Thursday, May 27, 2010

NAELEKEA UZEENI SASA!

Naelekea uzeeni sasa!

Msione kimya jamani ni majukumu yamenizidi tu.

Kwani nashindwa nijigawe vipi.

Kuna wakati mtu unashindwa kujua, ni kitu gani nikipe umuhimu, kati ya mambo mawili ninayoyapenda sana.

Napenda sana kublog na naomba nikiri kuwa kublog ni kitu ambacho kimenibadili sana kifikra tofauti na nilivyokuwa awali.

Lakini pia ninayo majukumu ya kiofisi na ya kifamilia kama mwanamke.

Ni hivi karibuni nimesherehekea miaka 25 tangu kuwepo kwangu hapa duniani.

Safari ya kuelekea ukubwani ndio imekwishaanza na ni lazima niwe mtulivu kimwili na kiakili.
Lakini nitapata wapi muda huo ilhali majukumu yamenizidi mie mtoto wa mzee Mkundi.

Mawazo yamenisonga nashindwa hata la kusema.
Kama kuna kitu ambacho hamkijui, ni kwamba, tasnia ya blog imejaa msongamano wa watu wenye akili tofauti, ukitaka kublog kwa amani ni lazima uwe na akili kama za mwendawazimu.

Ni mengi yamesemwa, lakini, mweh! Nimeyaacha yapite, kwani baada ya kitambo kidogo yatapita na kuyasahau.

Mambo mengi nimeyaona na mengi nimejifunza tangu kuanza kublog, naelekea uzeeni sasa ni lazima nitumie busara.

Nimejifunza kwa wasomaji na wanablog wenzangu na naamini wao pia wamejifunza kupitia fikra zangu hizi za kiwendawazimu.

Dunia imenielemea na ninahisi nina deni ambalo ni lazima nililipe, kwani kuna watu nyuma yangu ambao wananihitaji niwasemee.

Ohh! Koero mie, Nitapata wapi muda huo?

Nadhani nahitaji nijipange sawa sawa,.

Na ninajua nitashinda.

Majaribu ni mengi sana na mitihani nayo pia ni mingi.

Naomba mnivumilie kwa kipindi hili, ambacho nimeadimika, na ninaamini mpaka wiki ijayo nitarejea kama zamani.

Msione kimya bado ningalipo………..

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kwa ujumbe kwani nilianza kupata wasiwasi kuwa upo wapi? miaka 25 Hongera sana na ujua ya kwamba si uzee kabisa na wala huelekei uzeeni. Nimeipenda tarehe yako 25/5 na miaka 25. Upendo daiama!!

Fadhy Mtanga said...

Umri unasonga hivyo. Chagua mapema.

Anonymous said...

Namuonea huruma, huyo ambaye bahati itamdondokea kumuoa binti huyu, kwani kwa jinsi alivyo mwanaharakati huyu!.....patakuwa hapatoshi

Maisara Wastara said...

Tupo pamoja mwanakwetu,

Simon Kitururu said...

Kila la kheri kwa ufanyalo Mwanakwetu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kifo chaja. ila sasa ni kweli blog inabidi uwe na akili kama za chacha ng'wanambiti au kitururu

Mwanasosholojia said...

Mmh!Ujumbe mzito da Koero

Unknown said...

Usikonde mama, unampomtumainia Muumba basi huleta kila jambo na wakati wake muafaka. Endelea kumcha na mambo yote yatakwenda vizuri na presha itapungua. Tuko nawe hapa kwa ushauri...