Saturday, April 17, 2010

TAFAKARI YA LEO: IMANI INA NGUVU KIASI GANI?

Nikiyagusa mavazi yake tu nitapona

Tafakari ya leo tuangalie mfano huu wa imani kwa kusoma habari hii ya mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu, katika kitabu cha Marko 5:25-34.

Nitanukuu kutoka katika Biblia Takatifu:


“Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na mbili na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa na vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya. Aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka , naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa , nawe wasema , Ni nani aliyenigusa? Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo, Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.”

Huyu mwanamke alikuwa na hili tatizo kwa miaka 12, ambayo kwa kweli ni miaka mingi sana kuishi na ugonjwa. Na alijaribu kila njia, akitafuta tiba lakini hakuweza kupona.

Hata hivyo kitu kimoja kilichonivutia ni kwamba, pamoja na kuhangaika kwa miaka yote hiyo akitafuta tiba lakini hakukata tamaa, na baada ya kusikia habari za Yesu akaona ni vyema ajaribu huenda atapona, na hakika kutokana na imani aliyokuwa nayo akapona. Bwana yesu asifiwe!

Watu wengi wanadhani kuwa imani ni kama mazingaombwe kwamba unaamini tu halafu imani yako inakuletea kila kitu unachohitaji mikononi mwako .
Hii haiwezekani. Iwapo fikra hasi, au matamshi yako ni ya kukata tamaa na hujiamini, imani haiwezi kufanya kazi kwa mtu wa namna hiyo.

Kwa nini?

Ni kwa sababu Imani sio kitu kinachofanya kazi papo kwa hapo, bali inahitaji mchakato fulani huku ikirutubishwa na fikra chanya.

Ili imani iweze kufanya kazi ni lazima ipitie katika mchakato ufuatao ndio ufanye kazi:


Uamuzi: Kumbuka kwamba huyu mwanamke alikuwa amejaribu tiba kadhaa wakiwemo madaktari bingwa na maarufu, hakuweza kupona, lakini aliposikia habari za Yesu akafanya uamuzi katika moyo wake kwamba kupitia Yesu Kristo atapona. Huo ni mchakato wake wa kwanza kabisa kuelekea katika kupona.

Imani: katika Marko 5:28 yule mwanamke alisema “Nikiyagusa mavazi yake tu nitapona” Ile kauli ya kusema “Nitapona” ni kauli chanya na yenye nguvu na kama tulivyoona kuwa inatoka kwa mwanamke ambaye alikuwa amejaribu tiba kadhaa kwa miaka 12 bila kupona.
Ni katika Matayo 9:20:22 tunaposoma kuwa alijisemea kauli hiyo kutoka moyoni mwake. Hapo ndipo tunapoona kuwa ni kwa jinsi gani imani inavyokuwa na nguvu hata kwa kujisemea moyoni tu, inatosha kufanya jambo liwe.

Kutenda: Katika Marko 5:27, tunasoma kuhusu, mwanamke huyo Alivyopenya katika kundi la watu na kwenda kugusa mavazi ya Yesu Kristo.
Ni kitu gani kilimsukuma hadi akaamua kujipenyeza katikati ya kundi la watu ili tu kugusa mavazi ya Yesu?
Ni kwa sababu aliamini neno la mungu na ndio sababu ya yeye kuchukuwa uamuzi.
Kutenda kile unachokiamini ndio njia sahihi ya wewe kuelekea katika kufanikiwa, haitakiwi kusema tu, hiyo haitoshi.

Ili imani iweze kufanya kazi ni lazima upitie katika mchakato huo ndipo imani iweze kufanya kazi.


Tukutane Jumamosi ijayo.........

10 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Koero; leo siendi kanisani. Hii inatosha. Ngoja nikaimarishe imani yangu. Ubarikiwe!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

pia kuna sehemu wanaambiwa mgekuwa na ibani kidogo tu kama punje ya hadarali mge.........( )

kwamba punje ndogo ingekuwa kuubwa kinoma. imani ni muhimu na inamat sana katika maisha yetu yoote ya kila siku

imani inanguvu kushinda nguvu zozote zile za dunia hiii

imani ni muhimu sana na kila tunachohitaji tutakipata. tunahitaji kujisafisha na kuondoa nguvu hasi na mawazo mabaya akili mwetu kwa tafakuri ya kina zaidi (meditation)

sisi na uumbaji ni kitu kimoja na hivyo imani ni muhimu

ila yabidi uamni na sio uaminishwe kama ilivyo, ....biblia takatifuuuuuu...... labda ila binadamu ni mtakatifu zaid ya yote hayo

IMANI, UPENDO ni muhimu

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Matondo: Nakuhitaji kanisani kwanza leo kama paroko wako...lol

manyimbo yanaimbwa, mapambio nk kuwa imani imekwisha.

Waraka huu unatutaka tuamshe imani ilolala sasa na kuishi kiimani zaidi kwa kuwa ni katika kuiishi imani yetu mambo yote yatakwenda tunavyotaka yawe

Blessings!

Mzee wa Changamoto said...

Kama nitatakiwa kuufupish ujumbe huukwa maneno matatu matatu ningesma WAKE UP CALL.
Nilichopenda hapa ni namna ulivyohusisha IMANI yako na MAISHA ya kila siku na namna ambavyo IMANI uizungumzia inavyohitaji IMANI ya kweli kutuwezesha kuishi vema.
Hakuna kitu chema kama kuwa na mtazamo chanya.
Na kujua kuwa kila kitokeacho kina sababu na pia kina mwisho (kama alivyoamini mwanamke huyo) ni IMANI kuubwa ambayo tukiishika itatusaidia.
Nakumbuka Luciano aliimba katika wimbo wake HAVE FAITH akisema "why should you worry when you can pray? Why complain and it is such a lovely day? Why should you cry and pass your time away? When GOD has blessed you abandontly with lots of strength and energy. Why lament it's not necessary. BE WISE AND SING. You can move any mountain (with faith), you'll have a blessing like a fountain (with faith), you will never be forsaken (have faith)
APENDAYE KUUSIKILIZA NA AFUATE LINK HII
http://www.archive.org/details/HaveFaith

BLESSINGS

Yasinta Ngonyani said...

Ubarikiwe sana Da mdogo!! Asante kwa neno hili la leo.

Jacob Malihoja said...

Na kwa neno la leo tuwaombee wenzetu wa Ulaya, Yasinta na ndugu wote walioko huko na wenyeji wao, wasalimike na Mavolcano, hali ya usafiri irudi kama kawaida na kusiwe na madhara kiafya. maana kule kulivyo ndege ndio Ngorika zao!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ng'wanambiti - Najua unachokitaka. Sadaka!

Markus Mpangala said...

AMINA UBARIKIWE

Anonymous said...

Amina Koero. Tunashukuru kwa ujumbe hu. uliyesema tuombee waliopo Ulaya "Waulaya" ni kweli kabisa ndugu yangu. Maana kuna nchi kama Ufaransa, ndege hazisafiri na watu wa treni wapo kwenye mgomo hivyo sasa hivi ni mwendo wa bus kwa umbali mrefu sana.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___