Tuesday, May 11, 2010

NIMEAMBIWA ETI NINA TYPHOID

Ukimya wangu sio bure, kulikuwa na mkono wa shetani, nimesumbuliwa na homa za usiku kwa atakribani wiki moja na juzi nilipokwenda hospitalini, na baada ya vipimo kadhaa nikaambiwa eti nina ugonjwa unaoitwa typhoid.

Unajua kuna maradhi mengine ukiyatamka kwa kiingerza yanavutia tofauti na kuyatamka kwa kiswahili. kwa mfano ni vyema kusema nina typhoid badala ya kusema nina homa ya matumbo. au ni vizuri ukisema una diarrhea badala ya tumbo la kuhara.

Vile vile ni vyema kusema unaumwa tonsils badaya ya kusema unaumwa mafindofindo, au kusema unaumwa AIDS badala ya kusema una UKIMWI.

Si mmeona majina ya maradhi yakitamkwa kwa kiingereza yanavyovutia......
ndio sababu na mie nikasema naumwa Typhoid badala ya homa ya matumbo.

Inasemekana nimekunywa maji yasiyochemshwa na ndio sababu ya kupata ugonjwa huo, ingawa nakunywa maji ya chupa sijui nayo nahitaji kuyachemsha?


Mwenzenu naumwa.......................

16 comments:

Fadhy Mtanga said...

Pole sana mchungaji. Nakuombea kupona haraka.

Ni kweli maneno ya Kiingereza yananoga kuliko ya Kiswahili?

Kwa hiyo kusema I love you inanoga kuliko kusema nakupenda.

John Mwaipopo said...

naiogopa homa ya matumbo sana kwa tabia yake ya kumtafuna mgonjwa tararibu taratibu. inawezekana mtu akagundua kwa kuchelewa kwani huambatana na magonjwa ambayo sio rahisi kudhani yanahusika na vyakula tunavyokula ama vimiminika tunavyokunywa.

typhoid sio lazima ikakupata kwa kunywa maji machafu. nasikia hata kwenye matunda ma mavijitebo kama hayakutayarishwa ipasavyo.

kuna jamaa mmoja alitahiri akiwa ana miaka 35. ili isionekane mbaya akachagua kusema amefanyiwa 'circumcision'. naam lunga ngeni hupunguza makali

Christian Bwaya said...

Pole sana. Nakutakia afya njema upone mapema, urudi kutuangazia kibarazani hapa

Anonymous said...

Utapona tu bi mdogo. Pengine ni hao watongozaji wamesababisha hii Typhoid. Hebu na wakafie mbali huko....

Mija Shija Sayi said...

Pole sana Koero, nakuombea upone haraka.

Fadhy una mambo wewe!!

Fadhy Mtanga said...

Mija nina mambo yapi jamani dada?

Kibunango said...

Pole sana, jitahidi kufuata maelekezo ya Dk ili upate nafuu ya haraka..

Yasinta Ngonyani said...

Koero mdogo wangu pole sana nakuombe upone hara . Halafu una bwebwe wewe umenifanya nicheke kweli eti maneno ya kiingereza ya maradhi yanavuti...!!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pole Koero. Utapona, tena kwa haraka (ingawa sijui Kamala atasemaje). Tunakuombea!

Mzee wa Changamoto said...

Kwani Dokta kasemaje juu ya chances za ku-die? (Najaribu kutumia maneno ya kiingereza kuona kama yatakata makali). Lol
Pole Da Mdogo.
Nakuombea as always na naamini utarejea punde.
Much Luv

mumyhery said...

Pole koero Mungu akusaidie upone upesi

Watashi Koero daiski

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

umetengeneza ajira na kudhibitisha utaalamu wa madaktari, sasa unaelewa maana ya kuumwa typhoid.

HONGERa

Anonymous said...

nakuombea upone haraka uendeleze libeneke

Godwin Habib Meghji said...

Nakumbuka ni ugonjwa uliotusumbua sana tulipokuwa sekondari ya MZUMBE. Ni muhimu kunywa dawa zote kama ulivyo andikiwa na mganga. UGUA POLE

Anonymous said...

Pole sana Koero. Godwin umenikumbusha mbali sana, nakumbuka mara moja mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Morogoro alikuja Mzumbe kujibu maswali yetu kuhusu ugonjwa Koero na lile zongwe. Basi alisema usione haya kusema unaumwa ugonjwa Koero, lakini ijulikane wazi kabisa kwamba wale wadudu wanaosababisha huo ugonjwa wanatoka kwenye kinyesi. Ndio kusema ukisema unaumwa homa ya matumbo manake umekula kinyesi hata bila kujijua.

Simon Kitururu said...

Pole Mwanakwetu POLE!

Wimbo kidogo:

Koero unaumwa?
Ndio naumwa.
Ugali utakula?
Sili naumwa.
Pure na kibulu utakula?
Sili naumwa.

Maziwa je?
Lo ntakunywa lakini bado naumwa.
Lo ntakunywa lakini bano naumwa.

Mwisho wa wimbo

Mnaukumbuka wimbo huo?