Saturday, April 3, 2010

WAMALAWI NA NDOA ZA VIBINTI!

Mmoja wa wa waathirika wa ndoa hizo

Binti huyu naye ni miongoni mwa waathirika wa ndoa hizi za vibinti

Huyu sio babu na mjukuu wake bali ni mtu na mkewe

“Baba yangu wa kambo aliniamuru niache shule ili niolewe na mzee wa umri wa miaka 77, kwa madai kuwa umri wangu ni mkubwa ukilinganisha na darasa ninalosoma, kwani wakati huo ndio nilikuwa niko darasa la nne. Nilimkatalia na kumweleza wazi kuwa ningependa kuendelea na masomo”. Hivyo ndivyo alivyoanza simulizi yake binti huyu Balita Simpokolwe.

lakini hata hivyo kukataa kwake hakukuweza kumsaidia.

Kwani baba yake alianza kumtuma sokoni kuchukua fedha kwa mtu mmoja mzee hivi, ambaye alikuwa hamfahamu, ambapo alikuwa akipewa kiasi cha kati ya dola 5 mpaka 10, kiasi ambacho alitakiwa anunulie chakula na kiasi kinachobaki alikuwa kimpa baba yake huyo wa kambo.

Balita anakiri kwamba hakuweza kuhisi jambo lolole kuhusiana na zile pesa alizokuwa akipewa na yule mzee kwa kuwa aliamini kuwa yule alikuwa ni rafiki wa karibu wa baba yake wa kambo. Lakini wiki tatu baadae tangu awe anakwenda kuchukua fedha kwa mzee yule, alishangaa kumuona akija nyumbani kwao na jembe dogo la kulimia bustani. ( kwa mila za watu waishio Malawi Kaskazini hususan katika wilaya ya Nsanje jembe dogo la kulimia bustani inatumika kama ishara ya mahari)

“Nilishtuka sana, baada ya baba yangu wa kambo kunitaka nipokee jembe lile la bustani kutoka kwa yule mzee.(Kwa mila zao, binti kupokea jembe kutoka kwa mwanaume ni ishara kuwa amekubali kuolewa na mume huyo). Lakini huku nikiwa imechanganyikiwa, nilikataa kupokea jembe lile.”

Hata hivo mama yake aliungana naye kupinga binti huyo kuolewa kwa kuwa bado alikuwa ni mdogo, “baba yangu wa kambo alikuja juu akidai kuwa atampa talaka mama yangu iwapo atapinga mimi kuolewa na mzee huyo, na cha kusikitisha zaidi alidai kuwa haiwezekani nisiolewe na mzee huyo kwa kuwa tumeshakula fedha zake.” Alisema bintin huyo kwa masikitiko.

Hivyo alilazimishwa kuolewa na mzee huyo, lakini baada ya wiki mbili tangu aolewe kikundi kimoja cha kutetea unyanyasaji wa wanawake na watoto kiitwacho Chitipa Women’s Forum kilimuokoa kutoka katika ndoa hiyo baada ya kuwashwishi wazazi wa binti huyo wamrejeshe shuleni.

Belita Simpokolwe, sasa anaishi na mmoja wa baba zake wadogo, amefurahi sana baada ya kurejea shule kuendelea na masomo yake. Tukio hili ambalo lilimpata Belita Disemba mwaka 2008 lilimuacha akiwa na amesathirika kisaikolojia.

Kwa mujibu wa mwalimu anayemfundisha alikiri kuwa kuna wakati alikuwa anashindwa kuzingatia masomo yake pale kumbukumbu za tukio lile la kutolewa shuleni na kuozeshwa kwa nguvu linapomjia, lakini binti huyo ambaye alikuwa na miaka 13 wakati huo akiozeshwa, amemudu kuendelea na masomo yake ambapo anataka kutimiza ndoto zake za kuwa muuguzi hapo atakapomaliza masomo.

“Kinachoniuma ni kwamba nimekuwa ni muathirika wa ndoa ya utotoni baada ya wale niliowaamini kuwa watanitunza na kunilinda kunitoa kafara kiasi cha kutaka nisitimize ndoto yangu” alisema binti huyo aliyekuwa akisoma shule ya msingi Kawale kaskazini mwa Malawi, akiwa yuko darasa la sita wakati huo.

Belita ni mmoja kati yan mabinti walioathiriwa na mila marufu kama Kupimbira, ambapo mabinti hulazimishwa kuacha shule na kuozeshwa kwa wazee ili kujipatia mahari, na hii hufanyika bila hata ya binti kufahamishwa.

Wakati mwingine wazazi hulazimika kuwaozesha mabinti zao ili kulipa madeni.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na tasisi ya Chipita Women’s Forum inaonyesha kwamba ,taktibani asilimia 17 ya mabinti huachishwa shule na kuozeshwa kwa wazee, huku wengine wakilazimika kuacha shule wenyewe kutokana na unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na waalimu wa kiume na wanaume wakware wenye uchu wa kufanya mapenzi na vibinti.

Akizungumzia mila zinazotumika kuwakandamiza watoto wa kike na kuwakatisha shule Mwenyekiti wa Chipita Women’s Forum, Bi Ruth Mbale alizitaja mila kama ‘Kupimbira’, ambapo mabinti hulazimishwa kuacha shule na kuozeshwa kwa wazee ili kujipatia mahari, ‘Nhlanzi’ ambapo familia ya mke huozesha binti mwingine kwa mume wa binti yao kama zawadi kutokana na kuitendea wema familia husika, ‘Kulowa kufa’ mwanamke aliyefiwa na mume kuingiliwa kimwili na mwanaume mwingine ili kuondoa mkosi wa vifo kijijini, kwa kawaida shughuli hiyo hufanywa na mwanamume maalum wa kufanya shughuli hiyo. Mila hii pia inasemekana inafanyika hapa nchini hususana wilayani Ukerewe ambapo hujulikana kama ‘Kusomboka’, hii kwa hapa nchini hufanywa na wanaume na wanawake. Bi Mbale pia aliitaja mila ya ‘Fisi’ ambapo mume ambaye hana nguvu za kiume anamkodisha mwanume wa nje ili amuingilie mkewe kwa ajili ya kumpa ujauzito, lengo kuu ni kujipatia watoto.

Bi Mbale alikiri kupata ugumu katika kupiga vita mila hizi kutokana na usiri mkubwa uliokuwepo katika jamii hiyo ya watu waishio Kaskazini mwa Malawi.

Akizungumzia idadi ya mabinti waliiokolewa na taasisi yao tangu walipoanza kampeni ya kuwaokoa wanafunzi walioozwa kabla ya kumaliza masomo, Bi Mbale alisema kuwa wamefanikiwa kuwaokoa mabinti 40 waliokuwa na umri kati ya miaka 7 hadi 16 ambapo walirejeshwa shule na kuendelea na masomo.

Alisema kuwa, ingawa inakuwa ni vigumu kwa mabinti hao kurejea katika hali yao ya kawaida kabla hawajaolewa lakini huwapa ushauri nasaha hadi warejee kwenye hali zao za kawaida na kuendelea na masomo yao.

Habari hii nimeitoa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ukiwemo mtandao wa inteneti

15 comments:

Albert Kissima said...

Nampa pole huyo binti pamoja na wengine wote wanaokumbwa na madhila kama haya.


Jamii hii inahitaji elimu ya ziada ili kuiepusha na mawazo potofu ambayo wao wanaona ni maisha ya kawaida kabisa. Nasema maisha ya kawaida kwa kuwa yawezekana hata kuna baadhi ya mabinti ambao kwa namna moja ama nyingine huwa wanafurahia baadhi ya mila hizi au zote kabisa kwa sababu ya kutokuwa na namna mbadala ya kufikiri kuhusu mila hizo kwa sababu ya wigo wa kimila unaowapelekea kufikiria kuwa utaratibu huo ni wa kawaida na muhimu katika maisha yao.Wanaharakati wengi zaidi wanahitajika ktk eneo hilo ili washirikiane na waliopo ktk kuinasua jamii hii kwenye hali ya upofu waliyo nayo. Kuna jamii nyingi kama hizi Africa na ni jukumu letu sote kukabiliana na mila na tamaduni chafu kama hizi.Sote wenye nia njema tuwe wanaharakati.

MARKUS MPANGALA said...

ha ha ha ha hawa CHIPITA FORUMS sijui CHAPITA FORUMS au CHIDAPITA FORUMS. watajijuuuuuu.

NINA HAKIKA UNGEFANIKIWA KUISHI NA JAMII ZA WAMALAWI UNGEBLOGU HADI KUCHOKA AU UNGEANDIKA KIBATU CHENYE KURASA ELFU KADHAA,
nawaelewa we acha tu.

NSAMBE N'NUNGU, hao ndo AMI ABINGU WA MUTHARIKA

Yasinta Ngonyani said...

Nimesoma habari hii nikiwa na masikitiko sana. Ni jambo la kushangaza sana kumlazimisha binti aolewe na mwanamume ambaye ni sawa na babu yake kabisa. soma hhapa niliwahi kuweka makala kama hii pale kwangu. http://ruhuwiko.blogspot.com/2009/11/mwanaume-wa-miaka-112-amuoa-binti-wa.html

Unknown said...

Inasikitisha sana! Hii yote ni kwa sababu ya kutomjua Mungu. Watu kama hawa wanapaswa kufikiwa na Neno la Mungu wa Kweli.

MARKUS MPANGALA said...

Mungu ili afanyeje? yaani tukeshe makanisani na misikitini tukiimba PAMBIO kwamba Mungu awanusuru watu hao wakati alitupatia hekima na akili?

Huu mzaha, fanyeni utafiti siyo kulishana masikitiko. ha ha ha ha ha ha, Munguuuuu afanyeje? Neno la Mungu????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
Yaani tumefikiria weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee tumeshindwa kisha tunamrushia Mungu. Haya ni mambo ya imani siyo kujadili hoja

Anonymous said...

Dada Koero, leo ni siku ya kwanza kukutembelea humu. Nimeipenda sana blog yako. Nimeona umeandika sana kuhusu madhira ya mama zetu. Dada Koero mimi nakuunga mkono, maana I have lived this life. So I know it.

Swali langu kwako na wanawake wengine ni hili: Je ni kipi kifanyike KUPUNGUZA maana KUONDOA hii hali ni vigumu. Inaonekana wengi tunaliona tatizo na tumeishi na haya matatizo, lakini wote tunasema ni serikali ndo yenye jukumu! Mi nadhani we should be the change we seek!

Tuanze na jukumu la kuchagua viongozi responsible na tuwawajibishe. Leo hii CCM akijua kwamba hana majority bungeni ya kupitisha sheria anazozitaka kwa manufaa yake......trust me ..atakuwa na adabu jinsi anavyotuongoza, perhaps hela za ufisadi angeziweka kwenye mipango ya kuwawawezesha na si kuwasaidia hawa akina mama na wananchi kwa ujumla....

Tatizo kubwa kwetu sisi waafrika popote tulipo...tunapenda kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu. Ukiangalia kwa kiundani..hawa hawa unaowaonea huruma..ndo kesho utakuta wanaandamana kuipigia kura CCM! Sasa jamani..hivi mnategemea ukombozi wa mwafrika utatoka wapi? Mwenyezi MUNGU ALITUPA UTASHI lakini tunashindwa kuutumia. Do you really think Kikwete gives a damn to a dying villager down in Kwimba au Kigoma? only when he needs their votes!

Hapa tutakuja na excuse kibao..kwamba watu tunachagua viongozi wabovu kwa sababu ya umasikini, lakini tunashindwa kugundua kwamba..Politics is everything! whether you are in America or in poverty stricken Tanzania.

Narudia tena, waafrika..viongozi wetu wanatuchukulia for granted. Na sisi tumeridhika na hii hali.Na sisi tumekubali.. Hata the so called "elites"..ndo wanatuangusha..maana wakisha "toka" imetoka hiyo.....Hawaangalii nyuma....zaidi ya "kuwaonea huruma" waliobaki huko nyuma...

My take: Watanzania tuamke, tuchukue jukumu la maisha yetu. Tuache kumsingizia Mungu wala mwingine. HAITUSAIDII KULAUMU.

Dada Koero, Trust me..leo hata ungeteua 70% ya wabunge wote wakawa wanawake...hali za mama zetu hazitabadilika! Tunahitaji kubadilisha mfumo wa jinsi tunavyojitawala au tunavyotawaliwa. Imagine...mpaka leo hatuna umeme wa kuaminika..lakini hebu jiulize..tangu JK aingie madarakani..tumelipa mabilion mangapi kwa makampuni ya umeme hewa? and guess what? Everybody is quite! and in October we will vote in masses for the same messy!

Ofcourse, CCM siyo tatizo letu pekee..lakini..wakijua kwamba hata wananchi wanafikiria..hali itabadilika. For now..they know..they can do anything and go away with it. Mimi kiukweli...I get the feeling labda..ngoja umasikini uzidi kutuchapa weeeee (zaidi ya huu tulionao sijui itakuwaje ;-)...labda iko siku tutaamka na kuona kwamba we can influence things through the ballot!

Waungwana naomba nisiwachoshe..lakini..mimi kiukweli nchi yangu na wananchi wenzangu wananisikitisha sana...Tunashindwa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa yetu na watoto wetu. Umasikini na hali ngumu zinazowakabili mama na baba zetu utaendelea kudumu daima. Mpaka tutakapoamka na kusema INATOSHA!

God bless you all.

John Mwaipopo said...

alafu ooh binadamu ni kiumbe mwenye akili kuliko viumbe wengine. kwa hili i think we are more animals than humans. mwanamke aliyepevuka kibaolojia (na kiakili) anafaa kuolewa na mwanaume anayempenda au waliyependana. hili la kubambikiziwa babu kizee mie simo, mchanga wa pwani huooo.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Malawi...kama Tarime... :-(

Hivi ile NGO ya Koero na Yasinta inayoitwa Women Crying Every Day inafanya nini jamani? lol

Men RISE up!

Jacob Malihoja said...

Koero na wana blog wote ninawapa bigupp kwa michango mbali mbali lakini Mpangala ameniboa na amenitia wasiwasi. Katika mchango wake wa kwanza Mpangala anakatisha anaposema blogger (Koero) angechoka kuandika, maana yake ni nini? Kwamba asingeandika haya aliyotuletea au asirudie tenaa, hapa sielewi! Sentensi ya kwanza ya Mpangala inanitia hofu sana, maana neno utajijuu, mara nyingi hutamkwa na mtu ambaye amefanya jambo sasa anajibishana na mlalamikaji juu ya jambo alilolitenda! Mpangala anawaambia Chipita (Kimsingi na walalamikaji wote) watajijuu! Natamani kujua umri wa Mpangala, na natamani sana kujua umri wa mke wake kama ameoa! Kwasababu utajiju ni neon linalopendwa sana na kundi Fulani katika jamii yetu, na Maana ya neon hilo hasa hasa ni kwamba “ndio nishafanya utajijua mwenyewe”, au “ndio ishakuwa utajijua mwenyewe”!

Kwenye maoni yake ya pili, akijibu wazo la Bwana True Faith, Mpangala ameponda imani, yaani ameponda kabisa mchango wa kiroho katika kuttua matatizo ya kijamii! Hii pia imeniogopesha na kunishangaza. Kimsingi hata kama haamini Mungu lakini ukweli unabaki palepale mwenye elimu ya imani ya kiroho hawezi kufanya ushenzi kama huo. Lakini jambo lingine ni kwamba blog ni sehemu ya kubadilishana mawazo na kuonyesha hisia za kila mmoja. Lakini ni mahali ambapo kwa namna moja au zaidi kuna mmoja wa wasomaji anaweza akayafanyia kazi anayoyasoma, na yanayoendana nay eye au anayoyaweza.

Kwahiyo kama Mpangala anaona hana analoweza kuchangia kuhusu mambo ya kiroho akae kimya asiponde mchango wa wenzake. Pengine msomaji mmoja anaweza kwenda kuendesha elimu kubwa ya kiroho na mamo yakapungua huko! kama wewe unaweza kuishawishi Serikali kupeleka elimu fanya hivyo, anayeweza kushawishi polisi kukamata na kuwapeleka katika mkondo wa sheria, na afanye hivyo, anayeweza kushawishi watu wa imani wapeleke mafunzo ya kiroho na afanye hivyo. Huyu akipunguza wawili, huyu akipunguza kumi, huyu akipunguza watano kupitia njia anayoijua mwisho wa siku watu wengi wataondokana na ushenzi huo.

Kila mtu mchango wake unaweza kufanyiwa kazi kulingana na aina ya wasomaji wa mchango ambao mtu anautoa.

Hakuna vita inayotumia aina moja ya silaha.

MARKUS MPANGALA said...

Kaka Jacob Malihoja,
umenigusa sana na suala la umri wangu,na hongera kwa kuwa na miaka 38,NASHUKURU KUKUBOA TENA SANA.
nataka kukufafanulia kitu ambacho naamini hujakifahamu.

1. CHIPITA= ni kitu kinachopita.
2.CHAPITA= kitu kinachopita
3.CHIDAPITA=kitu kilichopita.
katika maoni yangu ya kwanza mwishoni nimeandika N'SAMBE N'NUNGU HAO NDO AMAI ABINGU WA MUTHARIKA.

yaani tuombe Mungu hao ndiyo akina mama wa Bingu wa Mutharika.

KUBLOGU HADI kuchoka ni kwamba haya mambo hayatakiwi tu kuzuka na kuyaandika sote tunatarajia kuona uhalisi unajadiliwa kwa kina na kuelezwa, hivyo kublogu hadi kuchoka kwani kuna mambo yanachekesha kwahiyo nayachukulia kama mzaha,
msingi wa kutenda ni uhitaji wa matendo ya mhusika. Huwezi kusema kwamba neno la mungu ndilo lilikosekana kwa hao watu kwa kujiangalia kwamba kwakuwa unalielewa na kulijua zaidi basi na wengine watashiriki.
NAACHA.....
soma maoni ya CHACHA na kile chama anachotania cha Da' Koero na Yasinta, ndipo utaelewa ninachoamini.
NIELENDELEE AU?
ni suala la fikra huru siyo kwamba nijiingize katika imani ambazo naamini kuwa suala la utetezi wa wanawake basi biblia ndiyo inanukuliwa kuhalalisha ukandamizaji wa wanawake.
Neno la mungu linasemaje katika huku ya adam na eva? AU nakosea na labda Mfalme Costantine na wenzake walichomokea halikuwa neno la mungu?
VIPI?
inawezekana suala la umri nalo ukaliona ni sababu ya mimi kuandika hayo, nakupa pass mark

Sula la mke wangu linakujaje hapa? ndiyo kujadili hoja huko? jadili mambo, jadili SERA ZA UKWMUAJI WA HAYA SIYO MALALAMIKO YASIYOKWISHA, mimi nasema suala la imani na utashi wa wanadamu siyo kila jambo linahitaji Mungu.

Ukishajua mke wangu....nini kitafuata?
NAMALIZA KWA KUCHEKA SANA.....
halafu...samahani mwenyekiti Koero kwa mcharazo ufuatao maana vikombora vya kufyatua matofali ya ubepari yamefika hapa.

SERA ZANGU KWA WANAWAKE.
tufanye nini tunapojadili hapa? Maana CHACHA ameshasema WOMEN CRYING EVERY DAY.

Leo nikae chini nikubali kuharibu katiba ya nchi ili kuweka uwiano sawa 50/50 kwa kusudio la upendeleo?
Ni nani alimpendelea mwanaume? SISI WANAUME NI WAJINGA?
JE HAO WAZEE NI WAJINGA? WAKENYA WANASEMA HIVI; MANENO MINGI KASI NDOGO
SI TUNAJUA UZEE NI BUSARA? UNAFIKIRI NI NINI KILICHOKOSEKANA KWA HAYA YOTE? MUNGU? atufanyie nini tena kwa miaka yote hii jamaniiiiii? tunamlilia kwa mambo mengine ambayo yanasbabishwa na watu ambao wamekosa kitu kidogo sana UTAMBUZI ndiyo maana nasema nawafahamu WAMALAWI siyo kwa kusimuliwa bali kwa kuishi na kuona ukiniambia suala la mungu Malawi nitakwambia nchi hiyo ni habari nyingine... tusiambukizane masikitiko...
HAPANA...
binadamu wana kawaida ya kujitisha, na kila wanachokiona wanajitia hofu, hilo ni anguko la kwanza. Pili tunatanguliza vikwazo ili tushindwe halafu tumuombe mungu.
Majuzi niliambiwa niende kwenye mkesha kuombea amani ya nchi.
NILICHEKA... na labda umri wangu ndiyo unanifanya nicheke..

WALIWAZA NINI HAWA KUOMBEA AMANI? ndiyo ushuhuda??
Nani anawapigia kura wanaoharibu amani?
Nani anawapa mamlaka wale wanaoanzisha asasi za kutetea wanawake, lakini hawafanyi hivyo.
AFADHALI KOERO WANGU ANAANDIKA KATIKA BLOGU NA KWA KUJITOLEA BILA MALIPO.... lakini nini wanachokifanya wale ambao wanafanya hayo kwa kulipwa pesa halafu wanashupalia habari za Mahita kuzaa na hausigeli

soma upya kwangu mimi ulishaisha zmaana ndiyo maana niliamua KUMJADILI KOERO MWENYEWE katika blogu yangu na nitafanya hivyo siku zijazo navuta pumzi..
wakati mwingine nichukulie tu vile unavyoamini na kujitisha kwa hofu... kumbuka nimeitwa jina la MCHARUKO kwasababu ya maoni yangu bloguni

umri wangu utaupata hapa ukinibipu ; lundunyasa@yahoo.com au jikomboe@gmail.com.

ASANTE KWA KUNISOMA; HII NI INJILI ILIVYOHUBIRIWA NA SHETANI MARKUS MPANGALA pale madhabahuni kwani asingelitambua dhambi kama Torati isingesema. na kwa umri wangu naenda kusikiliza WE MADE YOU ya EMINEM

Koero Mkundi said...

Mwe! naona mjadala umefikia patamu, hebu ngoja nimnukuu Annony wa tarehe 5 April 2010,

"Tatizo kubwa kwetu sisi waafrika popote tulipo...tunapenda kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu. Ukiangalia kwa kiundani..hawa hawa unaowaonea huruma..ndo kesho utakuta wanaandamana kuipigia kura CCM! Sasa jamani..hivi mnategemea ukombozi wa mwafrika utatoka wapi? Mwenyezi MUNGU ALITUPA UTASHI lakini tunashindwa kuutumia. Do you really think Kikwete gives a damn to a dying villager down in Kwimba au Kigoma? only when he needs their votes!"

Mwisho wa kunukuu.

Mwenzangu hapo umenikuna maana maoni yako ni makala tosha. Naomba uniruhusu niyatumie katika makala yangu ya Kisiasa ambayo iko jikoni.
karibu sana VUKANI.

MARKUS MPANGALA said...

@Koero; hata mimi nimedhamiria kutumia maoni ya Anony huyo, kwahakika ni kichwa safi. Lakini ukiniambia nisubiri pambio nitakwamba UNAWAZA NINI?

Hii ndiyo raha ya kujadili mambo yanachangamsha raaaaaaahhhhhhaaaa halafu unaongezea na Bakurutu ukinesanesa....

Natamani mjdala huu urudi tena kiambazani hapo au tuletee kingine chenye maudhui hayo tukijadili. Ndiyo uhuru na hatuvunji NYUMBA tunabomoa MLANGO tu. Mwenyekiti naomba kuiba maoni ya Anony huyo na ninaungaisha na ile mada yangu ya NAMJADILI KOERO J. MKUNDI

Jacob Malihoja said...

Mpangala, Wakunyumba! Nimekupata na Patriot yako! hata hivyo nimekusoma zaidi kupitia mtandao mwingine, na ni nimemezeshwa ufahamu wa kutosha juu yako. Nakupa Big Up. I apologize 4 my scud! By the way! natamani sana Likungu, Mbasa, Mbufu na Mbelele, mzee!

Anonymous said...

Dada Koero na wengine, mnaweza kutumia tuu hiyo quote..haina shida maana ni mawazo tuu.

Ukweli ni kwamba kama uko timamu Tanzania yetu itakuuma inavyoendeshwa na wale tuliowapa dhamana. Lakini tusiishie kuumia, lazima tuchukue hatua za kuibadilisha. Play your part. It can be done. Usimwangalie mwenzako. Its you! Naamini TANZANIA itabadilika kama watu tukitambua kwamba sisi ndo kiini cha mabadiliko. Kama mpiga kura, I ALWAYS believe mabadiliko yatakuja kwa njia ya amani and we can do that.

Kipindi cha kusingizia umasikini, ujinga nk..kimepitwa na wakati. We have to wake up and take full responsibility of our lives. Kwa nini lakini tunapenda mkato? kwa nini tunapenda kuonewa huruma? I believe Africa we aint genetically inferior kama wazungu baadhi wanavyoamini. Lakini matendo yetu na imani zetu zinatufanya tuonekane hivyo! Tutaendelea kurithishana umasikini mpaka lini? Naomba kila mtu ajiulize hili swali. Tangu uhuru..tunapigana na ADUI wale wale WATATU. Ujinga, Umaskini na maradhi! Imagine..next year we cerebrate HALF A CENTURY of INDEPENDENCE. What have we got to show for it? Inauma!

Mimi napenda kusali, lakini kamwe siamini kwamba Mungu atatuondolea matatizo yetu kwa kuomba. Rather, naamini Mungu atabariki juhudi Zetu kama tukifanya kazi inavyotakiwa! Huwezi kuiba/kufisadi hela ya kununua mitambo ya umeme, harafu unategemea kwenda kanisani Mungu akupe mvua! Jamani, why do we misuse our GOD?


Nitajitahidi kuwa nachungulia kwenye hii blog. Nimeipenda.

Koero Mkundi said...

Ndugu usiye na jina, maoni yako yatanifanmya leo nisilale kabisa kwani nishapata mada hapa ya kuandika.

Nimefarijika sana kuona kwamba umefurahishwa sana na kile ninachoandika humu japo kuna wanaoniona kama napoteza muda kwa kupiga taralila.

Niliwahi kusoma mahali kuwa moto uliosababisha chama cha KANU kule kwa majirani zetu nchini Kenya kuondolewa madarakani uliwashwa na Wanablog wa Kenya na hiyo ndio ikawa chachu ya kile kilichotokea nchini Kenya.

Ingawa kulitokea rabsha za hapa na pale lakini mpaka leo hii wengi mtakuwa mashahidi wa kile tunachokishuhudia nchini Kenya, wenzetu wameipigania katiba mpya kwa nguvu zote na sasa wako katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato….tuwaombee matakwa ya wananchi walio wengi yasikilizwe.

Lakini tofauti na hapa nchini kwetu, kuna matatizo ya mwamko wa watu kufuatilia habari za mtandaoni, sijui ni ukosefu wa ufahamu walionao wananchi walio wengi au nikutokana na kufinywa kwa teknolojia kutowafikia watu wengi hasa wa vijijini.

Tatizo lingine ni wachangiaji wengi kukimbilia kumjadili mtoa mada badala ya kujadili mada husika, hili ni tatizo kubwa ambalo kama mtu huna moyo kama wa mwendawazimu basi unaweza kuacha kublog na kukaa kimya,. Lakini kwa nini ukae kimya ilhali wapo watu wengi kwa maelfu ambao hunufaika na huu ujinga wetu humu?

Kwa nini mtu ambaye amesheheni mizigo yake kichwani akusababishe uache kutumia kipaji ulichopewa na Mungu tena bure kuwaelimisha watu na kuwakumbusha wajibu wao.

Kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili sisi wanablog, na tunachohitaji ni wachangiaji kama wewe ambao mnasoma mada na kuijadili kwa misingi ya kuamsha ari na shauku ya kuhoji kule haki zetu zilipofichwa na watu wachache ambao wametumia hila na ghilba kuingia madarakani.

What is ushindi wa kishindo? Kwa kutumia pesa za walipa kodi kuwalaghai watu ili kupata madaraka na kwa sababu ya ukosefu wa utambuzi walionao wananchi walio wengi hususana wa vijijini, halafu unapita na kukenua meno eti umepata ushindi wa kishindo.!!!!

Ngoja niishie hapa maana hii inahitaji mada inayojitegemea……