mwanasayansi ngoja niwaachie wenyewe, wanaofahamu mambo haya.

6 comments:

Unknown said...

Hii ni chngamoto nyingine.
Kusema ukweli haya mini nilikuwa siyafahamu, ndio kwanza nayasikia kutoka kwako.
Hongera dada kwa utafiti wako.


Nitarudi baadae kutoa maoni yangu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

usihukumu na wala usijiulize juu ya ukichaa wa watu. ni vigumu kujua nani kichaa. hata wewe kuna wakushangaao.

mfano; mwalimu wa primary alivua nguo na kuanza kuoga mtoni. wakati amejipaka sabuni, akaona mtu akivuta suruali yake, yule mwalimu akadhania ni utani, akaendelea kuoga. kumbe nguo hizo zilivutwa na kichaa mmoja hivi. baada ya muda yule mwalimu akakumbuka kuwa siku ile ndio alilipwa mshahala na ulikuwa kwenye mfuko wa suruali. akakurupuka na kummfukuza yule kichaa aliyevaa nguo zake. kichaa akakimbia akielekea madukkani (eneo lenye watu wengi). walipofiika mbele za watu, watu wakakimbilia kumuokoa mtu asidhuliwe na kichaa. sasa je, kichaa alikuwa ni nani? aliyrvalia nguo hata kama sio zake na labda haimenei vizuri? au alilyekuwa uchi na amejaa mapofu ya sabuni?

Mzee wa Changamoto said...

Asante Koero. Naamini kila mtu ana kitu ambacho anakithamini na ambacho hupunguza saaaana nafasi ya vitu vingine. Ndio maana wakasema anything too much is harmfull. Kwa hiyo kujikita zaidi katika masuala fulani hukufanya ujisahau kwingine maana vitu vyenyewe vyakinzana. Ukichunguza saaana (kwa jicho la "kidunia") wale waliojikita na kupitiliza kwenye dini nao utawaona kama vichaa, ukiangalia waliojikita na kupitiliza saana kwenye "dunia" (kwa jicho la "kiimani") utawaona wendawazimu na vichaa. Ni kwa kuwa vitu haviendani na wakati mwingine hukinzana na ndio maana ukijikita zaidi kwenye hiki, yule wa mtazamo mwingine anakuona mwendawazimu. Kwa hiyo hapa linakuja suala la nini unataka kufanya na nini unapenda kufanya. Huwa haijalishi watu wakikuona vingine kama wewe unafanya kile upendacho, umuducho na uthaminicho. Si unaona hata wake na waume. Wakati wewe unamshukuru Mungu kwa mke / mume uliyenaye, wengine wanamuomba akufungue macho maana hata hawajui ulipofuka lini kuwa na huyo uliyenaye. Na wakati mwingine wakati unatafuta sababu ya kuachana na mwenza wako, wapo ambao wanaombea itokee leo watimize ndoto za kuwa na mwenza bora zaidi ulimwenguni.
Kwa hiyo hapa ninalotaka kusema ni kuwa ukichaa na ama uwendawazimu wa mtu watokana na namna unavyomuangalia. Na ili hii isikuathiri, basi mara zote fuata mapenzi yako, fanya upendacho, umuducho na kile uaminicho kama ndoto yako ili hata kama wengine wakikuona kama kichaa, mjinga, unayepoteza muda ama mwendawazimu, wewe kwako iwe sawa maana ndicho upendacho. Si unakumbuka walivyosema kuwa sisi ni wajinga tuna-blog? Mimi naona wao "hawajui na hawajui kuwa hawajui" maana hapa ninajifunza mengi na nasaidiwa kukua maishani.
Mara zote TATIZO NI NAMNA TULIONAVYO

MARKUS MPANGALA said...

Duuh ngoja kwanza! mimi huwa napingana na wale wasionipatia hoja za kunishawishi niamini kuwa shambulizi la mwaka 2001 mwezi septemba tarehe ile 11 lilifanywa na magaidi. Naitwa kichaa siyo uwongo. kuna watu nawabishia kwa hoja nataka hoja kwani niliyonayo nayaamini sababu yanaulizika vema. Lakini dada Koero naitwa kichaa mwenzako kwani nadai kubadilisha kitu ambacho eti hakibadiliki.

Mimi nasema ikiwa magaidi walikuwa ndiyo waliolipua pale basi tujibuni hoja zetu ambazo mashuhuda na tunaofanya utafiti hatukubaliani nazo. Mwenzenu naitwa kichaa hakika hivi. Nakumbuka hata dada Yasinta alisema nitachanganyikiwa.

Kitabu cha POPULAR MECHANICS(PM) kimeandikwa na mhandisi wa NIST( National Institute of Standard & Technology} ya marekani aitwaye Sivary Shyam Sunder.
Huyu anatoa ushuhuda kwamba siyo ndege tu iliyofanikiwa kutungua majengo yale, anatoa viashiria vingi hasa jengo namba 7 ambalo lilianguka saa 6 baada ya mengine kuanguka.
Anaelezea kwa njia za kisayansi ambao inakubalika na NIST wenyewe, lakini dunia ipo ziiiiii eti magaidi tu walifanya mambo yale. kuna maswali 114 ambayo hayajajibiwa hadi leo iwe NIST au tume ya uchunguzi au CIA,FBI.

Kwanini nasema hivyo, ni udadisi, kutaka kujua na kujisumbua kujua lakini inawezekana kujisumbua kujua wengine hawataki kusumbuliwa kujua wanaona UKICHAA. lakini inawezekana ikawa UKICHAA lakini hata sijui nisemeje. Topiki ya sayansi imenishinda aiseeh duu!kwaheri

Fadhy Mtanga said...

Duniani kuna watu, 'sipatwe na mshangao,
Usidhani ni mafyatu, tu wamezidiwa wao,
Unawashangaa?

Geneous mara tatu, wamejaaliwa wao,
Hawashindwi nacho kitu, kwenye taaluma zao,
Unawashangaa?

Lakini dunia yetu, hushangazwa sana nao,
Matendo yao si yetu, hatufanyi kama wao,
Unawashangaa?

Zikizidi ni ufyatu, akili za vichwa vyao,
Tena huwaghasi watu, ama hujitenga nao,
Usiwashangae!

Koero Mkundi said...

Huwa napenda sana changamoto, maana ndizo zinazonifanya nikue kiakili na kifikra.

Kabla ya kuandika makala ya kuweka hapa najiuliza, Je wasomaji na wanblog wenzangu wanatarajia kitu gani kutoka kwangu?

Nimegundua kwamba mijadala iliyofanyiwa utafiti na yenye utata inaleta changamoto sana, na ndio sababu natulia na kutafakari kwa kina kabla sijaweka makala yoyote hapa.

bado nahitaji changamoto zenu.
Ili na mimi nikue kifikra.