Friday, August 20, 2010

Labda USIMTISHE MTOTO wako!

Kaka Simon wa tatu kushoto......LOL

Kuna kitu WATU wengi hawajui kuhusu MIE Simon KITURURU,...... ila ukweli ni kwamba mkono wangu wa kulia haufanyi kazi vizuri kama inavyotakiwa ,...


... kwa KIFUPI hata UKIWA sio mbali sana siwezi nikakurushia jiwe kama nataka kukubwenga JIWE kirahisi na MKONO WA KULIA.Na tatizo lilianza kisa nilikuwa naficha siri eti kwa kumuogopa BABA.:-(


STORI fupi laini na YA KWELI :Tulikuwa tunaishi SONGEA na moja ya vitu MDINGI alikuwa hapendi ikiwa pamoja na KUWA MCHAFU , kufeli mtihani enzi hizo nikisoma SHULE ya MSINGI MFARANYAKI (kitu ambacho nilikuwa sifeli) ,....


..... nilikatazwa kupanda juu ya MITI aka kuparamia miti kimichezo.Siku moja mie na marafiki zangu tukaenda kuiba maembe aka KUTUNGUA MAEMBE yasiyo yetu shambani kwa WANAFUNZI WA SONGEA GIRLS.


Enzi hizo shamba la songea GIRLS lilikuwa kubwa na sisi tulikuwa tunaingilia upande wa UWANJA WA MEDICAL karibu na nyumba za mwisho mwisho za walimu enzi hizo za miaka ya NAINTINI EITEZ( (Kumbuka ni miaka mingi sijafika Ruvuma sijui maeneo hayo yakoje siku hizi)Basi BWANA katika kuwinda maembe bolibo na embe sindano tukaupata mti ambao mbivu zilikuwa zimenona juu kabisa.


Na mie ambaye hukatazwa kupanda miti nilikuwa kiongozi kuparamia juu kabisa kutikisa mti.Kilichotokea ni kwamba,....... katika kutikisa tawi ili kudondosha maembe tawi likakatika na kilichofuata nilijikuta chini nikijiuliza niko HAI au NIMEKUFA,..........na chaajabu hata marafiki zangu wakinisemesha nilikuwa siamini kama niko hai kwa KUWASIKIA kwa kuwa nilikuwa nahisi kuwa labda hata MFU akisemeshwa huwa anasikia.:-)


Katika kufupisha stori hii ya kweli;... ....nilivyoanguka nilitegua mkono wa kulia na baadaye nikaja stukia labda na kitu kingine mkononi kiliharibika.:-(


KIKUBWA:Kwa kuwa kwanza nilikatazwa kupanda miti na PILI miye na marafiki zangu tulikuwa tunaiba maembe ya wana SONGEA GIRLS nilifikiri sio busara kusimulia hicho kitu nyumbani. NILIFICHA maumivu na ugonjwa kisa NAMUOGOPA BABA....


.....na kwa bahati nzuri ilikuwa ni kipindi cha baridi SONGEA na maswala ya SWETA na JACKETI pamoja na MAIGIZO kuwa NIKO BOMBA yaliniwezesha kuficha nimeumia mpaka mkono ukapona kinamna. TATIZO ni kwamba mkono ulivyopona mpaka leo hauwezi kumlenga MBAYUWAYU bila msaada wa mkono wa kushoto.Kwa kifupi :


Nilijitia udhaifu wa mwili KWA KUFICHA UGONJWA kisa NAOGOPA KUCHAPWA. na BABA:-(Unajua tena AKILI ZA KITOTO).
Stori hii nimeipenda sana na nimeweka hapa ili wasomaji wa kibaraza hiki wapate kujifunza kupitia simulizi hii ya kweli ya kaka yangu Simon Mkodo Kitururu. kwa kumsoma zaidi waweza kubofya hapa

9 comments:

emu-three said...

Wanasema tabia ya mtoto, au hulka au, kipawa huanzia utotoni. vitu hivoo vinaweza kutokea kwa kuzaliwa, kujengwa kutokana na mazingira, shule nk, sasa kwa mkuu Simion, yote yanajionyesha katika picha!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mficha uchi hazai!!

MARKUS MPANGALA said...

Mtakatifu Kitururu umenikumbusha sana mambo ya embe Bolibo na Sindano. Kumbuka embe sikio, Ndodi na kadhalika. Umenikumbusha kovu langu la mkono wa kushto enzi za kupanda miti na kuchuma MIZANGIZANGI...... kitururu unakumbukaaaaaa hiii Kituuuu????? ha ha ha ha Ysinta vipiiii??? kaka Jacob Malihojaaaaaa unakumbuka hii kitu??? Katika kukurudishia kumbukumba Mtakatifu Kitururu, siku hizi ile barabara uliyokuwa unakwenda kuchuma maembe iliwekwa wigo a.k.a Fensi lakini ukiendelea kushuka hivi utaona miti ya maembe imechoka kama wazee lakini kuna viunga mabinti muwali wa sekondari wamejimwaga katika vile vivuli, na siku hizi hakuna o level mtakatifu kuna A Level tuuuuu. Sasa yale maembe Bolibo yapo, ila ukibambwa mwanangu utakojoleshwa weeeeee hadi ukomeeeee... sasa umenikumbusha enzi zile natocha choo cha wasichana(maana hakuna choo cha wavulana pale). duh! hamadiiii mwanafunzi huyoooo akashangaa njemba imeingia chooni inakuwajeeeee? kumbe ilikuwa katika harakati za kuvizia Bolibo na Sindano Kisha ndodi.

Turudi katika Mfaranyaki.... nyumba zimezajazana kama upupu, labda kule alikojenga Dada Yasinta, alikochukua uwanja mkubwaaaa kifisadiiiiiiiii kama Gymkana mweeee kueleeee jamani. sasa ile stori ya kuvumilia ndani ya sweta ni nomaaaa

Kitururu umenikuna sana... ila UMESAHAU kuwa VUMBI lilikuwa linastawisha utamu wa maembe ha ha ha ha ha ha a.k.a Ngunja duh!!!! halafu ukutwe unakula maembe ya jeshi yale uone cha mtemi mkuni

Yasinta Ngonyani said...

kumbe wezi tupo wengi! mmmhh mpaka soni mimi bwana nilikuwa au nisema ni mgonjwa wa malimao(ndimu) basi bwana pale shuleni Lundo enzi hizo kulikuwa na bustani kubwa ya michungwa, malimao, maenmbe minazi nk. Ila mie nilizamia na malimao halafu sasa nilikuwa nakula malimao kwa chumvu. Na hiyo chumvi pia nilikuwa naiba mama akiuliza nani amechukua chumvi mie ndo nakuwa wa kwanza kujibu SIJUI kuogopa viboko.

Kaka Simon nakupongeza kwa kusema ukweli leo hata kama umeaharibu mkono lakini nadhani umejifunza kitu na pia umewafunza wengine ambai bado hawajawa baba na mama na pia hata wale ambao ni baba na mama. Ahsante Kaka Mkodo pia Mdogo wangu Koero kwa kutukumbusha hii mada.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mshajua eh!

PASSION4FASHION.TZ said...

Kaka Simon pole sana,ulikuwa utoto tuu sasa umekuwa umejua kosalako.

Koero nawe? hebu nenda na kwa bibi Koero ukapate simulizi zake au unaogopa omcheku? hahahaaaaaa!ukiongea nae mpe hi!5

Maisara Wastara said...

Kwa kweli smulizi nyingi za utotoni zinafurahisha na nyingine zinahuzunisha sana.

Kusema kweli hili ni somo kwa wazazi na wale wanotarajia kuwa wazazi kama Koero mwenyewe (Inshaalah mungu amjaalie apate mume)

Ingawa tunasema ni funzo kwa kaka Kitururu, lakini pia tumejifunza na kuona athari za kuwa wakali kwa watoto kupita kiasi.

Je baba yake Simon anajisikiaje amuonapo mwanae akishindwa hata kumlenga mbayuwayu?

Je hahisi kuwa alichangia mwanaye kuwa katika hali hiyo?

Kama wewer ni mzazi basi jifunze kuanzia leo kuwa wa[pole kwa watoto na kama itabidi kuwa mkali, basi ukali uwe na mantiki, sio kila wakati unapandwa na jazba hata kwa kosa la kumwaga mboga.

Ahsante Koero kwa kutuwekea simulizi hii, naamini wengi walikuwa hawajaisoma pale kwa kaka Simon, lakini baada ya kuiweka hapa kwako, tumejifunza mengi.

Simon Kitururu said...

:-)

Christian Bwaya said...

Msimulizi mzuri...! Kusimulia nako ni kipaji cha pekee.