Friday, April 9, 2010

ASILIMIA 90 YA UCHUMI WA TANZANIA INAMILIKIWA NA WAGENI!

Tumebaki kuwa wachuuzi tu.

ZAIDI ya asilimia 90 ya uchumi wa Tanzania unaendelea kumilikiwa watu wenye asili ya Asia na Ulaya, takwimu zinaonyesha.

Takwimu hizo zimetolewa huku kukiwa na kilio kikubwa cha Watanzania wazawa, kutaka wajengewe mazingira mazuri ya uwezeshaji ili kumiliki uchumi wa nchi kupitia migodi mikubwa ya madini na maeneo nyeti ya kiuchumi.

Lakini wakati kilio hicho kikiwa hakijapata ufumbuzi, Taarifa ya Utendaji ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, iliyowasilishwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi jana, ilisema watu wenye asili ya mabara ya nje wanaomiliki uchumi wa Tanzania ni sawa na asilimia moja ya Watanzania.

Takwimu hizo zilifafanua kwamba, asilimia hiyo 90 ya uchumi wa nchi umeshikwa na watu wenye asili ya Asia na Ulaya, wakati asilimia 99 ya Watanzania wazawa, hawana kitu.
Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizowasilishwa katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yusuph Mzee, tatizo la Watanzania weupe kumiliki uchumi, lilianza tangu wakati wa ukoloni.

"Wakati wa enzi za ukoloni na hata baada ya uhuru Watanzania wengi hawakuwa wakishiriki kikamilifu katika kumiliki uchumi wa nchi yao. Uchumi wa nchi umeendelea kutawaliwa na wageni wakishirikiana na Watanzania wachache," inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inasema "asilimia 99 ya wananchi ni Watanzania weusi na asilimia 1 iliyobaki inajumuisha Waasia na Wazungu ambao wana miliki zaidi ya asilimia 90 ya uchumi wa nchi hii (Msambichaka, 2008).

"Hii ina maana asilimia 99 ya Watanzania halisi wanamiliki asilimia 10 tu ya uchumi wa taifa lao," inasisitiza ripoti.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kurekebisha kasoro zilizoko, ikiwa ni pamoja na kuanzisha (lililokuwa) Azimio la Arusha, Vijiji vya Ujamaa, Elimu ya Kujitegemea, Serikali za Mitaa, Vyama vya Ushirika, Sera ya Uwekezaji na Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.
Inasema hata hivyo,juhudi hizo hazijazaa matunda yaliyotarajiwa na kwamba na kwamba kushindikana kwa juhudi za kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao, ndilo chimbuko la kubuniwa kwa mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi, katika ilani ya CCM ya mwaka 2000."

Habari hii imendikwa katika Gazeti la Mwananchi la tarehe 8/4/2010 na mwandishi Ramadhan Semtawa, nami nimeona niiweke hapa ili tujadili kwa pamoja.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu " Takwimu hizo zilifafanua kwamba, asilimia hiyo 90 ya uchumi wa nchi umeshikwa na watu wenye asili ya Asia na Ulaya, wakati asilimia 99 ya Watanzania wazawa, hawana kitu. mwisho wa kunukuu Hivi ni raha gani tunaona sisi Watanzania au ni upole tulio nao?

Godwin Habib Meghji said...

HAKUNA MTANZANIA ALIYEZUIWA KUSHIRIKI NA KUMILIKI UCHUMI WA TANZANIA. mashirika ya umma yote tumeyaua wenyewe kwa UBINAFSI. Sasa tunalalamika nini?

WATANZANIA WENYE ASILI YA ASIA NAO WAMEWEKWA WAPI? Nasikitika watanzania wengi wanawaona Watanzania wenzao wenye asili ya asia sio WAZAWA. Binafsi naona watanzania wenye asili ya kiasia wanajitahidi sana katika kuendesha biashara zao na kushiriki moja kwa moja katika uchumi wa nchi yetu

TUNAHITAJI KUKODISHA PIA BARAZA LA MAWAZIRI KUTOKA NJE, NA VIONGOZI WA JUU KWENYE LOCAL GOVERNMENT ZETU ILI TUWEZE KUPIGA HATUA
Nusu karne toka tupate uhuru viongozi wetu wamefanya nini?....

Anonymous said...

Hapa naona tatizo kubwa ni sisi wananchi kuwa na hii mentality ya "serikali itafanya hiki au kile". I for one, naamini kabisa kwamba jukumu la serikali ni kuweka mazingira thabiti "fair playing field" kusudi wananchi tuhangaike na kufanikiwa. Siamini kwamba serikali itatuletea maendeleo. Bali naamini inaweza kujenga mazingira tukajitafutia maendeleo. Mfano kama una bishara zako..kuwe na mfumo mzuri wa kodi..usibambikiwe kodi na tax man kwa kuonewa.., umeme wa kutegemewa uwepo..ingawa sisi tutaulipia..huduma za maji zipatikane..sisi tuzilipie..thats the role of government..(as far as I am concerned). We dont want free goodies! tunataka huduma.....

Lakini je, tufanye nini kama serikali haiwezi kujenga hayo mazingira? Mfano ukiangalia ubinafsishaji umefanyika tz..lakini mashirika yote yaliuzwa kwa bei ya kutupwa na wakubwa wakauziana. LAKINI sisi wananchi tulifanya nini? Did we PUNISH the government for that? No..infact we are waiting to vote for the same people come November.

What I see: Swala siyo ubepari wala ujamaa wala mfumo mwingine. Swala ni sisi wananchi kuamka na kujua what is at stake. Tujue daima kwamba bila kuwa vigilant serikali will never do anything, as long as they enjoy our hard earned taxes while sending their kids and cronyies to Europe and their wives to London for shopping.

Mapinduzi yoyote ya kweli, yanaletwa na wananchi. Wakinyanyasika wakaona wamechoka, basi hapo ndo wataamka. Something I dont see in my motherland here.

Tunaweza kuwasingizia wahindi/wageni wengine..lakini ultimately..nani anawapa hizo fursa? nani anawasaidia kukwepa kodi? nani anawauzia mashirika kwa bei chee? You and I we know the answer. The million dollar question is: You and I, knowing all that we know, what have we done?

If Kikwete, promised to loot out corruption, and improve standards of living...what happens when he does neither? Do we follow up and punish him for that? You and I know the answer.

I argue my fellow country women and men, we should aspire to build the country we dream. Wherever you go, citizens always determine their fate.

Mpaka kesho kutwa, naamini tatizo kubwa/mama la Tanzania ni failure of governance na wananchi kutowajibika. Na Si kwamba Kikwete ni kiongozi mbovu, no, ni kwa sababu sisi tuliomchagua ndo wabovu. Maana we dont follow up to ask him whther he fullfilled what we sent him to do. Mfano, ukiwa na kibarua umemtuma shambani. Ni wajibu wako wewe tajiri uende ukague shamba kama kibarua kafanya vyema. Kusudi either..umnyime ujira mpaka arudie kazi, umpe malipo pungufu, au umlipe mshahara wake.

So..tatizo si wahindi au wazungu walioshikiria migodi yetu kule Geita. Ni sisi. Especially mimi na wewe! Maisha mazuri/maendeleo siyo mana itakayotoka mbinguni. Lazima vifanyiwe kazi. SOMETHING WE AINT DOING.

Make no mistake, hizo takwimu..kwanza nadhani haziko sahihi...we aint got nothing we the people of this country. Tanzania sisi ni masikini beyond recognition..but perhaps..we need to suffer than we have suffered. Who knws?

Masanja

MARKUS MPANGALA said...

UMENIWAHI HII HABARI, NILIKUWA KWENYE KA OFISI KANGU NIKIANDIKA MUSWADA WA MAKALA KUHUSIANA NA HII KITU.Yaani sasa hivi nimefungua tarakilishi hii nakutkana na mada ambayo nimeaanda hoja zangu kuhusiana nalo.

Haya, siyo vibaya mimi nimetosheka na maoni ya wengine ni mazuri

Mzee wa Changamoto said...

Sijui kilio chaandikwaje. Ndio maana siandiki

Mzee wa Changamoto said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

tanzania ni nchi inayoendelea na inaendelea kwa haraka sana sasa tunaifungua kwa wazalendo majirani ili ngozi nyeusi yenye utajiri wa asili ipate kuongeza na kupandisha asilimia ya maoni yako