Thursday, December 31, 2009

NIMETAFAKARI MAONI YENU, VUKANI KUENDELEA KUWA MTANDAONI.

Kazi na Dawa

Ni jambo la kujivunia, kung’amua kuwa kumbe blog ya Vukani iko juu na inapendwa. Kusema kweli sikuwahi kufahamu kuwa blog ya vukani inapendwa kiasi hiki na hilo limenifanya nifikirie upya uamuzi wangu.

Ulikuwa ni uamuzi mgumu sana, lakini nimeona ni vyema niheshimu maoni ya wasomaji wa blog hii na wanablog wenzangu na hivyo nitaendelelea kublog kama kawaida. Tarajieni mabadiliko makubwa katika blog hii kwani mwaka mpya na mambo mapya…au sio?

Natoa shukrani kwa wasomaji wote, mliotumia muda wenu kutoa maoni na wengine kuniandikia email binafsi, nawahakikishieni kuwa blog ya Vukani itaendelea kuwepo kama kawaida.

Sina mengi kwa leo ngoja nijiandae kwa ujio wa mwaka mpya wa 2010.

Ahsanteni sana.

7 comments:

Faith S Hilary said...

kweli??? basi mi nipo kama kawa

Albert Kissima said...

Naaam,habari njema hizi, ni furaha kweli kweli na hii ni zawadi ya Mwaka mpya kwa wadau wote wa blog yako.

Heri ya mwaka mpya kwako, kwa familia yako na wadau wooote wa blogu hii.

Mzee wa Changamoto said...

Senkyu, senkyu, senkyu.
Senkyu vere vere.

Asante Dada kwa kutufikiria. Basi tunasubiri mabadiliko na kwa hakika kurejea kwako ni faraja kwetu. Basi nakutakia mwendelezo mwema katika ku-blog na mpangilio mzuri wa muda ili uweze kukamilisha yale MUHIMU ambayo unastahili kufanya pia.
Love you as always Lil Sis

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ulikuwa na ugiligili binti.

unajua kuna wakati unaweza kuhisi kwamba labda kublogu hakuna maana kwa sababu labda ni mara chache kublogu yanayokuhusu wewe kumbe watu kibao ni wapenzi na wanafuatilia hili

ungeamua kuacha bila kuandika ujumbe, wangeumia wengi sana kwa uamuzi wako.

binafsi huwa naaza kazi kwa kuzipitia blog kibao then job. niwapo mbali na mtandao duku duku kubwa huwa ni kwenye blog kuna nini

blog ni muhimu na zinapendwa na wengi kuliko unavyoweza kufikiri. muhimu ni kufanya kazi yako kwa makini, moyo na upendo kwa wasomaji.

Mija Shija Sayi said...

Asante sana Vidukani kwa kurudi, nimefarijika mno huwezi amini.

Nimezisoma makala ambazo zilikuletea matata na familia yako pamoja na kasheshe ulizopata ulipotaka kuacha masomo kwa ajili ya ujasiliamali.

Koero kitu kimoja ninachoweza kukwambia hapo ni kwamba UNA BAHATI SANA KUPATA WAZAZI ULIONAO NA WAZAZI WAKO WANA BAHATI SANA KUPATA BINTI KAMA WEWE, Binti mdadisi anayetaka kuujua ukweli na si kuburuzwa na dunia hii hatari. Na wazazi makini wanaotaka kuhakikisha binti yao yuko katika mstari(right lane)wakati akiendelea kupambana na dunia yake. Hope hukuacha shule.

Mna bahati mno, na karibu tena katika libeneke.

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ya ajabu kwa kusikia habari hii. Nasema KARIBU TENA TENA SANA MDOGO WANGU.

MARKUS MPANGALA said...

KAMALA UMENENA KAKA, VIPI ZILE NDEFU ZAKO KIDEVUNI ULINYOA SIKU NDOA/HARUSI? Lol.......

sikilizeni mimi Koero alinipachika jina la PAROKO,NA MHAFIDHINA, halafu huku mtaani marafiki wananiita WAKALE AU MCHUNGAJI.

sasa Koero mwenyewe kaongeza jina jingine MCHARUKO jamani nimekubali.......

SASA..................... NASHINDWA KUMPACHIKA JINA MWENYEWE TUKANA NA KUTUAGA KIUCHOYO. NDIYO KOERO MCHOYO KWANINI ULITAKA KUTUKIMBIA WANABLOGU? NIMEGUNDUA LABDA TUMWITE MCHOYO....hapana shauri yako mie simo ukimwita....mimi natafuta jina sahihi la huyu binti maana hii hatari.
Ndiyo maana siwezi kupitisha siku bila kumsoma MTAKATIFU WA FALSAFA NA WAZO NDANI YA NENO. + Ukijumlisha na VUKANI?= MICHARUKO