Friday, December 4, 2009

MATEJA NA UTAMU WA TENDO LA KUJAMIIANA!


Mimi kwa kawaida ni mdadisi sana, na naomba nikiri kuwa udadisi wangu uliwahi kuniletea matatizo wakati fulani. nakumbuka nilikuwa naendesha gari katikati ya jiji, na wakati nimesimama kwenye taa za kuongozea magari,akaja mama mmoja ombaomba ambaye namkadiria kufikisha umri wa miaka 60 hivi.
Alionekana kuwa na afya njema tu. Alipofika pale nilipo aliniomba pesa, nilitoa kiasi cha fedha na kumpa, lakini nilimuuliza kwa upole kwamba kwa nini anaomba barabarani wakati afya yake ni nzuri tu. mama wee....alinishambulia kwa matusi na kama sio taa za barabarani kuniruhusu labda angenipasulia kioo cha gari langu, kwani nilimuona kupitia kioo cha pembeni akiokota kitu nadhani kwa ajili ya kunirushia, lakini alichelewa kwani nilishafika mbali. Tukio hilo lilinikumbusha tukio lililompata dada yangu Yasinta Ngonyani na mwendawazimu wa Ruhuwiko Songea.

Ngoja nirejee kwenye kile nilichotaka kusimulia leo. Nimesema kuwa mimi ni mdadisi sana, na udadisi wangu naona saa utaniletea matatizo, lakini sitaki kuacha na sijui ni kwanini. Juzi nikiwa kwenye Intenert Cafe moja iliyopo maeneo ya Mikocheni nilikutana na kaka mmoja ambaye ni mtumiaji wa madawa ya kulevya, maarufu kama Teja. Kijana huyo ambaye nilisoma naye shule moja akiwa amenitangulia darasa moja mbele, alikuwa akisifika sana kutokana na kuwa na akili sana darasani wenyewe tulikuwa tunaita akili za Nature, na mpaka tukawa tunamuita Nature kutokana na kuwa na akili ambazo sio za kawaida.

Alifanikiwa kufaulu na kuendela na masomo ya sekondari, nasikia alifaulu kidato cha nne na kuingia kidato cha tano na kupangiwa kwenda shule moja maarufu mkoani Tanga na huko ndipo alipojitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kuwa Teja kiasi cha kusababisha kufukuzwa shule na kurejea jijini na kuendela na tabia hiyo.

Nilipokutana naye pale cafe nilipiga naye stori mbili tatu na ndipo nikamuuliza swali, kwamba kwa nini amejiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya wakati alikuwa na maendeleo mazuri shuleni. Nilimuona akibadilika ghafla kama vile amekasirika, niliona mambo si shwari, ikabidi nimuwahi kumuomba radhi kwa swali langu la kijinga, lakini aliniambia kuwa hajakasirika, na kwa upole akaniuliza swali......

"Samahani Da' mdogo Koero, hivi unajua utamu wa tendo la kujamiiana?" Nilishangazwa la swali lile, lakini kwa kuwa niliyataka mwenyewe nikajikuta nikimjibu kuwa nafahamu. Kisha akaniuliza tena..... "Je Unajua utamu wa tendo la kujamiiana unadumu kwa muda gani katika ubongo wa binadamu?" Duh! hili lilikuwa ni swali gumu kwangu na nilijua sasa na mimi nimepatikana maana nilijifanya kuwa mdadisi, lakini sasa mambo yananigaeukia.

Nilijikakamua na kumjibu kwa kifupi. "Sijui maana sijawahi kufanya utafiti huo"
Yule kijana kwa upole akaniambia, "kwa kuwa umeuliza swali basi nitakujibu tena kwa ufasaha ili wakati mwingine usije ukauliza tena kwa mtu mwingine"

Aliniambia kuwa kwa mujibu wa tafiti mbalimbali imebainika kuwa utamu wa tendo la kujamiiana unadumu katika ubongo wa binadamu kwa sekunde tano tu, mtu anapofikia kileleni, lakini mtu anapotumia madawa ya kulevya, yaani pale anapojidunga dozi, ule utamu anaoupata ambao unafanana na utamu wa tendo la kujamiiana unadumu kwa dakika kumi na tano.
Kisha akaendelea kusema kuwa, kama utamu wa kujamiiana ambao hata hivyo unadumu kwa sekunde tano tu, lakini watu wanaupenda kupita kiasi huku wengine wakihatarisha maisha yao dhidi ya gonjwa la ukimwi na wengine wakitiana ngeu au hata kuuana kwa sababu ya utamu huo, kwa nini yeye asiamue kuwa Teja ambapo anaweza ku-enjoy kwa takribani dakika kumi na tano bila bughdha kwa kitu ambacho hakimpi usumbufu.

Wakati wote akinipa darasa hilo nilibaki nimemtumbulia macho kwa mshangao na nisiamini kile alichokuwa akinisimulia. Kusema kweli sikuwa na swali la nyongeza, nilimshukuru kwa majibu yake nikamuaga ili niondoke, lakini alinitaka nimuachie hela akapate kete yake ili apate stimu kwani nilimvurugia stimu yake kwa kumuuliza lile swali.

Sikutaka kugombana naye, nilitoa kiasi cha pesa na kumpa, kisha nikaondoka. Yaani kiranga kiliniisha, maana sikutegemea yale majibu ambayo yalikuwa na ushahidi wenye utafiti ambao hata sikujua kama utafiti ule una ukweli kiasi gani.

Hata hivyo kwa umbeya wangu nimeona niiweke hii habari hapa kibarazani ili nilete changamoto toka kwa wadau na wasomaji wa blog hii.

8 comments:

Candy1 said...

Mmh, sie ambao hatuko kwenye hayo "madawa ya kulevya", personally simuelewi ku-compare ngono (is this the right word?) na madawa ya kulevya kwa sababu ni vyema kuelewa endapo, wenzetu wanasema "stepping into someone's shoes"... kwahiyo kwa mimi ningemuelewa only if ningekua natumia hiyo kitu...which I am not...so I don't get him..

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli kama unataka kujua ni kuuliza tu nilidhani nipo peke yangu kumbe! Ila huo mlinganisho kwa kweli ni mgumu kumwelewa hasa kwa asiyetumia hivyo vyote na kujua ukweli.

Bennet said...

Nina jamaa zangu wengi tu ambao tumekulia wote mitaa ya Ilala ambao walikuwa na mafanikio ya maisha tena mapema sana na wengine walikuwa wanaelekea kwenye mafanikio, lakini waliingia kwenye ulevi wa madawa ya kulevya na sasa hivi wana hali mbaya kuanzia ya maisha mpaka kiafya
Wanajuta lakini imekuwa ngumu sana kwa kuacha

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwani ngono ni tamu, nzuri au????? ni tamu kama nini sukari? inalambwa? tusaidie kiswahili jamani

Mzee wa Changamoto said...
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto said...

Ntasema nijualo juu ya hili. Kuna ukweli juu ya "ridhiko" lipatokanalo katika NGONO na MADAWA YA KULEVYA. Kuna ukweli wa HISIA za ridhiko hilo. Zile za ngono (Orgasm) huchukua muda wa takribani sekunde 15 kwa wanawake na 20 kwa wanaume (kumbuka hii ni wastani) na waweza kusoma hapa (http://www.sarilocker.com/advice/qa.php?id=1267) na zile hisia za madawa ya kulevwa hukaa takribani mara tatu zaidi ya zile hisia za ngono. Nanukuu taarifa hii isemayo
"How long does the feeling last?

Not long.
Cocaine is both fast- and short-acting.
Intranasal use, or "snorting," takes effect within a few minutes, and lasts 60 to 90 minutes.

Injecting produces a "rush" that is felt within minutes, and lasts 20 to 60 minutes.

Smoking causes a high within seconds, which lasts only five to 10 minutes.

When the cocaine high fades, the person may begin to feel anxious and depressed, and have intense craving for more of the drug.
Some people stay high by "binging," or continually using the drug, for hours or days."

Haya unaweza kuyasoma katika http://www.camh.net/About_Addiction_Mental_Health/Drug_and_Addiction_Information/cocaine_dyk.html
Naamini itasaidia kujibu baadhi ya yale yasiyojulikana kwa wengi.
Blessings

Godwin Habib Meghji said...

Yaani hapa naona kama vile vinafananishwa vitu viwili tofauti kabisa. Hii ni sawa na USINGIZI NA KIFO. Yaani USINGIZI unalala masaa 8 mpaka 12. na KIFO unalala milele. STIMU YA NGONO NA STIMU YA MADAWA YA KULEVYA INA VIZIO TOFAUTI. KAMWE HUWEZI KULINGANISHA

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___