Barua yangu ya wazi kwa dada yangu wa hiyari, Yasinta Ngonyani iliwachanganya wasomaji wengi hadi wengine walinitumia email ya kutaka ufafanuzi kwamba kulikoni tena mambo ya binafsi kuwekwa kibarazani?
Nilijua hilo litatokea na kweli limetokea, nimepokea email kadhaa zikinitaka nifafanue kile nilichoandika.
Kwanza naomba nichukue nafasi hii kumshukukuru dada Yasinta kwa kuniruhusu kuweka ile barua ya wazi katika kibaraza hiki nikidai kuwa namuandikia yeye. Naomba niweke wazi kwamba ile barua ilikuwa haimuhusu yeye na wala hakuwahi kuniandikia barua yoyote. Ile barua haikuwa ni ya kweli na wala haihusiani na mimi, ila kuna rafiki yangu mmoja niliyewahi kusoma naye ambaye aliwahi kuolewa mara tu baada ya kumaliza kidato cha 4.
Nakumbuka kila tulipokutana alikuwa akiniuliza kama nitaolewa lini. Siku moja aliniambia maisha ya ndoa ni mazuri na asiyeolewa labda ana matatizo kwa kuwa anakosa tamu ya ndoa. Nilimsikiliza na kumpuuza kwa kuwa nafahamu kuwa maisha ya ndoa hayana formula, yaani yanaweza kuwa mazuri kwa huyu na yakawa mabaya kwa yule. Hivi karibuni nimepata taarifa kuwa ndoa yake imeota mbawa na aliyempora mume ni nyumba ndogo na ndio nikajikuta nakaa na kuandika ule ujinga na kuuweka hapa.
Sikuwa namsimanga yule shoga yangu bali nilitaka kufikisha ujumbe kwa watu wenye mtizamo kama wake.

3 comments:
Ile ilikuwa ni sanaa nzuri ya uandishi. Ulitumia kipaji cha hali ya juu. Ulitushambulia vijeba ile mbaya. Lakini ulijitahidi kueleza ukweli kwa namna ya kimasikhara, lakini ujumbe uliokusudiwa umefika.
Ndiyo kublog huko. Hupaswi kulaumiwa ama kushutumiwa, kublog ni zaidi ya uhuru wa kueleza unachojisikia.
Pamoja sana.
sawasawa kaka Fadhy.......
lakini nilisema SIYO KILA NDIYO INA NDIYO KIUNDANI....KUNA NDIYO ZINGINE HUAMBATANA NA UTANI.
MSOME KAKA KITURURU ndiyo utaelewa lakini samahani usielewe zaidi
Mhhh!
Post a Comment