Hii taswira ya Arusha nimeipenda sana
Hatimaye nimetinga jijini Dar kimya kimya, baada ya kurudisha fomu za kugombea ubunge kule Arusha. Kuna wadau wamedai kuwa, I am too young to be politician, lakini nasema hatishwi mtu hapa, kwani nani hapendi kusinzia mjengoni kule Dom….LOL.
Nitakuwa Dar kwa siku mbili tatu , lakini nitakuwa kifamilia zaidi, nikipata mibaraka ya wazazi katika kukabiliana na changamoto za kugombea kuteuliwa.
Naamini tuko pamoja……Je, hamjambo wasomaji na wanablog wenzangu?
Nitakuwa Dar kwa siku mbili tatu , lakini nitakuwa kifamilia zaidi, nikipata mibaraka ya wazazi katika kukabiliana na changamoto za kugombea kuteuliwa.
Naamini tuko pamoja……Je, hamjambo wasomaji na wanablog wenzangu?
10 comments:
aisee!
Karibu sana Tanzania..lol!
Pamoja na kidamisi cha mtandao lakini bado tupotupo sana!!!!
Ni ule ule utani wako au umetangaza nia kweli? Jaribu basi kuwa "siriazi" kidogo ili watu tujue.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika Arusha na nilipapenda sana!
Mama Mchungaji hongera sana kwa kurudisha fomu. Naamini upo siriazi. Nasi jamii ya wanablog tutakuwa na mwakilishi mjengoni ingawa kuna uwezekano ubize wa majukumu na kubadilika kwa mtazamo kunaweza kukufanya uache kublog.
Alaa kumbe ushaingia Dar? Si unajua kuna wenyeji wa huu mji?
Karibu sana katika ulimwengu huu. Naamini wengi wamekumiss sana mimi nikiwa mojawapo. Na nashukuru sana na nakupongeza mdogo wangu kwa mama mwingine umekwisha peleka hizo fomu za Ubenge angalao na sisi katika ukoo tuwe na Mbunge...LOL. Tupo pamoja kabisa
Hongera kwa kurudisha fomu. Inabidi utueleze kabisa hapa kibarazani umepanga kutusaidia vipi. Nashauri hiyo karaha ya kobe (mtandao mchovu) uipe kipaumbele hili rigwaride riende mbere kwa mbere.
NAANZA HIVI; ni jana tu nilikuwa najadili suala la vijana na uchaguzi wa mwaka nikiwa na Mwalimu wangu Muhingo Rweyemamu(RAI). kikubwa nilikuwa nachangia mada yake iliyotoka Alhamisi wiki hii kuhusu namna vijana wanavyoamua kujiingiza moja kwa moja kushindana na wazee badala ya kusbiri. hili ni jambo zuri, lakini Muhingo na mimi tunakubaliana kuwa vijana hawakuandaliwa, na tutatakiwa kuandaliwa lkufanya hivi yaani kuthubutu kama Mama Mchungaji bila kujali umri. Tulirejea ELIMU YA MAKUZI 'Insearch of Identity' kwamba mara nyingi vijana tunataka kujitambulisha, tatizo tunakosa misingi ya kujitambulisha kwasababu hatujaandaliwa kujitambulisha. MATOKEO yake ni kwamba vijana wameamua KUJITAMBULISHA lakini hawajajua wanatakiwa kujitambulisha namna gani. Kwa uchaguzi huu tulikubaliana ni wa vijana lakini ule wa 2015 ndiyo utakuwa mzuri kwa vijana na zaidi ule wa 2020 ndiyo utakuwa haswa kwa vijana kwasababu AS MUCH AS WE DARE ndivyo tunavoamsha hari ya kufanya hivi. angalia namna vijana wanavyoshughulika na kugombea aidha udiwani,viti maalumu au ubunge, ni AS MUCH AS WE COULD ndivyo tunavyojenga nyumba. wazee naamini watashituka lakini muda umewaacha hawawezi kuzuia tena, na hata ule muda wao wa kutaka kuwaandaa vijana unakimbia, wanatakiwa nao kukimbia.
SASA mama Mchungaji mimi nakuunga mkono kwa hili UMENIKUNA HASWAAAAAA. katika hili nimejaribu kutafakari na kukufikiria tangu ulipodokeza unawania viti maalumu, nimesoma maandiko yako na kuhesabu TABIA yako kisha nikapata jawabu AS MUCH AS YOU DARE unafanana na Nakaaya SUMARI au Halima Mdee, nawapenda sana kwa jitihada zao za KUJITAMBULISHA. Hapo ndipo ninapowatamani wanawake wafikie, hapo ndipo ninapowataka wanawake wafanye.
Mama mchungaji YOUR EYES, YET MORE MY EYES,
YOUR BLOOD YET MORE MY BLOOD ...........rejea shairi la Armando Guebuza(rais wa msumbiji sasa).
mh, weka nia tu, mimi nimehairisha mpaka nilee kwanza
mie watu ambao wanatoa uoga na kujitosa kwenye siasa huwa nawafagilia sana. acha sie waoga tuendelee kuwa waoga na kuiacha inchi mithili iliumbwa kwa ajili ya akina fulani tu. baraka zangu umepata zote, ila sina uhakia baraka zangu zina upako kiasi gani(sio ule wa yasinta ngonyani)wakilisha.
waoga wengine wameshachangia hapo juu.
Kaza buti mwana blogu. Kaza buti uingie bungeni. Kaza buti mwana kwetu. Kaza buti iwezekane!
Kwa hiyo unaingia kwa viti maalum vya U-BLOG ama UCHUNGAJI?
Kinamama washajaa huko na najua hujawa mama. Na sioni kingine kikufaacho zaidi ya huku unakokumudu.
Mbunge wa viti maalum (Tovuti na blogu) Mhe Koreo Mkundi
Mmmmmmmhhhh!! Sounds great
Post a Comment