Sunday, December 20, 2009

HIVI HUYU KIJANA NI NANI?

Picha kwa hisani yake mwenyewe
Ni kijana mdogo kwa umri lakini ni mkubwa kwa umbo.
Kijana huyu ni suriama aliyechanganya kati ya makabila mawili ya Mpare kutoka milima ya upareni na Mjita kutoka kule Musoma kusikoisha vita kati ya koo za Wanchori na Wanchoka.

Alifanikiwa kupata elimu yake kupitia shule kadhaa hapa nchini kabla hajakuwa mjanja na kutowekea Ughaibuni miaka kadhaa iliyopita, akiishi katika mojawapo ya nchi za Scandinavia.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa, wakati akiwa shuleni alikuwa na kipaji maalum cha sanaa na alikuwa ni bingwa wa kucheza na misamiati na nahau. Watu waliowahi kusoma naye wanakiri kuwa alikuwa na tatizo la kutomudu kutumia Tafsida pale alipotakiwa kutoa mada fulani katika midahalo ya shule.

Tatizo hilo lilikuwa likimletea matatizo na waalimu wake kwa kuwa alionekana kama vile hana adabu japokuwa ujumbe alioutoa ulikuwa na maana sana katika jamii na wenye kufundisha na kufikirisha pia. Hata hivyo wapo waliomuelewa na wengi walijifunza mengi kupitia hoja zake hizo zilizojaa vioja. Msome kwa kubofya hapa.

Pamoja na misukosuko aliyoipata kutoka kwa waalimu wake hakukata tamaa aliendeleza kipaji chake na baada ya kutowekea ughaibuni amekuwa muelimishaji mzuri kupitia kibaraza chake alichokipachika jina la Mawazoni.

Katika kibaraza hicho amekuwa akifikisha ujumbe wake wa kuielimisha jamii kwa kutumia misamiati nahau na tilalila zake anazozijua mwenyewe na kutokana na kutotumia Tafsida wengi wamekuwa hawamwelewi kwa kuwa wakisoma kichwa cha habari tu wanachoka na wanaacha, maana tafsiri inayokwenda akilini mwao ni kitu kingine badala ya kile kilichokusudiwa.

Tatizo ninaloliona katika makala zake si lugha iliyotumika bali ni tafsiri inayokwenda vichwani mwa wasomaji kwa kukimbilia kuhukumu kichwa cha habari badala ya kile kilichomo ndani ya hicho kichwa cha habari. Kwa mfano halisi unaweza kubofya hapa au hapa.

Ni mchangiaji mzuri sana katika vibaraza vya wengine na kwa kutumia staili hiyo hiyo ya Ant tafsida, amekuwa akiwachanganya wasomaji wengi na naomba nikiri kuwa hata mimi nilikuwa ni mmoja wapo wa wale waliokuwa hawamwelewi kabisa.

Ilinichukua muda kidogo kumwelewa na kwa kutumia kamusi ya Kiswahili na vitabu mbalimbali vya Kiswahili, kikiwamo kitabu kinachoitwa Titi la Mkwe na cha Jando na Unyago, nilimudu kumuelewa kijana huyu na makala zake zilizojaa nahau na upembuzi yakinifu.

Naamini hanifahamu na mimi pia simfahamu ila kwa kupitia vibarazani mwetu tumetokea kufahamiana japo si kwa karibu sana. Pamoja na hayo bado najiuliza hivi huyu kijana ni nani?

15 comments:

Anonymous said...

Lugha yake na ulimwengu wake si wa kusoma wangu wangu ukaondoka, utajikuta unabeba kisicho chako. Nadhani Mtakatifu Kitururu anatumia lugha ya kuchokoza msomaji na kisha kumwacha apate maana au aendelee kudadisi maana halisi ya mwandishi na kwa hakika, ujumbe wake haujakamilika kwa posti ama tungo moja. Huyo ndiye Mtakatifu Kitururu nimfahamuye mimi.

Simon Kitururu said...

@kOERO : yANI ULIVYONISIFIA NISIPO PATA DEMU WA MTAANI BASI LAZIMA NIENDE KWA kIBABU FULANI bAGAMOYO:-(

kUHUSU SWALI LA mWISHO NIKILINUKUU ``Pamoja na hayo bado najiuliza hivi huyu kijana ni nani? -MWISHO WA NUKUU.

mimi mweNYEWE sijui jibu.:-(

Simon Kitururu said...

@kOERO : HUDHANI KATIKA swala uliloongelea neno `` KIJANA ´´ lingekuwa bomba kama lungeliandika ``MZEE HUYU?´´


:-(

Simon Kitururu said...

@Subi: Unajua kama ningekamilisha tungo labda ungekuwa mama watoto wangu?

Ni wazo tu hili na usinitukane Kichaga weye ingawa unajua SIE WAPARE ni bomba kuliko Wachaga .:-)

Mija Shija Sayi said...

Huyu ndiye the "think aloud" mwenyewe.

Koero Mkundi said...

Kaka Ambiere Simon Mkodo Kitururu hivi nikuite mzee wakati huna ndevu wala Mvi, si nitakuwa nawachekesha walionuna....

Wewe ni kijana tu...tena bwana mdogo sana...na sasa inabidi urudi kwenu Musoma ukaozeshwe binti kigori wa Kijita...maana Upareni huwezi kupewa mke kwa sababau wapare hawajazoea Mkong'oto kama wanawake wa Kijita.

Tena fanya haraka usije ukafa kwa UKIMWI bila kuacha vijukuu....LOL

Yasinta Ngonyani said...

Mada imeandikwa kwa ubunifu kweli. Huyu ndiyo Mt. Simon kitururu bwana wa mawazo. Awazaye kwa uwazi.

Mzee wa Changamoto said...

Mtaka"tifu" a.k.a Mtakafujo Simon wa Kitururu ni kama asemavyo, MAWAZONI.
Kumsoma yeye ni kudhihirisha dhana yangu kuliko mimi mwenyewe.
Anasema UKWELI na anausema asemavyo anapolitatua tatizo. Sasa lilalokuja kuleta tatizo ni namna mtu alionalo tatizo.
Ndio maana nikasema dhana yangu kuwa anakuwa mawazoni na watu wanasoma mawazo kuona tatizo na NAMNA WAONAVYO TATIZO NDIO TATIZO

Luuuv ya Sis and thanx for being you

Faith S Hilary said...

Hehe! Huyo ndio "Mtakatifu Simon Kitururu", anayenifanya fani yangu ya "skimming" iwe harder than it should be.

Maana personally mpaka nielewe anachoandika, it takes me about 20 minutes each post. Ila makala zake naona ni za kuburudisha na vile vile ni "chemsha bongo" fulani. Keep doin ur thing bro!

Mzee wa Changamoto said...

Well!!! Stop "skimming" my Lil' Sis.
Another addiction that doesn't work in some places like Mawazoni kwake Kitururu.
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa

MARKUS MPANGALA said...

Mtakatifu

Faith S Hilary said...

Mzee wa Changamoto, don't even go there! sometimes it works and sometimes it doesn't...so let me use it when it works lol...so stop it!!!

John Mwaipopo said...

mie huwa nafikiri upungufu wa comment katika post yake ni miongoni mwa sifa tele-tele za blogu yake. wachangiaji 'huogopa' kujikwaa ulimi. ombwe katika kijisehemu cha comment chake una maana kuu. genious nigger, this boy is.

Albert Kissima said...

Duh!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mambo ya kitakatifu hayo