Thursday, April 29, 2010

ANAPOZUNGUMZA MWENDAWAZIMU…….

Mabinti wengi Vijijini hutumia fursa ya kwenda kisimani katika kufanya mambo yao

Kuna msemo mmoja walisema Wahenga wetu usemao, ‘anapozungumza mwendawazimu, anayesikiliza ni mtu na akili zake’

Wazee wetu wa zamani walikuwa na misemo mingi ambayo ilikuwa ikitumika katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa namna ambayo sio rahisi kumkwaza mtu.

Misemo hiyo ilitumika katika kuelimisha, kufundisha, kutoa ujumbe au kutoa tahadhari juu ya jambo fulani kulingana na suala husika. Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuelewa hadi pale atakapoelekezwa maana ya msemo huo.

Na mara nyingi misemo ya kale ilikuwa na ujumbe ambao huwezi kuupata endapo ni mvivu wa kufikiri. Inahitajika mtu awe na fikara jadidi au mwepesi wa kuchanganua mambo, vinginevyo atahangaika pasipo kupata ujumbe mahususi.

Bibi yangu ndiye mwenye jina hili la Koero naweza kumwita Ulamaa(kama wale watalamu wa mashairi) au nimwite mtu mwenye misemo mingi ya kale yenye mafunzo mengi ndani yake. Huwezi kukaa na bibi Koero kwa mazungumzo bila kukupa semi za kale ambazo aidha za mafumbo au methali. Nathubutu kumwita mkali wa tamathali za semi.

Wakati fulani nilipomtembelea kule kijijini, nakumbuka siku moja wakati tunaenda kisimani kuteka maji tuliwakuta mabinti kadhaa pale mtoni wakicheza na wavulana badala ya kuteka maji. Na hili kwa mabinti wa vijijini ni mwanya mzuri sana, na baadhi yetu unatukumbusha kisa cha Ngoswe;Penzi kitovu cha Uzembe. Tunakumbuka Ngoswe alitumia mwanya wa binti Mazoea kwenda kisimani kuteka maji ili amwage sera zake.

Sasa, Bibi yangu aliwakemea wale mabinti kwa kuwataka wateke maji na kupeleka makwao badala ya kucheza pale na wale wavulana, aliwakemea sana na kuwatahadharisha juu ya mchezo wao ule wa kukimbizana na wavulana kuwa hautakuwa na mwisho mzuri.

Lakini wale mabinti walimpuuza na kuendelea na mchezo wao huo, isipokuwa binti mmoja ambaye aliamua kuteka maji na kujitwisha na kuondoka zake akiwaacha wenzake ambao walikuwa wakimcheka, kwa kumwona muoga.

Hapo ndipo Bibi Koero akasema, “anapozungumza mwendawazimu anayesikiliza ni mtu na akili zake”. Kwa hakika ilinigusa sana, na nakiri sikumwelewa alimaanisha nini, sikuchoka kudadisi,.

Lakini baadaye tuliporudi nyumbani nilimuuliza juu ya msemo ule kwa hamasa ili nijue, huku akitabasamu alinimbia kuwa, ule msemo unaweza kuleta maana iwapo nitaugeuza kinyume chake, yaani badala ya “anapozungumza mwendwazimu anayesikiliza ni ni mtu na akili zake” utamkwe hivi “anapozungumza mtu na akili zake anayesikiliza ni mwendawazimu”. Hakika niliduwaa,nilihitaji maelezo zaidi.

Ndipo alinieleza kuwa msemo ule maana yake ulikuwa ni kufikisha ujumbe kwa namna ambayo haitawakera watu, kwa maana ya kuwaita wendawazimu bali kufikisha ujumbe kuwa mara nyingi watu na akili zao wanapozungumza ni vigumu sana watu kuwaelewa na ndio maana wanadharauliwa na kupuuzwa, mpaka kitambo kidogo ndipo watu wanapong’amua ukweli wa yale yaliyozungumzwa.

Maneno hayo yalinikumbusha gwiji wa sayansi Galileo Galilei ambaye alisema kuwa dunia hii haiko kama meza, kama watu wa enzi hizo walivyokuwa wameaminishwa. Bali dunia ni duara na inazunguka katika mhimili wake na kulizunguka jua, ndiyo maana tunapata usiku na mchana, lakini mwanasayansi huyo alipingwa vikali na watu akiwemo mfalme, ikabidi ajinyamazie.

Baada ya miaka kadhaa tangu atoe kauli ile, ilikuja kudhihirika kuwa utafiti wake ulikuwa ni sahihi. Na hapo ndipo msemo huo unapokuwa na maana kama ukiuzungumza kwa kinyume chake.

Kwa mfano yule binti kule mtoni ambaye alimsikiliza bibi Koero na kuamua kuteka maji na kuondoka huku akiwaacha wenzie wakimcheka, Je ni nani mjinga kati yake na wale wenzie? Kama bibi koero alikuwa ni mwendawazimu basi ni Yule binti pekee aliyekuwa na akili zake aliyeelewa na kufuata malekezo ya bibi Koero, na kuwaacha wnzie ambao walimuona bibi Koero kama ni mwendawazimu, wakati wao ndio wendawazimu kwa kushindwa kuelewa kile alichosema.

Nimekumbuka msemo huu baada ya kupitia blog kadhaa siku ya leo na kukutana na habari chungu mzima ambazo zimekuwa kama zimebeba fikra za mwendawazimu. Tumekuwa tukiandika mambo mengi sana tukijaribu kugusa kila nyanja katika jamii yetu lakini kumekuwa na watu wachache wenye akili zao ambao ndio walioweza kusikiliza na kuelewa na wengine kutoa maoni yao.

Kuna siku niliwahi kuweka porojo zangu hapa ambazo zilikuwa ni fikra zangu tu za kiwendawazimu lakini si haba niliwapata watu kadhaa wenye akili zao ambao walimudu kusoma ujinga wangu na kutoa maoni yao.

Miongoni mwao kuna maoni ya msomaji mmoja ambaye hakutaka kuweka utambulisho wake bayana, ambaye na yeye aliweka fikra zake za kiwendawazimu katika mada hiyo, ambapo nilivutiwa sana na mchango wake. Naomba uungane nami kwa kusoma maoni yake kama ifuatavyo hapo chini:

"Dada Koero, leo ni siku ya kwanza kukutembelea humu. Nimeipenda sana blog yako. Nimeona umeandika sana kuhusu madhira ya mama zetu. Dada Koero mimi nakuunga mkono, maana I have lived this life. So I know it. Swali langu kwako na wanawake wengine ni hili: Je ni kipi kifanyike KUPUNGUZA maana KUONDOA hii hali ni vigumu. Inaonekana wengi tunaliona tatizo na tumeishi na haya matatizo, lakini wote tunasema ni serikali ndo yenye jukumu! Mi nadhani we should be the change we seek!Tuanze na jukumu la kuchagua viongozi responsible na tuwawajibishe. Leo hii CCM akijua kwamba hana majority bungeni ya kupitisha sheria anazozitaka kwa manufaa yake......trust me ..atakuwa na adabu jinsi anavyotuongoza, perhaps hela za ufisadi angeziweka kwenye mipango ya kuwawezesha na si kuwasaidia hawa akina mama na wananchi kwa ujumla....Tatizo kubwa kwetu sisi waafrika popote tulipo...tunapenda kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu. Ukiangalia kwa kiundani..hawa hawa unaowaonea huruma..ndo kesho utakuta wanaandamana kuipigia kura CCM! Sasa jamani..hivi mnategemea ukombozi wa mwafrika utatoka wapi? Mwenyezi MUNGU ALITUPA UTASHI lakini tunashindwa kuutumia. Do you really think Kikwete gives a damn to a dying villager down in Kwimba au Kigoma? only when he needs their votes!Hapa tutakuja na excuse kibao..kwamba watu tunachagua viongozi wabovu kwa sababu ya umasikini, lakini tunashindwa kugundua kwamba..Politics is everything! whether you are in America or in poverty stricken Tanzania.

Narudia tena, waafrika..viongozi wetu wanatuchukulia for granted. Na sisi tumeridhika na hii hali.Na sisi tumekubali.. Hata the so called "elites"..ndo wanatuangusha..maana wakisha "toka" imetoka hiyo.....Hawaangalii nyuma....zaidi ya "kuwaonea huruma" waliobaki huko nyuma...My take: Watanzania tuamke, tuchukue jukumu la maisha yetu. Tuache kumsingizia Mungu wala mwingine. HAITUSAIDII KULAUMU. Dada Koero, Trust me..leo hata ungeteua 70% ya wabunge wote wakawa wanawake...hali za mama zetu hazitabadilika! Tunahitaji kubadilisha mfumo wa jinsi tunavyojitawala au tunavyotawaliwa. Imagine...mpaka leo hatuna umeme wa kuaminika..lakini hebu jiulize..tangu JK aingie madarakani..tumelipa mabilion mangapi kwa makampuni ya umeme hewa? and guess what? Everybody is quite! and in October we will vote in masses for the same messy!Ofcourse, CCM siyo tatizo letu pekee..lakini..wakijua kwamba hata wananchi wanafikiria..hali itabadilika. For now..they know..they can do anything and go away with it. Mimi kiukweli...I get the feeling labda..ngoja umasikini uzidi kutuchapa weeeee (zaidi ya huu tulionao sijui itakuwaje ;-)...labda iko siku tutaamka na kuona kwamba we can influence things through the ballot!Waungwana naomba nisiwachoshe..lakini..mimi kiukweli nchi yangu na wananchi wenzangu wananisikitisha sana...Tunashindwa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa yetu na watoto wetu. Umasikini na hali ngumu zinazowakabili mama na baba zetu utaendelea kudumu daima. Mpaka tutakapoamka na kusema INATOSHA!"
(Mwisho wa maoni yake)………..
Fikra za kiwendawazimu za msomaji huyu zilinivutia sana nikaona si vibaya nikiwashirikisha watu kadhaa wenye akili zao kutafakari kile alichokisema mwenzetu.

Kuna jambo moja ninajiuliza, hivi vyombo vyetu vya habari hususan magazeti na Redio haviwezi kweli kutengeneza vipindi hata vya nusu saa kusoma ujinga wetu huu katika blog zetu hizi?

Kusema kweli kuna ujinga mwingi sana unaoandikwa katika blog zetu hizi ambapo kama ungapewa nafasi katika vyombo vyetu vya habari vya magazeti na redio kwa kuwa vinawafikia wananchi wengi hapa nchini ukilinganisha na blog, naamini idadi ya watu wenye akili zao ambao ndio wanaoweza kuelewa kilichojificha ndani ya ujinga wetu huo ingeongezeka.

Hebu wewe unayesoma hapa, jaribu kumtembelea mzee wa changamoto Mubelwa Bandio kwa kubofya hapa usome ujinga wake au mzee wa Jielewa Christian Bwaya kwa kubofya hapa, pia ni vyema kusoma maisha na mafanikio kwa kumsoma dada Yasinta Ngonyani na ujinga wake kwa kubofya
hapa.

Nachelea kusahau ujinga wa Profesa Mbele ambapo unaweza kubofya hapa kumsoma, bila kumsahau kaka yangu Profresa Matondo naye kila kukicha hachoki kuandika fikra zake za kiwendawazimu kwa kutulisha chakula kichungu na kitamu ambapo ukipenda kukila waweza kubofya hapa.

Naogopa kupigwa mapanga shaaaaa na Chacha o'Wambura Ng'wanambiti kwa kusahau kuwakumbusha wasomaji kusoma ujinga wake na uwendawazimu wake kwa kubofya hapa, …Heeee nisimsahau mzee wa mitini, tena huyu kama hayuko mirembe ni bahati maana hata simuoni mjini siku hizi, naambiwa amekimbilia Karagwe baada ya kufulia na akiwa kule anaendeleza libeneka kwa kuandika ujinga wake kwenye kijiwe chake cha nyegerage, huyu ni Kamala, hebu bofya hapa kumsoma pia.

Kaka yangu wa kulikoni ughaibuni Evarist Chahali na yeye upuuzi wake upo hapa, kaka yangu Malkiory wa kule Ufini na yeye hayuko nyuma katika kuandika ujinga wake na kuweka hapa, kuna ndugu yangu mmoja siku hizi na yeye anajifanya kichaa kabisa, Fadhy Mtanga, yeye ameamua kuimba na mashairi ya ndoto za alinacha na kuyaweka hapa.

Mfumwa Kitururu, naambiwa karudi Bongo kimya kimya na kajichimbia Morogoro akitafakari juu ya namna ya kuendeleza stihizai zake pale mawazoni na kutufikirisha kwa lugha zake zilizojaa utata mtupu unaweza kubofya hapa kumsoma.

Kuna bwana mmoja mie napenda kumwita Mcharuko, maana kadata mpaka ameamua kutengeneza kurasa mbili ili kuendeleza libeneke la kuandika ujinga wake, huyu sio mwingine ni mzee wa Nyasa Markus Mpangala aka Paroko aliyestaafishwa kwa manufaa ya kanisa, ujinga wake uko
hapa
Ninaye dada yangu mpendwa, huyu alinibatiza jina la Binti Kipaji, sina uhakika kama nastahili jina hili, lakini kwa kuwa yeye ameona na kwa vigezo vyake ameniona nastahili, nasema shukrani dada yangu. Huyu ni dada Mija Sayi nasikia ni dada yake Profesa Matondo, na yeye anaandika ujanja wake hapa. Nisimsahau mdogo wangu my Little world, Faith Hillary, akiwa kule ughaibuni hachoki kuandika ujinga wake na kuuaweka hapa. Na pia nisingependa kumsahau kaka Jacob Malihoja, na mbwembwe zake katika kibaraza chake unaweza kubofya hapa kumsoma. Na kaka yangu kwa mama mwingine Ramadhani Msangi yeye anaweka ujinga wake hapa. Hupo kaka yangu mwenye Utambuzi na anayejitambua, yeye huwa anatushangaza katika kibaraza chake, unaweza kubofya hapa kumsoma. Yupo pia dada yangu Subi, mie wakati mwingine humwita Passions, naye mara nyingi anatufikirisha kwa tamathali zake za kiwendawazimu kupitia kibaraza chake kilichopo hapa

Kwa kweli, kuna wadau wengi katika tasnia hii ya blog ambao wanaandika ujinga wao lakini imekuwa kama kelele za mwana mpotevu nyikani. Kama kungekuwa na ushirikiano wa vyombo vya habari nilivyovitaja hapo juu kuchukua uamuzi wa kupitia blog hizi kwa minajili ya kuwafikishia Watanzania kile tuandikacho ingesaidia sana kuelimisha jamii kwa kiasi kikubwa.

Tujiulize mbona CNN ilifanikiwa sana kutumia blog kupata habari za chaguzi za Iran, Kenya na Zimbabwe kama njia mbadala ya kupata maarifa na habari anuwai? Huo ni mfano tu. Tunahitaji ushirikiano huu kwa vyombo vya habari kwa sababu wote tunajenga nyumba moja ambayo ni Tanzania, hatuna sababu ya kunyimana fito.

Naomba kuwasilisha

12 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Mpaka kieleweke! ALUTA KONTINYUA :-)

Yasinta Ngonyani said...

Koero mdogo wangu hapa yaani umenikumbusha mengi kweli. Nakumbuka ilikuwa ni kijijini kingoli unaambiwa unachotelea maji mpaka mtungi uje basi hapo unaona ndo umepata nafasi ya kucheza maana ukienda huko kisimani ndo basi mpaka atumwe kaka mmoja kuja kukuchukua. Jamani maisha ya zamani na ya kijijini....we acha tu. Ahsante kwa kumbukumbu bibi yetu Koero.

Anonymous said...

You are trying TOO HARD....

Markus Mpangala. said...

Paroko aka Mcharuko bin kadata.
Ipo kazi ama kweli tunaweza kuwa KAMUSI ELEZO na kundika mengi zaidi. Tutasonga kwa mwendo wa karatasi au kinyonga.

Pumzika na Dr. Dre katika STILL DRE, midundo mitamu hii. Halafu andaa mada huku unamsikiliza

Mzee wa Changamoto said...

At least SHE IS TRYING (according to you Anon)
Ungejua THAMANI HALISI ya kuandaa alichoandaa, ungetafakari ulichoandika

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto. I didn't mean anything offensive but if you read her article, it is obvious that she is trying too hard. Sasa wewe unakurupuka kum-defend. Why? Do you know her? Is she your ex???

This is the problem with you TZ bloggers. You don't tolerate any opposing views. If what you are writing is intended to be DOGMA and never be questioned, then there is no point of even having these stupid blogs of yours. You make me very sad when you do this. That is why I will just stick with Jamii Forums and Wanabidii where free speech is acknowledged na siyo nyie marastafari FEKI...Everyday Luciano said this, Lucky Dube said this...Bullshit. These were drug addicts and why do you keep on quoting dem zombies? Did they even know what they were talking about???

This is the last time that I will vizit a Tanzanian blog - with an exception of Professor Joseph Mbele, Kamala Luta, Matondo Mzuzulimwa and Kaluse who doesn't mind to be questiond. May be you should change your blog to "The way I see your opposing views is the problem"

Mzee wa Changamoto said...

Well!! Anon
I guess you're on the same page as us. Kwamba UNAPINGA SISI KUTOTAKA KUELEZWA UKWELI WAKATI WEWE MWNYEWE HUTAKI KUELEZWA UKWELI. That's wonderful.
Kumbe nawe unapinga unalotenda? Kama hudhani kuwa kukosolewa ni kosa nawe ungenikosoa niliyosema nami nikakukosoa kwa uliyosema na hakuna shaka kuwa kuna wakati mwenye kusimama katika FIKRA ZA KWELI ATAKUWA MUELIMISHAJI KWA WENZAKE (si lazima anayekosoana naye). Sio kufanya ulivyofanya kwa kususa kwenda mahali ambapo hujakaribishwa na kutokuwepo kwako hakutapunguza lolote kwani wewe unakuwa mmoja wa MNAOKIMBIA UKWELI.
Nakwambia wewe si wa kwanza na hautakuwa wa mwisho
Sasa wewe unayepinga suala la kukosolewa unasema hutatembelea blog ambazo UKIKOSOA NAWE WAKOSOLEWA.
Kama ningekuwa naogopa kukosolewa ningekuwa nina-moderate maoni kwenye blog yangu na sifanyi hivyo kwa kuwa ukiandika FIKRA ZAKO nami NTAANDIKA ZANGU.
Najua unajidanganya kusema hutatembelea blog hizi kwani natambua fika kuwa utarejea hapa kusoma nililokujibu.
Kuhusu Lucky Dube, Luciano, Bob, Bushman, Burning Spear na yeyote yule nimsikilizaye na kuandika juu yake sitaacha. Nitafanya hivyo kwa kuwa wewe unayewaona kuwa si watu wema ndiye uonaye na si mimi. Na siamini kuwa mimi ni mtu mwema pia, bali najua wewe, wao na mimi sote tuna wema.
Kauli yako kuwa "you are trying too hard" inajieleza vipi? Inakosoa, inavunja moyo, inarekebisha, inaonya ama?
Labda ungeandika kwa ufafanuzi zaidi ingesaidia. Na ndio maana nikasema kuwa "at least she is trying" kwa kuwa nami najua inachukua muda gani kuandika post kama hii na kubwa ambalo ningefanya (na ambalo nimeshafanya mara nyingi) ni kueleza kile ninachoamini hakiko sahihi katika alichoandika na sio kutothamini kila kitu (ikiwa ni pamoja na muda wake)
Tutakutana hukohuko kwa Profesa Mbele, Profesa Matondo, Kaka Kamala, Kaka Kaluse na wengine ambao utawatembelea (nami nawatembelea pia) na nakuhakikishia kuwa huko utapata uelimishaji tosha (kama nipatavyo mimi) na kwa kuwa hata sehemu ya post zangu huwanukuu hao.
Siko pale KUTAFUTA WATEMBELEAJI (hasa wasiojitambulisha) na nitaendelea kutimiza ninalotimiza. Nakurejesha kulekuleeee ulikokataa kwa Bob kuwa "Dready got a job to do
And he's got to fulfill that mission
To see his hurt is their greatest ambition, yeah!
But-a we will survive in this world of competition,
'Cause no matter what they do
Natty keep on comin'through,
And no matter what they say,
Natty de deh every day."

Jina la blog litabaki kuwa hivyo lilivyo na wewe kuliona visivyo NDIO TATIZO.
Hahahahahaaaaaaaaaaaaa
Good luck

Anonymous said...

we anon 8:53AM, siku ingine usidandie treni kwa mbele.waulize walokole wa blogu ya gospo walivochemka hapo. kwani kumtetea mtu ndo kawa ex wako? mijitu mingine bana

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kamjadala kazuri haka; na kama kawaida mada imeachwa na tumeanza kushambuliana sisi kwa sisi. Jibu zuri Mzee wa Changamoto.

Ma-anony. hawa hawaishi kuzichangamsha blogu zetu. Wapo wanaotoa maoni ya kina sana, wapo wanaorusha madongo tu, wapo wafurahishaji. Ni watu wa muhimu sana katika uhai wa blogu zetu.

Sote lengo letu ni moja, tuvumilianeni na kujaribu kuona wema hata katika baya lisemwalo.

Kabla sijaanza kublogu nilikuwa nachemka kweli mtu akinirushia dongo na pale mwanzoni kabisa kabla sijamwelewa Kamala nilijaribu hata kupambana naye. Kwa sasa blogu imeniimarisha sana na nimejifunza kwamba kimsingi madongo ni ya lazima na wapiga madongo pengine wanaweza kutuimarisha. Tusongeni mbele.

Nilishawahi kuligusia jambo hili hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/04/fikra-ya-ijumaa-wanablogu-tusiwe-na.html

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Ukiwa mwanablog huwezi kupata BP kabsaa!

Unless sasa una tatizo lingine

Fadhy Mtanga said...

....sijui nilichelewea wapi? Haka kamjadala kamenivutia kweli.
Ma-anon endeleeni tu...nasi tunaendelea na libeneke..

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___