Friday, July 16, 2010

FULANA YANGU

Muafrika halisi

Jana katika pita pita zangu katika viunga vya hapa Arusha nikakutana na hii fulana na ikanivutia hasa. Ilibidi nijisachi na kuinunua kwani ilinipa taswira ya Mwanamke wa Kiafrika halisi.
pamoja na mtandao kuwa Kimeo siku za hivi karibuni, lakini nimemudu kuiweka picha hii kibarazani kwangu ili niweze kushea na wanablog na wasomaji wa kibaraza hiki kisichoisha visa na mikasa. Labda niwaulize wasomaji wa kibaraza hiki, kama nimependeza au?

16 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Bila kichwa utapendezaje?

Walopendeza ni hao walopo kifuani kwako...lol!

Natania mwayego!!!

Seriously: fulana ni utamaduni wetu ama wa kuiga sehemu? hatukuwa na fulana enzi hizo. Nafurahi fulana hiyo ina vikatuni vinavyoonesha kwa namna moja ama nyingine hali dhalili ya mwanamke wa kiafrika.

Nawaza kama ingekuwa na picha ya 'fataki' (mwanaume mwenye kitambi kama cha hao wamama) ungeinunua katika kile unachokieleza kama 'kuonekana mwafrika halisi'?

Nawaza tu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwani ulivaa ili upendeze, uwe mwafrika au ufikishe ujumbe?

najiuliza tu

Yasinta Ngonyani said...

T-shirt ni nzuri sana hata mie nimeipenda na nitaisaka mpaka niipata. Huyo aliyevaa kapendazeza na nina uhakika sio wewe kwani hatuoni kichwa kwa huyu hatuwezi kusema umependeza.Ni kweli hapo ni mwafrika halisi. Naomba ukizikuta nunua mbili na moja kwa ajili yangu.

Koero Mkundi said...

Chacha na Kmala endeleeni kujiuliza, na dada Yasinta huyo ni mie na hapo nilipiga picha kwa karibu zaidi ili muone hizo picha za kwenye fulana yangu.

Swala hapo halikuwa sura yangu ambayo bila shaka mnaijua, bali ilikuwa ni kuuza sura za hao kinamama wawili na watoto wao wawili walioko kwenye fulana yangu ,.....mweh...mbona na wewe Yasinta unakuwa kama umekumbwa na JINI KIPWEPWERE?

Anonymous said...

Dada yangu,tatizo na uzuri wa picha kama hiyo,nikuwa kila mtu akiiona anakuwa natafsiri yake.hiyo ndo uzuriwake,matatizo yanakuja pale wewe binafs unapogundua sivyo ulivyo kuwa unatarajia watu kutoa hojazao kuhusu picha hiyo.lakini msukumo ulio upata mpaka kutuma picha hiyo,hiyo hasa ndiyo msimamo wako,na ndiyo mawazoyako ambayoyo hayawezi fanana asilimia mia na ya watoa hoja juu ya picha nzuri uliyo tutumia.nahii ni saikolojia ya binaadamu katika ulimwengu wa sanaa nijinsi gani unakielezea kitu ukionacho mbele yako mfano picha hiyo.
shukrani,mimi nimeipenda tu.kaka s.

Koero Mkundi said...

Annoy hapo juu aka kaka S, nimekuelewa barabara, na huo ndio uzuri wa kublog. Ahsante sana kwa maoni yako, kaka na ninakukaribisha tena na tena hapa kibarazani kutoa mawazo yako bila hofu una uhuru wa kusema chochote kwa manufaa ya blog hiii

PASSION4FASHION.TZ said...

Koero umependeza sana na hiyo fulana yako,hata mimi nimeipenda mwafrika halisi,kaka Chacha(mtoto wa fisi)....lol fulana hatukuwa nazo hata hizo khanga na vitenge hatukuwa navyo,tumeiga na hata hao tuliowaiga nao hawakuwa navyo nao wanaiga na bado tunaiga nao wanaiga..... kama nimemuelewa Koero kilichomvutia hapo ni hiyo picha ya hao waafrika halisi juu ya hiyo fulana.

Anonymous said...

mimi ninapenda sana blogu yako imekuwa inatufundisha mambo mengi sana natunajifunza mengi kupitia blogu yako ubarikiwe sana sipitishi siku sijapitia blogu yako mimi leo niko nje kidogo ya mada mimi niko nje ya nchi kidogo sasa napenda sana kusoma hari kutoka tz sasa naomba unisaidii kitu kimoja ambayo nilikuwa natafuta lakini sjafanikwa naomba ikiwezekana uniwekee nyimbo ya gospel alizoziimba remmy ongala baada ya kuokoka na wachangiaji wenginekm kuna anayejua namna nitapa hizo nyimbo pls

Anonymous said...

Hao wanawake kwenye picha za tshirt wanaonekana kuwa na matako makubwa. Mimi napenda matako makubwa. Nikipata mmoja kama hawa it 'll be cool.

Koero Mkundi said...

Annony wa 17 July 2010 1:55 AM, umenitiolea mpya, yaani kilichokuvutia katika hiyo picha ya hao wanawake kwenye fulana ni hayo makalio yao!!!

Ama kweli kublog kuna raha zake, na hii ndio mojawapo ya raha ya kublog maan unakutana na visa asili vingi kikiwemo hiki cha wapenda makalio ya wanwwake.

Kuna mada naandaa juu ya kile kinachowavutia wanaume kwa wanawake hususan maumbile.

Je ni kitu gani kinachowafanya wanaume wengi wa Kiafrika kupenda wanawake wenye makalio makubwa?

MADA IKO JIKONI WANDUGU KAENI MKAO WA KULA.......

John Mwaipopo said...

tehe! tehe! tehe! ukiona nacheka nafurahia raha ya kublogu na kujutia ama kukasirikia siku umeme, mtandao ama mimi mwenyewe kutopatikana ili kublogu.

MARKUS MPANGALA said...

Hii mada ya matako a.k.a makalio makubwa inanikuna sana, maana kuna watu a.k.a mijitu au vijitu utawaonea huruma utadhani wameambiwa leo unakufa kisa kalio kubwa.

MASHTAKA
Mama Mchungaji kuna mada mbili hujazijadili kama ulivyoeleza kipindi cha nyuma. kwakukumbusha ni kuhusu MAPROFESA na wale walioshindwa UPADRI. nadhani umenielewa sasa. eeeeh mwanamke takoooooo siyo ha ha ha ha MCHARUKOOOOOOO

MARKUS MPANGALA said...

Hii mada ya matako a.k.a makalio makubwa inanikuna sana, maana kuna watu a.k.a mijitu au vijitu utawaonea huruma utadhani wameambiwa leo unakufa kisa kalio kubwa.

MASHTAKA
Mama Mchungaji kuna mada mbili hujazijadili kama ulivyoeleza kipindi cha nyuma. kwakukumbusha ni kuhusu MAPROFESA na wale walioshindwa UPADRI. nadhani umenielewa sasa. eeeeh mwanamke takoooooo siyo ha ha ha ha MCHARUKOOOOOOO

Christian Bwaya said...

Nadhani utamaduni wetu unaweza kuboreshwa kwenda na wakati. Hata kama hatukuwa tunavaaga tsheti zamani, kwa sasa tukizivaa zikiwa na maonjo ya Kiafrika kama alivyofanya Koero bado ni kuuenzi utamaduni wetu!

Simon Kitururu said...

Uliyepigwa picha unakifua kizuri kweli.
Ni wazo tu baada ya T shirt kuonwa.:-(

Mzee wa Changamoto said...

".....nikakutana na hii fulana na ikanivutia hasa. Ilibidi nijisachi na kuinunua kwani ilinipa taswira ya Mwanamke wa Kiafrika halisi."
Najitahidi kuamini kuwa huamini kuwa UAFRIKA HALISI wanunuliwa ama kuvaliwa. Najitahidi kuamini kuwa watambua kuwa ulipovaa fulana hiyo ULIFICHA uafrika halisi (kama uliooneshwa na Dada Yasinta hapa http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/07/warembo-wa-kihimbapicha-ya-wiki-hii.html)
Najitahidi kuamini kuwa unatambua kuwa huwezi pata uafrika halisi ulo "made in china"
Na pengine hutapata uafrika halisi kwa kuwa na kilichotengenezwa kwa malighafi zilizoinyinya Afrika zikakimbizwa kwa waliozibuni na kubuni mchoro wa mwafrika kisha wakazitengenezea huko ili wawauzie waafrika wakitegemea faida.
Narejea tena kuwa uafrika halisi na ambao umeukimbia kwa kununua hiyo fulana ni huu hapa http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/07/warembo-wa-kihimbapicha-ya-wiki-hii.html

Hahahahaaaaaaaaaaaaaa
NAWAZA KWA SAUTI TUUU
Nakupenda dadangu na niliku-miss saana