Wednesday, February 17, 2010

KAMPENI YA ZINDUKA MALARIA HAIKUBALIKI: MHESHIMIWA RAISI ALITAKIWA KUIDHINISHA MATUMIZI YA DAWA YA DDT

Mheshimiwa Rais akizuindua kampeni za Zinduka malaria haikubaliki pale viwanja vya Leaders club

Niliwahi kuandika wakati fulani juu ya janga la malaria linavyowamaliza Watanzania, katika makala hiyo niliyoipa kichwa cha habari kisemacho ‘shiranga la ugonjwa wa malaria: bora tufe kuliko kuathiri mazingira!’ nilieleza mengi juu ya kukwama kwa makusudi dhamira ya kuutokomeza ugonjwa huo, kama ungependa kujikumbuasha bofya hapa.

Hivi karibuni katika kampeni ya Zinduka Maleria haikubaliki iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alizungumzia jinsi malaria inavyowamaliza watanzania, wimbo ule ule ambao umekuwa ukiimbwa na wanasiasa kila uchao.

Naamini kila mtu anajua kuwa Malaria inaua wananchi wengi sana hapa nchini kuliko hata ugonjwa wa Ukimwi, lakini cha kushangaza mpaka leo hii hakuna hatua madhubuti ambayo imechukuliwa katika kuutokomeza ugonjwa huo.

Awali nilijua kuwa Raisi angetumia kampeni hizo kuidhinisha matumizi ya DDT, dawa ambayo imefaninkiwea kwa kiasi kikubwa kutokomeza ungonjwa wa malaria katika nchi ambazo zinatumia dawa hizo hususana Zanzibar.

Nilishangazwa na kauli ya Rais pale aliposema, naomba ninukuu, "Kila siku ya Mungu, hapa nchini, wanakufa watu hadi 291 kwa ugonjwa wa malaria. Kwa maneno mengine, kila saa inayopita, wanakufa watu zaidi ya 10 kwa ugonjwa wa malaria. Hawa ni watu wengi mno. Hivyo, malaria ni Janga la Taifa letu. Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba malaria ni ugonjwa unaoweza kuzuilika na kutibika. Ndiyo maana tumeamua kuwa wakati tunaendelea kushughulikia kutibu wagonjwa wa malaria, tuelekeze nguvu zetu katika kuzuia kwa kuanza juhudi za kutokomeza malaria nchini." Mwisho wa kunukuu,

Pia alibainisha njia kuu tatu za kupambana na kuushinda ugonjwa wa malaria, akisema kuwa njia ya kwanza ni kutumia dawa zenye nguvu na uwezo wa kutosha kuwatibia wale watakaokuwa wamepatwa na ugonjwa wa malaria.


Njia ya pili, alisema, ni kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa ya kuua mbu na akaelezea jitihada za Serikali yake juu ya kupatikana kwa vyandarua vya namna hiyo. Alisema kuwa mpaka sasa watoto wenye umri wa miaka mitano na kina mama waja wazito wanapewa vyandarua vya namna hiyo bure, lakini mipango inakamilika kuiwezesha kila kaya nchini kuwa na angalau vyandarua viwili vya namna hiyo.

Akasema kuwa njia ya tatu ni kuhakikisha kuwa mbu wanaobeba malaria hawazaliani na wanatokomezwa kabisa.
Kwa maneno yake mwenyeweRais Kikwete alisema, "Ni lazima tuhakikishe tunawamaliza mbu wanaoleta malaria kwenye mazalia yao. Tunaweza kabisa kuhahakisha kuwa sisi tunakuwa kizazi cha mwisho kufa kwa malaria. Nchi nyingine duniani zimeweza na naamini hata sisi tutaweza. Ndugu zetu wa Zanzibar wameweza na sisi wa Tanzania Bara tunaweza pia."

Mimi nilitarajia kuwa huo ndio ulikuwa ni wakati muafaka wa yeye kutangaza rasmi matumizi ya dawa ya kuulia wadudu ya DDT, ambayo ndiyo inayotumiaka Zanzibar pia katika kuutokomeza ugonjwa huo.

Huwezi kuyataja mafanikio yaliyofikiwa na Wazanzibari katika kuutokomeza ugonjwa wa Malari bila kuitaja dawa ya DDT.

Binafsi naona kampeni hiyo ilikuwa na sura ya kisiasa zaidi kuliko kile ambacho kilitarajiwa na wananchi wengi, kwani hakuna jipya, hizo njia kuu tatu alizozitaja mheshimiwa raisi zimekuwa zikitajwa kila siku na wanasiasa na wataalamu wetu wa afya lakini hazijazaa matunda mpala leo na watu wanaendelea kuteketea.

Cha Kushangaza Kiwanda cha A to Z cha hapa Arusha ambacho ndio mtengenezaji mkuu wa vyandarua ni miongoni mwa wadhamini wakuu waliodhamini uzinduzi wa kampeni hiyo ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria, hii haiingii akilini, kwamba mtu anayetengeneza pato lake kwa kutegemea ugonjwa wa malaria akubali eti malaria iishe hapa nchini, kama sio siasa ni kitu gani, basi atakuwa ni mwenda wazimu.

Mimi naamini kuwa mheshimiwa Raisi anayo dhamira hasa ya kuutokomeza ugonjwa huu wa malaria, lakini wataalamu wetu wameshindwa kumshauri raisi wetu kufanikisha dhamira yake hiyo.

Bado nasisitiza kuwa kamwe hatuwezi kuutokomeza ugonjwa wa malaria kama hatutaruhusu matumizi ya dawa ya kuulia wadudu ya DDT.

6 comments:

Anonymous said...

DDT ilishapigwa marufuku huko Bara, ni vema kwanza ukaelezea ni kwanini iliachwa kutumiwa.

Yasinta Ngonyani said...

kuhusu malaria ni hivi:- Tatizo ni kwamba inawezekana ya kwamba wamepewa vyandarua na hawajui matumizi yake hawajaonyeshwa jinsi ya kutumia. Ni sawa na kumpa mtu kondom bila kumwonyesha matumizi yake. Na kesho yake uukakuta amegandishia barafu. kwa hiyo hapa kinachokosekana ni ELIMU. kuhusu DDT ngoja nifanye utafiti kwanza.

Bennet said...

Afrika ya kusini wanatumia DDT kwa kupiga kwenye kuta za nyumba zao ili mbu akitua afe, napinga matumizi ya DDT kama itapigwa kwenye mazingira kwa sababu inamadhara makubwa sana kwa viumbe hai

Kwa upande wangu hata mimi ni mvivu kulalia chandarua labda nikiwa field kwa sababu mara nyingi huwa natumia mahema hapo ndio nalalia chandarua, kwa nyumbani huwa napulizia dawa ijulikanayo kama ICON kwenye kuta za nje ya nyumba ninayoishi na hii huzuia mbu kuingia ndani na tuna miaka hatujawahi kuumwa malaria

Mzee wa Changamoto said...

Siasa, Siasa, Siasa.
Hili swali la kwanini malaria itokomee Zanzibar na si Tanzania bara nilimuuliza Mhe Waziri Asha Abdallah wa Zanziba na alichosema waweza kumsikiliza mwenyewe hapa http://vimeo.com/7217741

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mh! usanii mtupu. Da Koero umesema vema kuwa hicho kiwanda hakiwezi kutengeneza vyandarua vyenye kupelekea malaria kuisha. sana sana ni kuwa atatengeneza vyenye dawa ya viwango vya chini ili twendelee kuumwa na mbu!

pengine suluhu ni hiyo umwagiaji wa dawa ktk kuta kama Kaka Bennet alivosema ambapo dola milioni 18 zimetengwa mwaka huu kwa ajili ya umwagiliaji wa dawa majumbani kwa mikoa yenye malaria nyingi ambayo ni Kagera, Mwanza, Mara Shinyanga na ile ya kusini (pengine).

MARKUS MPANGALA said...

Kilio chako kilishasikika tangu uniruhusu kuitumia makala ile iliyozungumzia DDT. kwa taarifa nilizonazo ni kwamba DDT imerudi mtaani na wizara ya afya imekusikiliza Koero, nadhani Rais alipitiwa tu