Thursday, January 1, 2009

MAKALA YA DINI: NAOMBA KUFUNGA MJADALA

Ndugu wanablog wenzangu pamoja na wasomaji wa blog hii, nasikitika kuwajulisha kwamba hii makala ya dini niliyoiweka hapa hivi karibuni imechafua hali ya hewa katika familia yangu.

Hivyo nimeambiwa nichague jambo moja, aidha nifunge hii blog au nisiendelee na huu mjadala.

Kwa kuwa sipendi kuwaudhi wazazi wangu nimechagua kuachana na huu mjadala ili kuinusuru hii blog.

Mimi bado ni binti mdogo sana, na bado nawategemea wazazi wangu kwa hiyo siyo busara kutofautiana nao katika umri huu.

Ningependa kuchukuwa nafasi hii kuwashukuru wanablog wenzangu waliochangia mada hii, kaka Evarist, Kaka Bwaya, kaka Fadhy Mtanga aliyeomba nimpe muda ili atafakari (Huyu naona aliiogopa hii mada). Wengine ni kaka Kamala, na kaka Mtwiba.
Nasema ahsanteni sana kwa michango yenu.

Sasa naomba mniruhusu kufunga huu mjadala.

Nawatakia heri ya mwaka mpya.

Ahsanteni sana.

8 comments:

Evarist Chahali said...

Pole sana dada yangu.Yaliyokusibu ni sehemu ya milima na mabonde katika safari hii muhimu ya kublogu.Nachoweza kukufariji ni hiki:action ikisababisha reaction,then inamaanisha ilikuwa na substance.Mara nyingi vitu visivyo muhimu huwa havisababishi reaction,lakini vilivyo muhimu hugusa hisia za watu ambapo baadhi yao hushindwa kujizuia ku-react kwa namna moja au nyingine.Natumai utazidi kuja na mada "za kichokozi" (i.e. zenye kuhangaisha ubongo kwa tafakuri) na hopefully wazazi na wenye mamlaka wengine wataelewa umuhimu wa kukuachia utumie vizuri uhuru wako wa kujieleza,kusaka majibu,kukosoa,kusherehesha,nk.

Pole,na happy new year 2009.

Mzee wa Changamoto said...

Ninadhani ilikuwa mada yenye kuigusa jamii nzima. Lakini pia nakubaliana nawe kuwa hutaki kukorofishana na wazazi kwa hili. Kuna mengi ya kufanya, kuna mengi ya kuandika na kuna mengi ya kuisaidia jamii na kwa wewe kuachana na hili ili kutoa nafasi kwa mengine na kujenga mahusiano mema na wazazi ni busara. Nashukuru pia kuwa wazazi wamekuja na uchaguzi wa wewe kufanya. Yaonesha waeelimika na ni werevu kiasi gani. Washukuru kwa CHANGAMOTO HIYO na endelea kuwaombea na kuwatii.
Heri ya mwaka huko mliko, japo sisi twausubiri

MARKUS MPANGALA said...

Duuh! mbona nimekosa hondo? unajua nilikuwa na mambo ya hapa na pale, mra dada Yasinta kutua bongo kwahiyo sikutulia kwa kweli. kwa shingo upande nakubalia uamuzi wako dada Koero lakini nimesikitika wazazi kuleta songombingo kwani huu si ugomvi bali kujadiliana.

AYA ZA MOTO
nilianza kugomea kwenda kanisani mwaka 1996 nikiwa darasa la saba. Ninagoma na nitaendlea kugoma kwani siwezi kuikana nafsi yangu wakati ipo katika maumbile yangu, haina maana kuikana nafsi huku ukiamini roho ipo. Tuache. Dada Koero nafurahi sana mambo haya ya dini kwani mimi siamini kabisa kwamba kumuua mgunu lazima uwe na dini ndiyo maana naamini african tradtional religions. siziotaki hizi dini wanazokwiba kila kukicha. ni kweli nchi ya ahadi muangua aliamuru watu wafe ili waitwae ardhi yao? je huo ndiyo mwelekeo wetu binadamu. BAHATI mbaya dada Koero huwa naandika makala za uchambuzi, niliwahi kuhoji kama kuna tofauti katika DINI, UTAMDUNI NA IMANI. basi maadamu umefunga kwa hsingo upande nakubali lakini binafsi nimelelewa mazingira ya kikatoliki na wamisionari lakini licha ya kutaka kuwa padre, sikusita kuhoji, kuadadisi na kwanini yapo kama yalivyo. SITAKI KUSIKIA DINI HIZI ZA HUKO KWA MABABU WA MSHARIKI YA KATI.

Pole dada Koero ndiyo maisha

MARKUS MPANGALA said...

samahani ebu tukitafute kitabu cha PLACID TEMPEL kiitwacho BANTU PHILOSOPHY, dada Koero pale maktaba Mlimani kipo katika shelfu za Political science.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hapa ndipo lilipo tatizo la wazazi wetu. wanadhani wanatumiliki eti kwa sababu tumepitia wao kuja hapa duniani. na wanaendelea kudhani kwamba wanajua kilichochema kwetu kuliko sisi wenyewe tunavyojua chema chetu na kukiishi. wanataka tuwe wao na tusiwe sisi ili tuishi kama wanavyotaka na kuwafurahisha. ni tatizo kubwa linalotufanya tusiwe sisi bali tuwe wao.

angalia usijechaguliwa na mume wa kukuoa na kazi ya kufanya na kadhalika.

wengi wetu tumechaguliwa kla kitu. kuna kijana wa kijijini kwetu anakaribia kuwa padri kwa kulazimishwa na babake. wengi husoma yale tusiyoyapenda kuyafanya kisa baba au mama kataka na maisha yetu huishia kuwa ya matatizo makubwa yenye ugigili.

kuwa wewe. unaweza kufanya mambo yako kwa siri. kwa mfano. sio lazima utumie jina lako na icha yako. hakikisha unapata ukipendacho na sio wazazi wako wapendacho.

hili la wazazi wetu na kutaka mafanikio yao kupitia sisi nitalijadili kwa kina hapo mbeleni na mjadala huu ni muhimu kwetu.

waambie wazazi wako kwamba wewe ni binadamu kamili, umekamilika na unamtizamo wako, maisha yako na uyapendayo hata kama wao hawayapendi.

hawakumiliki bali wewe unaimiliki na umekamilika.

kumbuka hukuomba kuzaliwa na hukuwaomba wazazi fulani (ulionao) wakuzae. kuzaliwa kwako ni matokea ya vitendo vyao. tangu ukiwa mimba mpaka unazaliwa hawakujua kama utakuwa wewe ulivyo. ni lazima ujifunze kufanya mambo yako kama wewe bila kuingiliwa na ikiwezekana kwa kuficha jina lako.

hakuna laana duniani na usiziogope laana. haya yote nitayajadili kwa kina huko mbeleni.

Koero Mkundi said...

Kweli, kazi ipo!

Ningependa sana mjadala huu uendelee. lakini nadhani huu sio wakti muafaka.
Naomba mvute subira, wakti ukifika nitairejesha hii mada upya na huenda ikawa tamu kushinda sasa.

nawashukuru sana kaka Evarist, kaka Mubelwa Bandio aka mzee wa changamoto, na kaka Markus Mpangala kwa maoni yenu. Nasema ahsanteni sana.

Kamala Maoni yako nimeyasikia na nitayazingatia.
Naona mwenzangu umeiva kwa utambuzi.

Unknown said...

Sijui nilikuwa wapi hadi hii mada ikanipita hivi hivi.

Nilitaka kusema mengi lakini Kamala kasema karibu yote niliyotaka kusema.

Dada Koero, tunaishi kwa mazoea, tunaishi katika ulimwengu wa mfumo dume, ambapo watoto hasa wa kike hawana maamuzi mbele ya wazazi.
Mimi siwalaumu wazazi wako kwani wanatumia kile walicholishwa katika walezi yao tangu utotoni.

Wamekulia katika dini wamelelewa katika dini ambayo kwa mujibu wa makala yako nao walirithi kutoka kwa wazazi wao ambao ni babu na bibi yako ambao nao labda walirithi kwa mtiririko huo, yaani mlolongo ni mrefu, huwezi kujua huyo aliyelishwa hiyo dini au dhehebu aliaminishwa kiasi gani.
Kwa bahati mbaya wazazi hawataki tujiamulie, wanataka tuwe wao, tusali kama wao tuimbe kama wao, tucheze kama wao na tufikiri kama wao.

Hivi dini nini? Dini mpaka wapi?

Tumebaki kudanganyana tu, uongo waliorithishana miaka na miaka sasa tumeanza kuushitukia. Tunahitaji kina Koero wengi wenye mitizamo ya kuhoji hizi imani tulizolishwa utotoni, kwani tusipokuwa makini watoto wetu watakuja kutusuta.

Tunapoelekea dini zinaonekana kukosa mashiko na watoto wanaozaliwa siku hizi sio kama sisi tuliokubali kila kitu, hawa wanazaliwa wanakuta TV, Compyuta, Internet, Simu za mikononi ambazo nazo zina internet, wanatembea na taarifa viganjani, unafikiri utawadanganya? Watakucheka tu.

Pole sana, naomba uwe na subira labda hii mada huu sio wakati wake.

Nakutakia heri ya mwaka mpya.

Koero Mkundi said...

kaka Kaluse nimekusoam.
Ahsante kwa maoni yako.