Wednesday, April 21, 2010

HEBU SOMENI UTAFITI HUU!



Tafiti nyingi zilizofanywa kuhusiana na upotezaji muda unaofanywa na waajiriwa ni kwamba, wafanyakazi maofisini huwa wanapoteza saa tatu kila siku katika kufanya mambo ambayo hayana maana kwa mwajiri au kwa kazi zao. Kwa wale ambao wana mitandao ya intenet maofisini mwao na wanaweza kuangalia kwa kadiri wanavyopenda hutumia dakika 54 kwa siku kuangalia mitandao hiyo.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 18 kila siku kuchungulia madirishani. Hata wale ambao viti na meza zao katikati ya ofisi, huwa wanasimama na kwenda kuchungulia madirishani mara kwa mara. Kwa wastani hutumia dakika 18 kutwa.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 14 kwa kwenda kujisaidia au kwa wanawake kwenda kujipamba au kujipodoa upya bafuni au vyooni. Ile nenda rudi ya kujisaidia au kujipodoa upya huchukua wastani wa dakika 14 kila siku. Kumbuka, kuna watu hujisaidia haja kubwa hata kwa dakika kumi.

Watumishi wa maofisini yaani wale ambao hukaa ofisini, hutumia dakika 35 kila siku kupiga soga zisizohusiana na kazi na pengine zisizo na maan sana. Soga zinazohusu mpira, siasa, ufuska, majungu na umbeya mwingine hutawala.

Halafu hutumia dakika 17 katika kunywa kahawa au chai na pengine soda. Inaweza kuwa wananywea kwenye mighahawa ya kazini au pale ofisini walipo. Wengine wakati wakiwa wanakunywa kahawa au chai hawagusi kazi kabisa.

Siku hizi maofisini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuteka mawazo au akili ya watumishi. Vitu kama mitandao, kuchati na simu zao za viganjani, viriba vya chai na kahawa vya kujichotea na mengine mengi yanafanya kujikuta mtumishi ameacha kazi na kuingia katika kitu kingine.

Lakini watumishi wengi wa maofisini hasa wale ambao wanatumia muda mwingi ofisini,inadaiwa kwamba, hawafanyi mazoezi. Hii inasababisha watumishi wengi wa kazi za aina hiyo kufa au kustaafu mapema kutokana na ubovu wa afya.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Jambo hili kwa kweli linapigwa vita sana kwa mfano hapa sweden kumepigiwa marufuku muda wa kuzi kuingia mtandaoni yaani mfano mzuri aliye na face book nk. Muda wa kazi basi ni kufanya kazi ni kweli watumishi wengi wanatumia muda huo kama ndio muda wa starehe. Nadhani tunakoenda huko kutakatazwa kabiasha komputa za kazi maofisini.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Source?

Binadamu siyo roboti, na japo sishabikii uzembe kazini (mf.kukaa kwenye facebook au kwenye mitandao kusaka mambo ya kikubwa), pia sipendi mfumo wa kibepari unaomwona binadamu kama mashine tu ya kuzalisha mali, huku ukipuuzia mahitaji yake ya kiroho, kimwili na kihisia.

Kuna ubaya gani kwa kimwana kwenda kujirembesha kama kufanya hivyo kutamwongezea morali, kumfanya ajisikie "fresh" na kuchapa kazi vizuri zaidi?

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Dah! Hata kusoma hapa nimepoteza dk kazaa tayari....lol


Wataalamu wanasema kuwa watu wanaolala mchana wakati wa kipindi cha mapumziko mchana a.k.a siesta hufanya kazi kwa ufanisi zaidi!!

Sijawahi kulala wakati huko hivo sijui utamu wake....lol

Ila kama takwimu ziko hivo inabidi tujiangalie namna tunavotumia muda wetu (time management)

Bennet said...

Kitu muhimu ni kufikia target zako ambazo umewekewa, lakini kuna kazi nyingine ni za kuhudumia watu moja kwa moja sasa hapo ukipoteza muda ndio unawachelewesha wateja

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh> itabidi tuwe tunafunga pampas na kumaliza haja humohumo ili tusipoteze muda