Sunday, February 7, 2010

WAALIMU WETU NA MAJINA YA KEJELI

Mwalimu akifundisha

Katika kusoma kwangu nimebahatika kusoma katika shule mbalimbali zikiwamo za hapa Jijini Dar na za mikoani.

Kusema kweli maisha ya shule ni kumbukumbu pekee ambayo kila mtu ambaye amebahatika kufuta ujinga anaweza kubaki nayo. Naam ni kipindi ambacho unakutana na watu kutoka katika mikoa mbalimbali na wenye tamaduni tofauti tofauti.

Nimegundua kuwa sekta ya ualimu ndiyo inayoongioza kwa waalimu kupewa majina ya utani na wanafunzi, na majina hayo yanaweza kuwa ni kutokana na tabia ya mwalimu, aina ya mavazi anayopenda kuvaa, kauli zake za mara kwa mara, matamshi na hata vituko anavyofanya, maana unaweza kukuta mwalimu ana vituko kama The Comedy.

Jana tulikuwa tunakumbushana mambo mbalimbali yaliyopita na dada zangu ambao walikuja kututembelea hapa nyumbani, na miogoni mwa kumbukumbu likajitokeza hilo la majina ya utani waliyokuwa wakiwapa waalimu wao.

Ilikuwa ni kumbukumbu nzuri ambazo ziliifanya siku yangu ya jana niione nzuri ajabu. Nami nimeona niwashirikishe wasomaji wa kibaraza hiki juu ya kumbukumbu hizi. Hata hivyo naamini kuwa miongoni mwa wasomaji wa kibaraza hiki wapo waalimu ambao nao huenda walikuwa au ni miongoni mwa watu ambao walikutana na kisirani hiki cha kupewa majina ya utani na wanafunzi.

Naamini sio vibaya kama nao wataweka changamoto zao walizowahi kukutana nazo au wanazokutana nazo katika taaluma zao hizo.

Binafsi nakumbuka kuna mwalimu tulikuwa tunamwita darubini, huyu alikuwa ana macho makali, kwa mfano unaweza kuwa kwenye chimbo (Chimbo ni eneo la kujificha) na kama akipita eneo hilo ukawahi kukimbia, utashangaa siku ya pili mkiwa kwenye gwaride akikuita kwa jina kuwa upite mbele, na hapo ni lazima upate bakora.

Kingine ni pale ambao umejificha mahali, halafu ukawa unachungulia kwenye kona ya ukuta, akiona jicho tu utashangaa akikuita kwa jina na hapo pia utachezea bakora, alikuwa na kipaji cha kukariri majina na sura za wanafunzi wake, huyu alikuwa ni mwalimu wa nidhamu na mara nyingi waalimu wa nidhamu ndio wanaokutana na adha hii ya kupewa majina ya ajabu.

Mwalimu mwingine tulikuwa tunamuita Pindipo. Huyu alipenda sana kutumia neno la ‘Pindipo utakapobainika’ pale ambapo anatahadharisha juu ya jambo fulani. Kama kawaida wanafunzi wakampachika jina la Pindipo.

Mwalimu mwingine ninayemkumbuka tulikuwa tunamwita ‘Kala nini’ huyu naye kama umefanya makosa na amekasirika sana, alikuwa akipenda kusema ‘binti reo utaniereza nimekura nini usiku wa jana’ huyu alikuwa anatokea kule kwa akina Chacha Wambura. Na ndipo wanafunzi wakamwita Mwalimu Kala nini.

Huko Sekondari napo nikakutana na vituko hivyo, kuna mwalimu wetu wa Biology tulikuwa tunamwita mwalimu Mandible, Mandible ni zile antenna za Panzi, sasa yeye alikuwa akipenda kulitamka hilo neno mpaka tukamwita hilo jina la mwalimu Mandible.

Mwalimu mwingine alikuwa ni mwalimu wa Kiswahili huyu tulimwita jina la Ngoswe, kama mnakumbuka kile kitabu cha Ngoswe, Penzi kitovu cha uzembe.

Mwalimu mwingine alikuwa akiitwa ‘However,’ huyu, hawezi kusema maneno matatu ya kiingereza bila kutamka hili neno la However, na hapo wanafunzi wakampa jina la However.

Kwa kweli ni majina mengi mno na kama nikisema niyataje hapa, basi nitawachosha, ngoja niwaachie na wasomaji wengine watoe kumbukumbu zao.

12 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Duh Koero nawe uminikumbuka sana wakati nikisoma sekondari huko Uchagani kulikuwa na walimu dizaini sana!

Kuna huyo 'Darubini' wenu yeye hakuangalia macho. huyu alikuwa anaangalia KISOGO ukimkimbia tu hata ukikaa mwezi atakupata tu kwa kuwa anadai visogo havifanani :-) Pamoja na hili huyu naye alikuwa na sifa ya kubainisha mambo...wakati fulani msichana alikamatwa na Mzee wa Fyongo wakila malavedave na walipopelekwa staff room mvulana akaambiwa 'shehe twambie...hata kama uliweka kichwa tu lakini si umet....?' What an embarrassment!!!

mwingine tulimuita Mzee wa Fyongo! Nakumbuka wakati fulani waziri wa elimu alikuja na akapewa kazi ya kusoma risala na akaanza historia ya shule 'ndugu waziri.....shule yetu ina wanafunzi shilingi 840!....oh! sorry ndugu waziri ni wanafunzi 840!!'

Huyu ndo aliwabamba wale walokamatwa wakila malavedave na walipobanwa wakakataa akamaka...'oo..wanasema uongo mwl...nimewakamata wakati sex ikiwa mbichi!' You can imagine vicheko na hasira humo staff room.

kulikuwa na mwingine msukuma ambaye alisomea ujermani na alikuwa hataki kusalimiwa kisukuma. kwa kujua hilo tulikuwa tunachezea shere kwa kumwamkuwa...'mwangaluka mwl! nae alifyumu ile mbaya na kujibu...mimi huwa sipendelei, siku nyingine ntakutandika..anyway mola duhu' ilikuwa ni burudani hasa ukichanganya kiswahili aliochokuwa akizungumza kwa lafudhi ya akina Mija na Matondo!!!

mbali na walimu na wanafunzi nao wana vituko vyao...
alikuwepo mwanafunzi mmoja toka shinyanga ambaye alikuwa na uwezo wa kunywa uji wa moto unaotokota in no time! ukimuuliza alidai kuwa ana friji mdomoni :-)

mwingine alitoa kioja kwa kuanguka na gudulia la uji yeye akawa chini gudulia juu na hakuna tone la uji lililodondoka :-)

Ramson said...

ha ha ha haaaaa.....Kaka Chacha, yaani nimecheka ilw mbaya mpaka wenzangu wananishangaa, HKwa kweli dada Koero anajua kuchokoza mada, maan hii nilikuwa sijawahi kukutana nayo.....Duh, nadhani Mtakatifu Kitururu, Mubelwa, Kamala, Prof. Matondo, Da Mija, Da Yasinta, watakuwa na mengi ya kutueleza, maana hakuna atakayesema kuwa hakuwahi kukutana na hayo aliyoyasema Koero...

Mimi bwana Kule Sumbawanga nako kulikuwa na vituko vyake, kuna mwalimu tulimuita Kipago, yeye alikuwa kama ana matege hivi na hawezi kubana miguu, Uchagani napo nilipowahi kusoma kulikuwa na mwalimu alikuwa anaitwa Andunje, yeye alikuwa mfupi kweli, kama mnakumbuka kitabu cha darasa la tatu kama sikosei kulikuwa na hadithi ya mtoto mmoja nadhani nai wa kike mfupi anaitwa Andunje na kutokana na ufupi wa mwalimu akaitwa hilo jina.

Jamani najaribu kukumbuka maan visa ni vingi kweli lakini kumbukumbu zimepotea

Yasinta Ngonyani said...

Oh! Koero umenikumbusha kulikuwa na mwalimu wakati nasoma shule ya msingi mwl. wa hesabu alikuwa hawezi kusema kitu bila kusema mwezi mpya kwa hiyotukampa jina la MWL. MWEZIMPYA.

Na mwinginealikuwa mwl. wa kiswahili yeye tulimwita mwl AKILI maana kila neno alilosema lazima aseme akili. duh! umenikumbusha zamani na naipenda sana zamani.

Mzee wa Changamoto said...

Tulikuwa na mwalimu wetu wa Agriculture (alale mahala pema huko aliko) ambaye aliitwa NUNGU. Huyu alikuwa mkatili saana. Ukiwa na kosa usingeweza kuwa mbele yake ukaendelea kusimama. Atakuuliza "una makosa halafu umesimama mbele yangu kama miiba ya Ngungunungu? Piga magoti".
Kama alipanga kukuadhibu (na akawa kwenye mood nzuri) atakupa option kuwa ukubali akuchape, ama akuulize swali na ukishindwa kujibu akuchape. Kisha (mara nyingi) atakuuliza Mbuzi ni nini? Sikuwahi kuona mwanafunzi yeyote akiepuka kichapo baada ya swali hilo. Mpaka anakufa hakuwahi kutupa jibu la swali hilo.
Mwingine aliitwa DICTIONARY. Huyu alikuwa mwalimu wa kiingereza kwa form one. Alikuwa akijiita "living dictionary" akimaanisha kuwa neno lolote (kwa elimu ya kidato cha kwanza) angelijua na sio tu kukutafsiria kwa kiswahili, bali mpaka kiHaya. Well! Unaweza kuona namna ambavyo tuliamini kuwa ANAJUA KIIINGEREZA CHOOOOTE wakati maswali tuliyouliza ni "nini maana ya therefore?" Hahahahaaaaaaaaaaa.
Pia tulikuwa na mwalimu mwingine (naye apumzike pema peponi) aliyepewa jina la MYUSKOS. Huyu alikuwa anatusimamia mtihani wa Biology lakini katika kuchapisha mtihani, neno moja halikusomeka. Mwanafunzi mmoja (aliyewahi kulifikia hilo swali) akamuuliza Mwalimu neno lililofutika, basi mwalimu akalitamka kuwa ni MYUSKOS. We were like whaaaaaaat?? Maana lilikuwa neno geni. Basi tulipouliza tena akasema "ngoja niandike ubaoni ili msiulize tena na tena na tena". Alipoenda kuandika, guess what? Kumbe neno lilikuwa MUSCLES.
Binafsi nili-declare ushujaa kwa kujizuia kucheka. It was funny as hell.
Wakati niko Ndanda Sekondari huko Masasi tulikuwa na Academic Master aliyepewa jina la NANG'OLO. Hata sijajua huyu ni mdudu gani ila kila mara katika kudhihirisha umwamba wake alikuwa akisema "MIMI NDIYE NANG'OLO DUME"
Wacha niachie hapa wengine waendelee

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kama mwalimu, mimi siwezi kusema cho chote hapa kwani sijui wanafunzi wangu wananiiteje. Itabidi nianze kupeleleza. Mada nzuri dada Koero!

Anonymous said...

asante dada kaero umenikumbusha mbali wakati niko sekondari huko moshi tulikuwa na mwalimu ana mashavu makubwa sana hivyo tulikuwa tunamuita manguchu na mwalimu wetu wa kiingereza tulimuita colloquial maana alipenda kulitumia hilo neno

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nikisema yangu patakuwa hapatoshi manake! mengine ni ya kihaya na nini! jina kama MKUNDI, kwetu ni nini sijui

Mija Shija Sayi said...

Basi alikuwepo mwl kule Nganza Sec, huyu nadhani alipokuwa mdogo aliugua Ndui maana uso wake wote ngozi imevurugika kwa makovu, pia
alikuwa na ulimi mzito na inabidi umsikilize vizuri kumuelewa kitu ambacho inasemeka imetokana na ugonjwa huo aliougua utotoni. Basi siku moja alikuwa darasani akifundisha darasa la mdogo wangu, wakati akiendelea kufundisha akagundua hasikilizwi na kama kuna mchezo unaendelea mle ndani maana wanafunzi walikuwa wameanza kucheka kichini chini, mwl akaminya. Huku nyuma kumbe mwanafunzi mmoja alikuwa ameandika ujumbe kwenye kikaratasi na kuanza kupasiana kichini chini, mwl akakiona kikaratasi baada ya mmoja kukosea stepu akakiomba, ikabidi apewe. Huku darasa likiwa linatetemeka akakifungua na kukisoma kimeandikwa .."Uso wa Mwl B... utadhani nyama ya ini"... Duuh Mwl alipagawa alitoka nakukipeleka ofisini, kilichofuatia ilikuwa ni darasa zima fimbo kutoka kwa waalimu wote, fimbo zile sitakaa nizisahau. Kuanzia hapo mwl alijipatia jina lingine Nyama ya ini.

Anonymous said...

Nimeisoma habari yote na comments, sijaona pointi? Yaani, objective ya kuwakejeli walimu ni nini kama sio utovu wa nidhamu? Pili, how would you feel kama ukipewa jina la kejeli kutokana na, kwa mfano, physical disability ambayo wewe hukuiomba kwa Mungu. Do you think it's fair kumwita mtu mfupi Andunje? Au mwenye kisogo kirefu? Au kichwa kikubwa? Au kumwita mwalimu Surambaya because he is not good looking?

Come on bloggers wa ki-Tanzania! Kuna mambo mengi ya maana ya kujadili kuisaidia jamii badala kukumbushia majina ya kejeli ya walimu waliowasaidia, kwa kiasi fulani, kujua kusoma na kuandika na leo kuwa bloggers

twenty 4 seven said...

nimekumbuka mbali pia..

Anonymous said...

Mimi nawakumbusha wenzagu tuliosoma shule ya msingi uhuru mchanganyiko dsm kulikuwa na mwa Mabura huyu ni zeruzeru huyu alikuwa mnoko na anapiga ile mbaya siku moja alipimpiga mwanafunzi mmoja kwa jina ni Juma ambaaye ni kipofu yeye hakujali hilo alimtmtandika kishenzi.nakumbuka kuna mw mmoja wa kike anaitwa mw Gambo alipokuja katika kipindi chake kuona ile hali basi alilia na kwa ile huruma alimtuma mwanafunzi mmoja akanunue soda na keki na akapewa yule asiye ona yaani Juma.basi mimi na wenzangu ambao nawakumbuka kama vile yussuf katwila,hamza,rashid na wengine tukaamua nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi yeye anakawaida ya kwenda kulewa tukamchukuwa paka na kutumbukiza kwenye nyumba yake kwa dirishani bwana wee!!! alivyorudi huko mbona alitia akili! siku ya jumatatu alipokuja kufundisha ana mabendej!! kila kona. na hii ndio ikawa dawa kwake. mimi saleh.

ABEL said...

Mimi hapa nina kali za mwaka huu maana nimekuwa mwalimu na pia nimepitia uwanafunzi kama wengine,Kuna Mwl.Tulimwita Bunsen Burner maana wakati anafundisha chemistry alipenda sana kuitaja,kuna mwalimu alikuwa anaitwa Shekitundu,sisi tukamwita Shekitobo,kuna mwl alijiita G.P(Godfrey Paul)wanafunzi wakamwita Guruwe Pori,kuna mwalimu huko Sumbawanga Kanta tulimwita Pocho kwa kuwa alishindwa kutamka Portuguese na alitamka pochogiz,Kuna Chijua cha Pombe,ha ha ha ha Nadhani majina haya yana reflect elimu ya Tanzania na unaweza kujifunza ubora wa elimu tuipatayo kwa kujua majina ya walimu.Ugeni wa vifaa kama bursen burner,maneno kama however na matamshi na vitendo vya walimu vimeathiri nick names zao